Sunday, February 9, 2014

SERIE A: JUVE YALAZIMISHWA SARE YA BAO 2-2 VS VERONA-TEVEZ ATUPIA

MBALI ya Juventus kutangulia kwa Bao 2 za mapema kupitia Carlos Tevez, Hellas Verona walijipanga na hatimaye kurudisha Bao zote na kupata Sare ya Bao 2-2 walipocheza na Mabingwa hao wa Italy ambao pia ni Vinara wa Serie A huko Italy.

Baada Tevez kupiga Bao 2, Luca Toni aliifungia Hellas Verona Bao la kwanza na Muargetina Juanito Gomez kusawazisha katika Dakika ya 94.

Baada ya hii Leo Timu ya Pili AS Roma nao kubanwa na kutoka Sare 0-0 Lazio, Juve wamebaki kileleni wakiwa Pointi 9 mbele ya AS Roma na wako Pointi 13 mbele ya Timu ya Tatu Napoli ambao waliifunga AC Milan 3-1 hapo Jana Jumamosi.

RATIBA/MATOKEO:

Jumapili Februari 9

Torino 1 Bologna 2

Lazio 0 AS Roma 0

Parma 0 Catana 0

Sampdoria 1 Cagliari 0

Livorno 0 Genoa 1

Hellas Verona 2 Juventus 2

2245 Inter Milan v Calcioa

MSIMAMO-Timu za Juu:

NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Juventus FC 23 19 3 1 56 18 38 60
2 AS Roma 22 15 6 1 45 11 34 51
3 SSC Napoli 23 14 5 4 47 27 20 47
4 Fiorentina 23 13 5 5 42 24 18 44
5 Hellas Verona 23 11 3 9 39 37 2 36
6 Inter Milan 22 8 9 5 39 27 12 33