Tuesday, May 14, 2013

UFAFANUZI KUHUSU LIGI YA MABINGWA MIKOA

LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) ilianza tarehe 12 Mei 2013 ikishirikisha klabu bingwa za mikoa yote ya Tanzania Bara, isipokuwa mikoa ya Pwani na Manyara ambayo kutokana na sababu tofauti ilishindwa kuwasilisha majina ya klabu zake hadi siku ya mwisho iliyowekwa na Kamati ya Mashindano, yaani tarehe 10 Mei 2013.

Suala la kukosekana kwa wawakilishi wa mikoa hiyo miwili limezua maswali mengi kiasi kwamba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linalazimika kutoa ufafanuzi kwa faida ya wadau wote wa mpira wa miguu.

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa, ambayo ni mpya baada ya TFF kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa mpira wa miguu, ilipangwa kuanza tarehe 5 Mei 2013, lakini hadi tarehe ya mwisho ya kuwasilisha majina ya mabingwa wa mikoa, yaani tarehe 2 Mei 2013 mikoa michache ndiyo iliyokuwa imemaliza ligi zao na kupata mabingwa.

Kuchelewa huko kwa mikoa kumaliza ligi zao kuliilazimisha Kamati ya Mashindano ya TFF kuongeza muda wa mikoa kuwasilisha majina ya wawakilishi hao hadi tarehe 10 Mei 2013 na hivyo siku ya kuanza kwa Ligi kusogezwa mbele hadi tarehe 12 Mei 2013.

Hadi kufikia tarehe hiyo mpya ya mwisho ya kuwasilisha majina ya mabingwa wa mikoa, ni mikoa sita tu iliyofaidika na kuongezwa huko kwa muda na kupata wawakilishi wake. Mikoa hiyo ni Iringa, ambayo pamoja na kuongezwa kwa muda, iliandika barua ya kuihakikishia Kamati ya Mashindano kuwa itapata bingwa kabla ya kuisha kwa siku ya tarehe 10 Mei 2013.

Mikoa mingine ni Lindi, Mtwara, Geita, Tabora na Dodoma.
Mkoa wa Manyara haukuweza kumaliza ligi yake hadi mwisho wa siku ya tarehe 10 Mei 2013 na hivyo Kamati ya Mashindano iliyosubiri majina hadi saa 12:00 jioni siku hiyo kuamua kuwaondoa wawakilishi wa Manyara kwenye ratiba.

Awali, Kamati ya Mashindano iliamua kuwa ratiba ya mechi za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa ipangwe tarehe 7 Mei 2013, ikishirikisha mikoa ambayo ilishapata mabingwa wake, lakini baada ya kuona baadhi ya mikoa ilikuwa haijakamilisha ligi zake, Kamati iliamua kuwa ratiba ipangwe kwa kutumia majina ya mikoa kwa matumaini kuwa hadi kufikia tarehe 10 Mei 2013, mikoa itakuwa imeshapata wawakilishi wake na kwa kuwa ratiba inahusu mikoa jirani, ingekuwa rahisi kwa timu kusafiri kutoka kituo kimoja hadi kingine.

Lakini Mkoa wa Manyara haukuweza kufanya hivyo na Kamati kulazimika kuuondoa kwenye ratiba kutokana na kushindwa kukidhi utashi huo.



Mkoa mwingine ambao uliondolewa kwenye ratiba ni Pwani ambayo pamoja na kutuma jina la mwakilishi wake, Kamati ilipokea malalamiko kutoka klabu zilizoshiriki Ligi ya Mkoa, zikidai kuwa jina la bingwa wa Pwani lililowasilishwa TFF lilikuwa batili kwa kuwa klabu ya Kiluvia United haikustahili kushiriki Ligi ya Mkoa kutokana na ukweli kuwa haijasajiliwa mkoani Pwani na wala haikushiriki ligi ya mkoa msimu uliopita. Kamati ya Mashindano iliiondoa Pwani kwenye ratiba na kulirudisha suala hilo mkoani.

Ingawa Katibu wa Pwani alijaribu kuishawishi Sekretarieti ya TFF iliangalie suala hilo kwa undani zaidi, Sekretarieti ilimjibu kuwa lilishafanyiwa uamuzi na Kamati, hivyo uamuzi huo usingeweza kutenguliwa na kumshauri katibu huyo arejee mkoani kwake kuwasiliana na viongozi wenzake kuona ni jinsi gani mkoa unaweza kunusuru hali hiyo kwa kufanya uamuzi ambao ungeuwezesha mkoa kupata mwakilishi.

Kwa mantiki hiyo, masuala ya Manyara na Pwani yalikuwa ndani ya uongozi wa mikoa husika na si Kamati ya Mashindano ya TFF kwa kuwa Kamati ilitaka ipatiwe jina la bingwa ambaye alipatikana kwa mujibu wa mfumo mpya wa Ligi ya Mikoa.

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa inachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini na hivyo timu zilizokutana tarehe 12 Mei 2013, zitarudiana mwishoni mwa wiki hii na kupatikana timu zitakazosonga mbele kwenye raundi nyingine hadi timu tatu bora zitakazopanda daraja kwenda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zitakapopatikana.

Ligi za Mikoa, kwa mujibu wa kanuni mpya, zinatakiwa ziwe na timu kati ya 16 na 20 na zinatakiwa zicheze mechi mbili za nyumbani na ugenini, hata kama zitakuwa zinatumia uwanja mmoja.

Uamuzi wa kubadilisha mfumo huo ulifanywa ili kuhakikisha kuwa mikoa inakuwa na na mashindano kwa mwaka mzima na hivyo kuiwezesha mikoa kujikita katika kutafuta mbinu za kupata fedha na kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu kwenye mikoa yao.

Uamuzi huo pia unasaidia kupunguza mtindo wa wachezaji kuzunguka klabu tofauti katika msimu mmoja kwa kuwa wanalazimika kutulia kwenye klabu moja hadi muda wa usajili unapofika.

Pamoja na wachezaji kutulia sehemu moja kwa muda mrefu, pia walimu wanapata fursa ya kujikita vizuri kwenye programu zao kwa kuwa wanakuwa na uwezo wa kufuatilia maendeleo ya wachezaji wao.


Pamoja na hayo yote, mfumo huo utasaidia kurudisha msisimko kwenye mikoa na hivyo kutoa fursa kwa vijana wengi wenye vipaji kuonekana na kuendelezwa.

TFF inatoa wito kwa viongozi wa mikoa kuanza kubuni sasa mikakati ya kuendesha ligi hizo msimu unaokuja kwa kuwa hakutakuwa na nafasi tena ya kuongeza muda kwa mikoa kuwasilisha majina ya wawakilishi wao.

KIINGILIO MECHI YA SIMBA, YANGA 5,000/-
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Mei 18 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000. Kiingilio hicho kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.

Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 30,000.  

Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni.

Mwamuzi wa mechi hiyo atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro ambapo atasaidiwa na Samuel Mpenzu wa Arusha, na Jesse Erasmo kutoka Morogoro. Mwamuzi wa akiba ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.

Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Leslie Liunda.

KOCHA KIM KUZUNGUMZIA MECHI YA MOROCCO
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya tiketi kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco. Mkutano huo utafanyika keshokutwa (Mei 16 mwaka huu) saa 5 kamili kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Mechi hiyo ya kundi C itachezwa Juni 8 mwaka huu kwenye jiji la Marrakech nchini Morocco. Taifa Stars ilishinda mechi yake iliyopita jijini Dar es Salaa kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Morocco.

Angetile Osiah
Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

ROBERTO MANCINI HUYOO NJE ATUPIWA VIRAGO MAN CITY


Wakisheherekea ubingwa wao Timu ya Manchester United huku ikimuaga kwa kila heri Meneja wao Sir Alex Ferguson baada ya Miaka 26 ya Utumishi uliojawa na furaha tele kwa Jumapili walikabidhiwa Kombe la Ubingwa England na Jumatatu Jioni wakizunguuka nalo Mitaa ya Jiji hilo  kwa Maandamano ya furaha kubw lakini upande wa pili wa Manchester City mekuwa na majonzi makubwa  baada ya kuukosa Ubingwa na Juzi kukosa FA CUP walitandikwa na Wigan kwenye Fainali, na hili leo kilio chao kuhitimishwa kwa  Meneja wao Roberto Mancini kutupiliwa virago katika timu hiyo.
kitu kilichopelekea kutimuliwa kazi kwa Roberto Mancini alidumu kwa Miaka mitatu na nus, tamko la Klabu lisema: manchin Ameshindwa kutimiza malengo ya Klabu Msimu huu ukiachia kufuzu kucheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Klabu hiyo imesema Meneja Msaidizi, Brian Kidd, ambae alishawahi kuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson huko Man United, ndio atakaimu nafasi hiyo kwa Mechi zao mbili za BPL zilizobaki za Msimu huu na pamoja na Ziara yao ya kabla ya Msimu mpya kuanza ya huko Marekani.
MANCINI_n_BALOTELLI-MSHIKEMSHIKERoberto Mancini alitwaa kibarua Man City Desemba 2009 alipotimuliwa Mark Hughes na kuiongoza kutwaa FA CUP Mwaka 2011 na Ubingwa wa England 2012 lakini mara baada ya Jumamosi kufungwa Fainali ya FA CUP Bao 1-0 na Wigan kipigo ambacho kinafuatia kupokonywa Ubingwa wao na Mahasimu wao Man United, Mancini alionekana kukalia kuti kavu baada ya kumaliza Msimu huu mikono mitupu.
Mara baada kufungwa na Wigan kwenye FA CUP, Mancini alikurupuka na kuulaumu uongozi wa Man City kwa kutokanusha uvumi wa Pellegrini, Raia wa Chile, kuja kutwaa kazi yake.
aidha baadhi ya Wachambuzi huko England wamemponda Mancini na kudai hana haki ya kuilaumu Man City kwani hata yeye alipoteuliwa kwenda Klabu hiyo Mark Hughes alikuwa bado Meneja.
hata hivyo ingawa Mancini aliiwekea Man City historia nzuri ya kutwaa Kombe lao la kwanza baada ya
Miaka 35 walipotwaa FA CUP na kutwaa Ubingwa wao wa kwanza baada ya Miaka 44, kumaliza Msimu huu kwa ukame kunadaiwa kuwakera Wamiliki Matajiri wa Man City toka Falme za Nchi za Kiarabu ambao Jumamosi walikuwa Wembley kushuhudia Timu yao ikitwaa Kombe kwa mgongo wa ‘vibonde’ Wigan lakini wakajikuta chali baada ya kutunguliwa Bao 1-0 na Kombe la FA CUP kwenda Wigan, Timu ambayo huenda Msimu huu ikaandika Historia ya kuwa Klabu ya kwanza kutwaa FA CUP na kushushwa toka Ligi Kuu Msimu huo huo.
Kocha ambaye anatarajiwa kuchukuwa mikoba ya  manchin ni Manuel Pellegrini, Kocha wa Malaga ya Spain raia wa Chile, atapewa wadhifa wa kumrithi Mancini ingawa mwenyewe amesisitiza hayo si kweli.

Monday, May 13, 2013

MFAHAMU KWA UZURI DAVID BECKHAM KATIKA HARAKATI ZA SOKA.

                                    David Beckham
David-Beckham3.jpg
Taarifa kuhusu yeye
Full nameDavid Robert Joseph Beckham
Date of birth2 May 1975 (age 38)
Place of birthLeytonstoneLondon, England
Height6 ft 0 in (1.83 m)[1]
Playing positionMidfielder
Timu ya sasa
Current clubParis Saint-Germain
Number32
Youth career
Tottenham Hotspur
Brimsdown Rovers
1991–1993Manchester United
Timu za ukubwa
MwakaTimumechi(Goli)
1993–2003Manchester United265(62)
1994–1995→ Preston North End (loan)5(2)
2003–2007Real Madrid116(13)
2007–2012Los Angeles Galaxy98(18)
2009→ Milan (loan)18(2)
2010→ Milan (loan)11(0)
2013–Paris Saint-Germain9(0)
Timu ya taifa
1992–1993England U183(0)
1994–1996England U219(0)
1996–2009England115(17)


MATAJI ALIOTWAA KUPITIA KLABU HIZI
MANCHESTER UNITED
Ligi kuu (6): 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03
Kombe la fa (2): 1995-96, 1998-99
Fa community shield (4): 1993, 1994, 1996, 1997
Fa cup vijana (1), 1991-1992
Ligi ya mabingwa (1), 1998-1999
Intercontinental cup (1), 1999
REAL MADRID
La Liga (1), 2006-07
Supercopa de España (1): 2003
LOS ANGELES GALAXY
Ligi Kuu ya Soka Kombe (2): 2011, 2012
Shield MLS Wafadhili '(2): 2010, 2011
Ligi Kuu ya Soka Magharibi Mkutano
Washindi (mara kwa mara na msimu) (3): 2009, 2010, 2011
Washindi (Playoffs) (3): 2009, 2011, 2012
PARIS SAINT-GERMAIN
Ligue 1 (1): 2012-13
KIMATAIFA TIMU YA TAIFA.
Uingereza
Tournoi de France: 1997
FA Summer mashindano: 2004


TUZO BINAFSI.
1.Ligi Kuu ya Mchezaji wa Mwezi (1): Agosti 1996
2.PFA Young Mchezaji wa Mwaka (1): 1996-1997
3.FWA Tribute tuzo: 2008
5.Mheshimiwa Matt Busby mchezaji wa Mwaka (1), 1996-1997
6.Uingereza Mchezaji wa Mwaka: 2003
7. UEFA Club Mchezaji wa Mwaka (1), 1998-1999
8.UEFA Club Kiungo wa Mwaka (1): 1998-1999
9.Ligi Kuu ya 10 Seasons Awards (1992-1993 na 2001-02):
10.Ndani na ujumla wa Timu ya Muongo
11.Goli la Muongo {miaka kumi } michuano ya wimbledon, Agosti 17, 1996
12.BBC Sports tuzo ya Mwaka (1) ,2001
13.UEFA timu ya Mwaka: 2001,2003
14.Real Madrid Mchezaji wa Mwaka (1): 2005-2006
15.PFA Team ya Mwaka (4): 1996-97,1997-98,1998-99,1999-2000
16.ESPY tuzo - Mwanaume bora ya soka Player: 2004 [195]
17.ESPY tuzo - Best MLS Player: 2008 [195]
18.Kiingereza Football Hall of Fame: 2008
19.BBC Sports Personality wa Tuzo ya Mwaka Lifetime Achievement (1): 2010
20.Ligi Kuu ya Soka Comeback Mchezaji wa Tuzo ya Mwaka (1): 2011
21Ligi Kuu ya Soka Best XI: 2011
22.ESPY tuzo: Best MLS Player 2011

MAAGIZO NA TUZO MAALUM
1.Afisa wa Mpango wa Dola ya Uingereza na Malkia Elizabeth II: 2003
2.Mfuko wa Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Goodwill Balozi (2005-hadi sasa)
"Uingereza Greatest Balozi" - 100 Greatest Waingereza tuzo
3.Namba 1 kwenye orodha ya watu 40 wenye ushawishi mkubwa zaidi chini ya umri wa miaka 40 nchini Uingereza [200] - Arena, 2007
Dhahabu Blue Petro Badge mshindi, 2001

KUMBUKUMBU
1.Mwingereza wa kwanza kushinda mataji katika nchi nne tofauti (Uingereza, Hispania, Marekani, Ufaransa)
2.Mchezaji wa Kwanza  wa Uingereza kufunga katika michuano mitatu ya kombe la dunia.
3.Mchezaji wa kwanza ya Uingereza kucheza Ligi ya Mabingwa michezo 100.
4.Mchezaji bora wa England wa mara kwa mara wa Kombe la Dunia mwishoni alishinda mwaka 1966 - baada ya kuundwa nafasi zaidi.
5.Mchezaji wa tatu katika Ligi Kuu wakati huo katika kusaidia kuwa na chati, na kusaidia 152 katika mechi 265.

Sunday, May 12, 2013

MFAHAMU ZAIDI MICHAEL ESSIEN KATIKA ULIMWENGU WA KANDANDA"

                               Michael Essien
Essien Real Madrid.JPG
Taarifa kuhusu yeye
Full nameMichael Kojo Essien
Date of birth3 December 1982 (age 30)
Place of birthAccraGhana
Height1.77 m (5 ft 10 in)[2]
Playing positionMidfielder
Timu ya sasa
Current clubReal Madrid
(on loan from Chelsea)
Number15
Youth career
1999–2000Liberty Professionals
Senior career*
mwakaTimuMechi(Goli}
2000–2003Bastia66(11)
2003–2005Lyon71(7)
2005–Chelsea163(17)
2012–→ Real Madrid (loan)18(1)
Timu ya taifa
2002–Ghana52(9)


MATAJI AKIWA NA CLUB HIZI
Lyon
Ligue 1 (2): 2003-04, 2004-05
Trophée des Mabingwa (2): 2003, 2004
Chelsea
Ligi Kuu (2): 2005-06, 2009-10
Kombe la FA (4): 2006-07, 2008-09, 2009-10, 2011-12
Kombe la Ligi (1): 2006-07
FA Community Shield (1): 2009
Ligi ya Mabingwa (1): 2011-12

TUZO BINAFSI
2005 UNFP Ligue 1 Mchezaji wa Mwaka
BBC Afrika Mchezaji wa Mwaka: 2006 [56]
Ghana Mchezaji wa mwaka: 2008
Lengo la Chelsea msimu: 2006-07 vs Arsenal, [57]
2008-09 vs Barcelona [57]
2008 Kombe la Mataifa ya Timu ya mashindano [58]
Chelsea Mchezaji wa Mwaka: 2007 [57]
Ligue 1 Timu ya Mwaka: 2003
Ligue 1 Timu ya Mwaka: 2005

AZAM FC YAITANDIKA JKT MGAMO 3-0 KUCHEZA KOMBE LA SHIRIKISHO

AZAM FC imefanikiwa rasmi kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Mgambo Shooting jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Ushindi huo, unaifanya Azam ifikishe pointi 51, nne nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye 57 kila timu ikiwa imebakiza mechi moja kumaliza ligi.

Hadi mapumziko, tayari Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na John Raphael Bocco dakika ya 23 kufuatia kazi nzuri9 ya Humphrey Ochieng Mieno.
Kipindi cha pili, Azam tena walirudi na kasi nzuri na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 65 lililofungwa na Kipre Herman Tchetche baada ya kuichambua ngome ya wapinzani na kupioga shuti mariadi.
Hilo lilikuwa bao lake la 17 msimu huu hivyo kujihakikishia ufungaji bora wa Ligi Kuu, akiritihi mikoba ya Bocco ‘Adebayor’, ambaye naye alimrithi Mrisho Khalfan Ngassa akiwa Azam pia kabla ya kutolewa kwa mkopo Simba SC.  
Joackins Otieno Atudo aliunganishwa kwa kichwa kona ya Erasto Edward Nyoni dakika ya 80 na mpira ukatinga nyavuni na hata kipa Tonny Kavishe alipojaribu kuuokolea ndani, lakini ukagonga nyavu za juu na kudondokea ndani tena, hilo likiwa bao la tatu katika mchezo wa leo.
Azam sasa watacheza tena michuano ya Shirikisho mwakani, baada ya mwaka huu kutolewa Raundi ya Tatu na AS FAR Rabat ya Morocco wakishiriki kwa mara ya kwanza.

VIKOSI VYA TIMU ZOTE MBILI
Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Aggrey Morris, Joackins Atudo, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk85, Kipre Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Abdi Kassim dk83 na Brian Umony/Seif Abdallah dk63. 
JKT Mgambo; Tony Kavishe, Salum Mlima, Ramadhani Malima, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Mussa Gunda, Juma Mwinyimvua/Peter Mwalyanzi dk 56, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor 
Gumbo.

 RATIBA.
Jumamosi Mei 18
Toto Africans Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs African Lyon
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
TZ Prisons Vs Kagera Sugar
Simba SC Vs Yanga SC
JKT Oljoro Vs Azam FC
Polisi Moro Vs Coastal Union
MSIMAMO:
KUMBUKA YANGA BINGWA
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
YANGA
25
17
6
2
45
14
31
57
2
AZAM FC
25
14
6
4
42
20
25
51
3
SIMBA SC
25
12
9
4
38
23
15
45
4
KAGERA SUGAR
25
11
7
6
25
18
8
41
5
MTIBWA SUGAR
25
10
9
6
29
24
5
39
6
COASTAL UNION
25
8
11
6
25
23
2
35
7
RUVU SHOOTING
25
8
7
9
21
23
-2
32
8
JKT OLJORO
25
7
8
10
21
26
-5
29
9
TANZANIA PRISONS
25
7
8
10
16
22
-6
29
10
JKT RUVU
25
7
5
13
21
38
-17
26
11
MGAMBO SHOOTING
25
7
4
13
16
24
-8
25
12
POLISI MOROGORO
25
4
10
11
13
23
-10
22
13
TOTO AFRICAN
25
4
10
11
21
33
-12
22
14
AFRICAN LYON
25
5
4
16
16
38
-22     
19