Klabu ya TP Mazembe hatimaye imewaruhusu wachezaji wake Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kujiunga na timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo tayari imewasili Harare, Zimbabwe kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika.

Taifa Stars itacheza na Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ katika mechi ya marudiano raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Mechi hiyo itachezwa
Jumapili (Juni 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Harare.Samatta na
Ulimwengu watawasili Harare kesho Saa 3.40 usiku kwa ndege ya Kenya Airways na
watajiunga na TP Mazembe mara baada ya mchezo huo ambapo Juni 2 mwaka huu,
wakienda moja kwa moja Ndola, Zambia ambapo timu yao imepiga kambi kwa ajili ya
mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek Juni 7.