Maafande wa Jkt Ruvu kutoka kibaha mkoani pwani kushuka kitaanza Ligi Kuu Bara bila ya wanandinga wake saba wa kikosi cha kwanza.
Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Felix Minziro, amethibitisha kutokuwepo kwa wachezaji hao ambao wamekwenda kushiriki michuano ya Majeshi ya Afrika Mashariki iliyokuwa ikifanyika mjini Zanzibar.
Wachezaji wangu takribani saba wa kikosi cha kwanza, hawapo kwa sasa, hili linanipa wakati mgumu sana.
Minziro amesema ligi inaanza siku ya Jumamosi, uwepo wao una mchango mkubwa katika timu na wako Msumbiji kwa sasa kulitumikia jeshi katika masuala la michezo.