Wednesday, April 30, 2014

MALAWI KUTUA NCHINI KESHO MEI 1 MWAKA HUU.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Mrisho Ngassa (kushoto) akiangalia namna ya kumtoka mlinzi wa timu ya Taifa ya Mawali, Wisdom Ndhlovu wakati timu hizo zilipochuana katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa katika uwanja mpya wa taifa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Henry Joseph wa Taifa Stars. (Picha na Mroki Mroki).TIMU ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kuwasili nchini kesho Mei 1 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Mei 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Flames yenye msafara wa 31 utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu cha Malawi (FAM) utaingia Mbeya kwa usafiri wa barabara. Wachezaji katika msafara huo ni 20.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha mpya, Mart Nooij tayari ipo jijini Mbeya kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.