MAOFISA wa klabu ya
Arsenal, wamesafiri kwenda Hispania kwa matumaini ya kumamilisha dili
kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata.
Mshambuliaji huyo amekuwa akiwindwa na Arsene Wenger kwa muda mrefu na
klabu imeamua kuanza harakati za kumsajili nyota huyo mwenye miaka 21
mapema, kwani Juventus nao pia wanamuwinda.
Madrid wako tayari kumuuza
lakini wanatarajiwa kusisitiza kutaka dau lao walilomnunulia kitu
ambacho kinaonekana kitakuwa kigingi kikubwa kwa timu
zinazomuhitaji. Arsenal walijaribu kumsajili kinda huyo wa kimataifa wa
Hispania majra ya kiangazi mwaka jana na safari hii wanaamini uhakika wa
kupata namba katika kikosi cha kwanza atakaoupata utawasaidia kumvutia
kwao. Morata amefunga mabao tisa katika mechi 28 alizocheza akiwa na
Madrid msimu huu na alitokea benchi katika mchezo wa fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya uliofanyika Jumamosi na kuisadia timu yake
kuisambaratisha Atletico Madrid. Arsenal pia wanamtaka mshambuliaji
mwingine wa Madrid Karim Benzema lakini Carlo Ancelotti anamtaka nyota
huyo wa kimataifa wa Ufaransa kusaini mkataba mpya na timu hiyo.