Sunday, May 19, 2013

BPL YAFIKIA TAMATI MAN U, MAN CITY, CHELSEA, ARSENAL KUCHEZA UEFA.

MATOKEO BPL LEO

England
 - Premier League (Table) 
 18:18May 19 
 FTChelsea2 - 1Everton
 FTLiverpool1 - 0Queens Park R.
 FTManchester C.2 - 3Norwich C.
 FTNewcastle U.0 - 1Arsenal
 FTSouthampton1 - 1Stoke C.
 FTSwansea C.0 - 3Fulham
 FTTottenham H.1 - 0Sunderland
 FTWest Bromwich A.5 - 5Manchester U.
 FTWest Ham U.4 - 2Reading
 FTWigan Athletic2 - 2Aston Villa

BABA WA NEYMAE ASISITIZA MWANAE KUBAKI BRAZIL MAPAKA 2014

BABA wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Santos, Neymar kwa mara nyingine amesisitiza kuwa mwanae atabakia nchini Brazil mpaka kipindi cha majira ya kiangazi 2014. Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu nyota huyo kutimkia klabu ya Barcelona katika kipindi cha miezi michache ijayo huku kocha wake Tito Vilanova akithibitisha kuwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yamefanyika. Hata hivyo baba yake Neymar amesisitiza kuwa mwanae amepanga kumaliza mkataba wake na Santos akidai kuwa kama Barcelona na Real Madrid zina mpango ya kumsajili nyota huyo basi hawana budi kusogeza mipango yao mwakani. Mzee huyo amesema mipango iliyopo ni kuona mwanae anamaliza mkataba na Santos na kama klabu hiyo ikiamua kumuuza kabla ya mkataba wake kumaliza basi wanapaswa kutoa taarifa kabla ili aweze kuzungumza na mwanae kama yuko tayari kwenda Ulaya.

ROY AKERWA NA CHELSEA, MAN CITY VS TOTTENHAM KWENA MAREKANI.

Meneja wa England ROY HODGSON amekerwa na kitendo cha uamuzi wa Klabu za Chelsea, Manchester City na Tottenham kusafiri kwenda ya nje ya Nchi kucheza Michezo ya Kirafiki wakati ndio kwanza Msimu umemalizika.

Klabu hizi 3 zitasafiri n kuelekea Marekani kuumana  zenyewe kwa wenyewe katika Mechimbili za kirafiki huku Tottenham wakitua Visiwa vya Bahamas kucheza na Jamaica.
ZIARA:
Mei 23: Man City v Chelsea [St Louis]
Mei 25: Chelsea v Man City [New York]
Mei 23: Tottenham v Jamaica [Thomas A. Robinson National Stadium, Nassau Paradise Island, Bahamas]
England nayo inatarajiwa kucheza na Republic of Ireland, Uwanjani Wembley hapo Mei 29 na kisha kuruka kwenda Brazil kucheza Uwanja wa Maracana Jijini Rio De Janeiro na Brazil hapo Juni 2.
Kikosi cha Hodgson alichokiteua kuiwakilisha England katika Mechi hizo mbili kina Wachezaji wanane toka Timu hizo tatu.
Chelsea inasemekana imekubali kuwaruhusu Frank Lampard, Ashley Cole na Gary Cahill kuondoka baada ya Mechi yao ya kwanza ya Tarehe 23 na Man City ili kurudi London kujiunga na England.
Lakini Hodgson amesema wao walipanga Mechi zao za Kimataifa kwa makusudi ili kuwapa Wachezaji wote mapumziko ya Wiki moja baada ya Msimu wa Klabu zao kumalizika kisha kuwachukua wao kwa Wiki moja na baada ya hapo kuwaachia kwenda Vakesheni zao kabla kurudi Klabuni kwao kwa matayarisho ya Msimu mpya wa 2013/14.
Hogson amesema Ziara hizo za Klabu zitawafanya wasafiri safari ndefu kuvuka Bahari ya Atlantic na kurudi tena na hilo halitasaidia matayarisho yao.
Akimalizia Hodgson alisema: “Hii ndio hali ambayo tumejikuta tunayo na hatuwezi kulazimisha Klabu nini wafanye.”
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Ben Foster, Joe Hart, Alex McCarthy.
MABEKI: Leighton Baines, Gary Cahill, Ashley Cole, Phil Jagielka, Glen Johnson, Phil Jones, Joleon Lescott, Kyle Walker.
VIUNGO: Michael Carrick, Tom Cleverley, Frank Lampard, James Milner, Alex Oxlade-Chamberlain, Theo Walcott.
MAFOWADI: Andy Carroll, Jermain Defoe, Wayne Rooney, Daniel Sturridge, Danny Welbeck.

PAMBANO LA SIMBA, YANGA LAINGIZA MIL 500/-

Pambalo la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh. 500,390,000.

Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Saturday, May 18, 2013

YANGA YAITANDIKA SIMBA BAO 2-0 NAKUPELEKA SHANGWE JANGWANI.

Katika mechi wa kukata na shoka wapinzani wa jadi katika soka la Tanzania ambapo kwa ujumla leo ndio ilikuwa  tamati ya ligi kuu Vodacom Tanzania bara yanga leo imesheherekea ubingwa wake kwa furaha kubwa baada ya kuibamiza simba Bao 2-0 katika Mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Yanga ambao walijinyakulia Ubingwa mapema wakiwa na baadhi ya michezo mkononi, wameanza mechi hii kwa kasi zaidi ambapo kunako dakika ya 4 ya mchezo mchezaji wa kimataifa kutoka Burundi Didier Kavumbagu aliweza kutupia bao la kuongoza na kuleta furaha kwa mashabiki wa yanga kote Tanzania.
Lakini katika Dakika ya 28 simba walipata nafasi safi ya kusawazisha Bao hilo walipopata Penati kufuatia Nadir Haroub 'Cannavaro' kumuangusha Mrisho Ngassa katika eneo la hatari lakini Mussa Mudde alikosa Penati hiyo baada kipa alli Mustapha  barthez kuicheza penati hiyo..
dakika 45 za kipindi cha kwanza Yanga 1 Simba 0  katika Kipindi cha Pili, Dakika ya 63, Hamis Kiiza alifungia Yanga Bao la Pili.
Kwenye Dakika ya 89 Mechi hii iliingia balaa baada ya masoud Cholo wa Simba na  DidierKavumbagu kuvaana na Refa Martin Saanya alipoingilia kati na kuanguka  chini na  alipoamka  refa huyo alionekana kutokwa damu lakini Mechi iliendelea.
VIKOSI VYA LEO:
Yanga: Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Athuman Idd 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima
Akiba: Said Mohamed, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nurdin Bakar, Nizar Khalfan, Said Bahanuz, Jerry Tegete
SimbaJuma Kaseja, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, Haruna Chanongo
Akiba: Abel Dhaira, Miraji Adam, Ramadhan Singano 'Messi', Felix Sunzu, Christopher Edward, Jonas Mkude, Hassan Mkude
REFA: Martin Saanya [Morogoro]
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Mei 18
Simba SC 0 Yanga 2
Toto Africans 2 Vs 0 Ruvu Shooting
Mgambo JKT  1 Vs African Lyon 0
JKT Ruvu 1 Vs 0 Mtibwa Sugar
TZ Prisons 0 Vs 1 Kagera Sugar
JKT Oljoro 0 Vs 1 Azam FC
Polisi Moro 1 Vs 0 Coastal Union
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Timu tano za juu hucheza michuano ya BANK ABC huku Yanga pia mwakani ikiwakilisha Taifa katika Club Bingwa afrika bila kusahau Azam fc kurejea tena katika michuano ya kombe la shirikisho barani afrika kwa mara ya pili baada ya mwaka ya mwaka huu kutolewa na timu ya Far Rabat kwa jumla ya bao 2-1.
Timu 3 zimeshuka daraja african lyon,Polisi morogoro,Toto african kuzipisha Mbeya city kutoka mbeya tanzania, Ashanti united ya Dar es saalam bila kusahau Rhino Rangers ya Tabora kucheza VPL Msimu ujao.

MSIMAMO: 
*YANGA =BINGWA
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
yanga
26
18
6
2
47
14
33
60
2
azam fc
26
15
6
4
45
20
25
54
3
simba sc
26
12
9
5
38
25
13
45
4
kagera sugar
26
11
8
6
26
19
8
44
5
mtibwa sugar
26
10
9
6
29
25
5
39
6
coastal union
26
8
11
6
25
24
2
35
7
ruvu shooting
26
8
8
9
22
26
-2
32
8
jkt oljoro
26
7
8
10
21
26
-5
29
9
tanzania prisons
26
7
8
10
16
23
-6
29
10
jkt ruvu
26
7
5
13
21
38
-18
29
11
mgambo shooting
26
7
4
14
16
27
-11
28
12
polisi morogoro
26
4
10
11
13
23
-11
25
13
toto african
26
4
10
11
21
33
-13
25
14
african lyon
26
5
4
16
16
38
-22
19