Tuesday, September 9, 2014

STAND UNITED YAPATA UDHAMINI WA MWAKA MMOJA

klabu ya Stand United imeingia mkataba na Beki ya Exim Tanzania udhamini wa mwaka mmoja na inayojiandaa kushiriki ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 unaotarajia kuanza septemba 20 mwaka huu.
Stand United yenye makao makuu yake Mkoani Shinyanga itaanza kampeniza zake nyumbani kwa kuvaana na wageni wenzao wa ligi kuu, Ndanda fc kutoka Mtwara.
Taarifa zanaeleza kuwa katika mkataba hao, Stand United watalamba milioni 10 za Kitanzania.
Huu ni udhamini wa pili kwa klabu hiyo kwani tayari walishalamba udhamini wa kampuni ya Binslum sambamba na klabu za Mbeya City na Ndanda fc ya Mtwara.
Kwa maana hiyo, Stand United watakuwa wanakusanya fedha za udhamini kutoka Binslum, Azam TV na Benk ya Exim Tanzania.
Hivi karibuni wachezaji wa Stande United waliripotiwa kugoma kufanya mazoezi wakishinikiza kulipwa mishahara, lakini uongozi ukafafanua kuwa kuna mahali kulitokea tatizo na fedha zipo.
Viongozi hao walikiri kufanya uzembe na walifanikiwa kumaliza tatizo.
Kwa udhamini huu, Stand United watakuwa na uwezo wa kufanya mambo ya msingi klabu kwao.