Taifa stars ya Mart Nooij itakabiliana na Msumbiji
katika mchezo wa mwisho wa mtoano kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka
tiketi ya fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morroco.
Hii imeto
kana na sare ya 2-2 waliyopata jioni hii
dhidi ya wenyeji wao, timu ya taifa ya Zimbabwe.

Zimbabwe walioripotiwa kuwafanyia hujuma vijana wa
Tanzania wameambulia patupu leo hii baada ya kuoneshwa soka safi na vijana wa
Tanzania.
Haikutegemewa kuwa mechi ya mabao mengi kiasi hiki,
lakini Zimbabwe ndio walianza kuamsha `mizimu` ya vijana wa Taifa stars
waliokuwa wanamtazama kiongozi wao wa msafara, Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwa
jukwaani.
Bao la dakika ya 10 walilopata Zimbabwe kupitia kwa
Phiri Danisa liliwashitua mashabiki wa Tanzania, lakini nahodha wa Taifa
Stars, Nadir Haroub Canavaro katika dakika ya 21 aliwazisha bao hilo na
kuufanyaubao wa matangazo kusomeka 1-1 mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Wakati Zimbabwe wakiwa katika presha ya kusaka bao
la pili, dakika ya 46 kipindi cha pili walifanya makosa na Thomas Emmanuel
Ulimwengu hakufanya makosa na kuwaadhibu goli la pili.
Dakika ya 55 kipindi hicho cha pili, Katsande
Willard aliifungia Zimbabwe bao la pili la kusawazisha.
Baada ya hapo mpira ulianza kuchezwa kwa timu zote
kutafuta mabao zaidi, lakini wenyeji ndio walikuwa kwenye presha kubwa zaidi
kwasababu tayari Stars walikuwa na mtaji wa mabao zaidi.
Taifa stars ya Mart Nooij ilionesha kiwango safi na
upinzani mkubwa ugenini na kuwafurahisha watanzania wachache waliokuwa uwanjani
na waliokuwa wanaangalia kupitia televisheni.
Haikuwa kazi nyepesi kwa vijana wa Tanzania kuwafunga Zimbabwe, lakini jitihada kubwa walizofanya na kutambua kuwa mamilioni ya watanzania wapo nyuma yao, ilitosha kuwapa morali kubwa.
Haikuwa kazi nyepesi kwa vijana wa Tanzania kuwafunga Zimbabwe, lakini jitihada kubwa walizofanya na kutambua kuwa mamilioni ya watanzania wapo nyuma yao, ilitosha kuwapa morali kubwa.

Canavaro amekuwa kiongozi wa kuigwa kwani alionesha
ushupavu wa kuwaelekeza njia wenzake ikiwemo kufunga bao muhimu la kusawazisha.
Beki kazi yake ni kulinda, inapofika wakati
anafunga, basi amejiongezea majukumu kwa lengo la kuisaidia timu yake ipate
mafanikio.
Kuwa nahodha sio kuvaa kitambaa tu bali ni pamoja na
kuisaidia timu kama wanavyofanya akina Sergio Ramos.
Kazi nzuri
Nadir Haroub `Canavaro`.
Ulimwengu ni mchezaji wa TP Mazembe. Kuna faida ya
kuwa na wachezaji wa kimataifa kama yeye. Kudhihirisha umuhimu wake, alifunga
bao safi na kuwavusha watanzania hatua inayofauta. Kazi nzuri kijana.
Kwa matokeo ya leo, Taifa stars imefuzu hatua ya
mwisho ya mtoano kwa wastani wa mabao 3-2 kuwania kupangwa hatua ya makundi
kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika.
Hii inatokana na ushindi wa bao 1-0 iliopata uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa kwanza na matokeo ya 2-2 mjini Harare jioni hii.
Hii inatokana na ushindi wa bao 1-0 iliopata uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa kwanza na matokeo ya 2-2 mjini Harare jioni hii.
Kwa maana hiyo, Taifa Stars inajiandaa kuutafuna
mfupa wa Msumbiji katika hatua ya mwisho ya mtoano.
Msumbiji walifuzu hatua hiyo kwa wastani wa mabao
5-0 baada ya juzi kutoka suluhu ya bila kufungana na Sudan Kusini Ugenini,
wakati waliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 mjini Maputo.
Msumbiji wana historia ya kuwaharibia Taifa stars
katika michezo muhimu ya mashindano, hivyo ni jukumu la wachezaji na kocha
Nooij kupanga mikakati kabambe ya kuwanyamazisha `Mamba hao weusi`.
Mechi nyingine iliyomalizika jioni hii ni baina ya
Lesotho na Liberia na kushuhudia Lesotho wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kikosi chaTaifa Stars;
Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mwinyi Kazimoto, Simon Msuva/Said Mourad
dk78, Amri Kiemba/Frank Domayo dk62, John Bocco, Thomas Ulimwengu/Mrisho
Ngassa dk88 na Erasto Nyoni.
Jumapili Juni 1
Zimbabwe 2 Tanzania 2 [2-3]
Lesotho 2 Liberia 0 [2-1]
14:30 Congo v Namibia [0-1]
15:00 Benin v Sao Tome And Principe [2-0]
15:00 Chad v Malawi [0-2]
16:00 Equatorial Guinea v Mauritania [0-1]
Nchi ambazo zimeingia Makundi moja kwa moja: Nigeria,
Ghana, Ivory Coast, Zambia, Burkina Faso, Mali, Tunisia, Algeria,
Angola, Cape Verde, Togo, Egypt, South Africa, Cameroon, DR Congo,
Ethiopia, Gabon, Niger, Guinea, Senegal and Sudan.
KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Taifa stars vs Msumbiji
|
Mechi ya kwanza 18–20 Julai |
mechi ya pili1–3 Agosti |