Saturday, April 5, 2014

BPL:CHELSEA YAKWEA KILELENI MWA LIGI HIYO:

MATOKEO:
Jumamosi 5 Aprili 2014
Man City 4 Southampton 1
Aston Villa 1 Fulham 2
Cardiff City 0 Crystal Palace 3
Hull 1 Swansea 0
Newcastle 0 Man United 4
Norwich 0 West Brom 1
Chelsea 3 Stoke 0
CLUB ya Chelsea imefanikiwa  kurudi kileleni mwa Ligi Kuu England baada ya hii Leo kuitandika Stoke City Bao 3-0 Uwanjani Stamford Bridge na kukalia nafasi hiyo wakiwa Pointi 1 mbele ya Liverpool na mbili mbele ya Man City walio Nafasi ya 3 lakini wao wamecheza Mechi 1 zaidi ya Liverpool na 2 zaidi ya City.
Goli la Kijana mahiri wa Misri, Mohamed Salah, ambae Leo ndio alianza Mechi ya Ligi kwa mara ya kwanza alipofunga katika Dakika ya 3.
Frank Lampard alifunga Bao la Pili katika Dakika ya 61 baada ya Penati yake kuokolewa na Kipa Begovic na mwenyewe kuitokea tena na kumalizia.
Penati hiyo ilitolewa kufuatia Mohamed Salah kuangushwa na Andy Wilkinson ndani ya Boksi.
Willian alipachika Bao tamu la 3 katika Dakika ya 72 kwa Shuti safi nje ya Boksi.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumapili 6 Aprili 2014
1530 Everton v Arsenal
1800 West Ham v Liverpool
Jumatatu 7 Aprili 2014
2200 Tottenham v Sunderland
MSIMAMO:
NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Chelsea 33 22 6 5 65 24 41 72
2 Liverpool 32 22 5 5 88 39 49 71
3 Manchester City 31 22 4 5 84 29 55 70
4 Arsenal 32 19 7 6 56 37 19 64
5 Everton 31 17 9 5 49 31 18 60
6 Manchester United 33 17 6 10 56 38 18 57
7 Tottenham Hotspur 32 17 5 10 40 44 -4 56
8 Southampton 33 13 9 11 50 44 6 48
9 Newcastle United 33 14 4 15 38 51 -13 46
10 Stoke City 33 10 10 13 37 48 -11 40
11 West Ham United 32 10 7 15 36 42 -6 37
12 Hull City 33 10 6 17 34 40 -6 36
13 Aston Villa 32 9 7 16 35 48 -13 34
14 Crystal Palace 32 10 4 18 23 39 -16 34
15 Swansea City 33 8 9 16 45 49 -4 33
16 West Bromwich Albion 32 6 14 12 37 48 -11 32
17 Norwich City 33 8 8 17 26 52 -26 32
18 Fulham 33 8 3 22 33 74 -41 27
19 Cardiff City 33 6 8 19 29 64 -35 26
20 Sunderland 30 6 7 17 28 48 -20 25