GOLIKIPA wa Arsenal,
Lukasz Fabianski amekubali kujiunga na Swansea City wakati mkataba wake
na klabu hiyo utakapomalizika mwezi ujao. Golikipa huyo wa kimataifa wa
Poland alikataa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ili kumzuia asiondoke
na sasa ameamua kuhamia katika Uwanja wa Liberty unatumiwa na
Swansea. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao, Arsenal
walithibitisha kuondoka kwake na kumshukuru golikipa huyo kwa mchango
wake aliotoa katika kipindi ch
ote alichokuwepo na kumtakia kila la kheri
huko anapokwenda. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na
Arsenal akitokea Legia Warsaw mwaka 2007 na kucheza mechi 78 katika
kikosi cha kwanza katika mashidano toka alipojiunga nao.