Kiungo nyota wa
kimataifa wa Ufaransa, Samir Nasri ameomba radhi kwa tabia yake lakini
amesisitiza kuwa hajaua mtu hivyo anapaswa kupewa nafasi nyingine ya
kujirekebisha. Kiungo
huyo anayecheza katika klabu ya Manchester City alifungiwa mechi tatu
na Shirikisho la Soka la Ufaransa kufuatia kumtukana mwandishi katika
michuano ya Ulaya 2012 na hajaitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya
nchi hiyo toka kipindi hiko. Hatahivyo
Nasri sasa yuko tayari kurejea katika mchezo wa kirafiki kati ya
Ufaransa na Ubelgiji baada ya kocha Didier Deschamps kuridhishwa na
tabia ya mchezaji huyo. Nasri
mwenye umri wa miaka 26 aliomba radhi kwa tukio alilofanya katika
michuano hiyo mwaka jana na kudai kuwa angetakiwa kukabiliana na tatizo
hilo kwa weledi zaidi kuliko alivyofanya. Nyota
aliendelea kudai kuwa anashukuru kupewa nafasi nyingine ya
kujirekebisha na ana mategemeo yaliyotokea hayatajirudia kwasababu hivi
sasa anajua jinsi gani ya kumudu hasira zake tofauti na ilivyokuwa
kipindi cha nyuma.