Mbrazil, Emerson Roque ambae anacheza nafasi ya Kiungo leo ameanza kujifua katika kikosi cha Yanga.
Taarifa zilizopo Emerson atafanya majaribio kwa wiki mbili, ambapo leo imekuwa siku ya kwanza.
Emerson ambaye inaelezwa atachukua nafasi ya mshambuliaji, Jaja alionekana kama vile amezoeana na wachezaji wengine wa Yanga.
Pamoja naye, kiungo Coutinho na Kocha Marcio Maximo, nao walianza mazoezi yao kwa mara ya kwanza baada ya kurejea nchini, jana.