Mwenyekiti wa timu hiyo Abuu Changawa amesema wamefikia hatua hiyo baada ya timu yao kuwa na mwendo wa konokono katika ligi hiyo wakiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi A.
Pamoja na kwamba wapo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi letu, matokeo ya timu yetu hayaridhishi. Tumekuwa tukishinda 1-0 na kutoka sare ndiyo maana tumeaona tuachane na watendaji wote wa benchi la ufundi,” amesema Majeki.
Lipuli FC, aliyowahi kuifundisha Shadrack Nsajigwa (sasa kocha msaidizi Yanga), imekusanya pointi 21 katika mechi zote 11 za raundi ya kwanza ya FDL, pointi moja nyuma ya Friends Rangers walioko nafasi ya pili na tatu nyuma ya Majimaji FC wanaoshika usukani wa kundi hilo.
Aidha, Majeki amesema kuanzia Alhamisi wataanza msako wa kukamata watu wote wanaojihusisha na biashara haramu ya kutengeneza na kuuza jezi zenye nembo ya klabu yao kwa kuwa hadi sasa hakuna kampuni wala mtu aliyeidhinishwa kutengeneza na kuuza jezi zenye