
Mkutano
Mkuu wa Wanachama wa mabadiliko ya baadhi ya Vipengele kwenye Katiba
utafanyika siku ya jumapili Juni Mosi 2014 katika Ukumbi wa Bwalo la
Polisi - Oysterbay kuanzia majira ya saa 3 kamili asubuhi huku wanachama
wote hai wa klabu ya Young Africans wakiombwa kujitokeza kwa wingi.
Akiongea na waandshi wa habari makao
makuu ya klabu, Afisa Habari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto
amesema mkutano huo wa siku ya jumapili ni kwa ajili ya marekebisho ya
katiba kama maagizo ya Shirikisho la Soka nchini TFF ilivyoagiza.
"Jumapili
tunafanya makutano wa marekebisho ya katiba lengo ni kuhakikisha
wanachama wanapata nafasi ya kutoa maoni yao na kupitisha hivyo
vipengele ambavyo vitapelekea Yanga kupeleka katiba yake TFF na kisha
kwa msajili ili shughuli zote za klabu ziweze kufanyika kwa kufuata
katiba mpya" alisema Kizuguto.
Mara baada ya mabadiliko hayo
nadhani tutakua tayari kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi kwani
tulikuwa tunasubiria marekebisho ya Katiba tu, TFF na msajili
wakishaiptisha Katiba basi tutakua tayari kuelekea kwenye Mkutano Mkuu
wa Uchaguzi wa Viongozi.
Watakoruhusiwa kuhudhuria mkutano mkuu
siku ya jumapili ni wanachama wa Yanga SC walio hai tu, kwa maana ambao
wamelipia ada zao za uanachama mpaka kufikia kwa mwezi ujao wa Juni
2014.
Wanachama ambao bado hawajalipia Ada zao za uanchama
wanaombwa kulipia mapema kabla ya siku ya mkutano, malipo yote
yanafayika kwenye Idara ya Fedha makao makuu ya klabu kila siku muda wa
kazi na siku ya jumamosi saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana.