Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza
wachezaji
watakaotumika katika mechi ya Bonanza ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba
dhidi
ya Yanga lazima wawe wale waliosajiliwa kwa mujibu wa kanuni.
Yanga au Simba hazitaruhusiwa kumtumia mchezaji
yoyote ambaye
hayuko kwenye usajili wakati wa mechi hiyo ya Oktoba 13 kwenye Uwanja wa
Taifa
jijini Dar.
Maana yake, Simba haitaweza kumtumia kiungo wake
Mgambia, Omar
Mboob hadi hapo itakapomsajili.
Kama itamsajili, itawakosa mmoja kati ya Amissi
Tambwe au Pierre
Kwizera ambao italazimika kuwatema.
Hadi sasa inaonekana Simba bado inamjaribu, hivyo
haitakuwa rahisi
kupata uhakika wa kumsajili hadi Desemba.
Hata hivyo, Mboob atapata nafasi nyingine ya
kuonyesha uwezo wake,
kesho kwenye Uwanja wa Taifa wakati Simba itakapoivaa Express ya Uganda.