WEKUNDU wa Msimbazi Simba imelala bao 1-0 jioni ya leo mbele ya Mgambo Shooting Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kwa
mara nyingine leo kipa Ivo Mapunda amefungwa bao rahisi, baada ya
kumtemea mpira mshambuliaji Fully Maganga dakika ya 29 kufuatia mpira wa
adhabu.
Wachezaji
wa Simba SC walipambana sana kujaribu kusawazisha bao hilo tangu hapo,
lakini Mgambo Shooting leo walisimama imara kuhakikisha wanaondoka na
pointi tatu.
Kwa
matokeo hayo, Simba SC inabaki na pointi zake 31 baada ya kucheza mechi
17, wakati Mgambo inatimiza pointi 12 na inaendelea kushika mkia.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dk57, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Awadh Juma/Uhuru Suleiman dk62, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amisi Tambwe na Ali Badru/Haroun Chanongo dk46.
Mgambo Shooting; Saleh Tendega, Bashir Chanache, Salim Kipaga, Bakari Mtama, Novaty Lufunga, Mohamed Samatta, Peter Mwalyanzi, Bolly Ajali, Fully Maganga Malima Busungu.