Monday, September 15, 2014

WEKUNDU WA MSIMBAZI WAREJEA ZANZIBAR KUWEKA KAMBI KWA MARA YA PILI.

Klub ya simba wekundu wa Msimbazi , Simba SC wamerejea tena Visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya ligi kuu soka  Tanzania bara inayotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu.
20140913_160508Simba chini ya kocha Mzambia Patrick Phiri wataanza kampeni za kusaka ubingwa walioukosa kwa misimu miwili dhidi ya Wagosi wa ya, Coastal Union, septemba 21 mwaka huu uwanja wa Taifa , Dar es salaam.
Hii itakuwa mara ya pili Simba kujificha Zanzibar kwa sabababu ilikuwa huko kabla ya kuja Dar es salaam kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, septemba 6 mwaka huu uwanja wa Taifa na kuitandika 3-0.
Ijumaa ya wiki iliyopita, Simba ilicheza mechi ya pili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya URA ya Uganda na kulala bao 1-0.
jumamosi ya wiki iliyopita, Simba ilisafiri kwenda Mtwara ambapo ilicheza mechi ya kirafiki na Ndanda fc katika uwanja wa Nangwanda Sijaona na kutoka suluhu pacha ya bila kufungana.
Baada ya mechi hiyo, jana wachezaji walipewa mapumzikio, na leo jumatatu wanaanza mazoezi kabla ya kuelekea Zanzibar.
Simba wamekuwa wakiijenga timu upya chini ya kocha Phiri na usajili wao unawafanya wapinzani wawe na wasiwasi.
Wachezaji wa kigeni waliopo Simba wameonekana kuwa na ubora wa kutosha, hivyo kujenga imani kwa mashabiki wao.
Warundi, Amissi Tambwe, Pierre Kwizera, Mkenya, Paul Kiongera na Waganda Joseph Owino na Emmanuel Okwi wameonekana kuwa na msaada mkubwa kwa Simba.
Pia wapo wazawa waliosajiliwa kama, kipa Hussein Sharrif, Shaaban Kisiga, Elius Maguli,Joram Mgeveke, Tshabalala, na wengineo.
Wachezaji hawa wameonakana kuelewana na kucheza mpira mzuri kama walivyoonekana kwenye mechi dhidi ya Gor Mahia na URA.