Saturday, May 18, 2013

YANGA YAITANDIKA SIMBA BAO 2-0 NAKUPELEKA SHANGWE JANGWANI.

Katika mechi wa kukata na shoka wapinzani wa jadi katika soka la Tanzania ambapo kwa ujumla leo ndio ilikuwa  tamati ya ligi kuu Vodacom Tanzania bara yanga leo imesheherekea ubingwa wake kwa furaha kubwa baada ya kuibamiza simba Bao 2-0 katika Mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Yanga ambao walijinyakulia Ubingwa mapema wakiwa na baadhi ya michezo mkononi, wameanza mechi hii kwa kasi zaidi ambapo kunako dakika ya 4 ya mchezo mchezaji wa kimataifa kutoka Burundi Didier Kavumbagu aliweza kutupia bao la kuongoza na kuleta furaha kwa mashabiki wa yanga kote Tanzania.
Lakini katika Dakika ya 28 simba walipata nafasi safi ya kusawazisha Bao hilo walipopata Penati kufuatia Nadir Haroub 'Cannavaro' kumuangusha Mrisho Ngassa katika eneo la hatari lakini Mussa Mudde alikosa Penati hiyo baada kipa alli Mustapha  barthez kuicheza penati hiyo..
dakika 45 za kipindi cha kwanza Yanga 1 Simba 0  katika Kipindi cha Pili, Dakika ya 63, Hamis Kiiza alifungia Yanga Bao la Pili.
Kwenye Dakika ya 89 Mechi hii iliingia balaa baada ya masoud Cholo wa Simba na  DidierKavumbagu kuvaana na Refa Martin Saanya alipoingilia kati na kuanguka  chini na  alipoamka  refa huyo alionekana kutokwa damu lakini Mechi iliendelea.
VIKOSI VYA LEO:
Yanga: Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Athuman Idd 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima
Akiba: Said Mohamed, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nurdin Bakar, Nizar Khalfan, Said Bahanuz, Jerry Tegete
SimbaJuma Kaseja, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, Haruna Chanongo
Akiba: Abel Dhaira, Miraji Adam, Ramadhan Singano 'Messi', Felix Sunzu, Christopher Edward, Jonas Mkude, Hassan Mkude
REFA: Martin Saanya [Morogoro]
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Mei 18
Simba SC 0 Yanga 2
Toto Africans 2 Vs 0 Ruvu Shooting
Mgambo JKT  1 Vs African Lyon 0
JKT Ruvu 1 Vs 0 Mtibwa Sugar
TZ Prisons 0 Vs 1 Kagera Sugar
JKT Oljoro 0 Vs 1 Azam FC
Polisi Moro 1 Vs 0 Coastal Union
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Timu tano za juu hucheza michuano ya BANK ABC huku Yanga pia mwakani ikiwakilisha Taifa katika Club Bingwa afrika bila kusahau Azam fc kurejea tena katika michuano ya kombe la shirikisho barani afrika kwa mara ya pili baada ya mwaka ya mwaka huu kutolewa na timu ya Far Rabat kwa jumla ya bao 2-1.
Timu 3 zimeshuka daraja african lyon,Polisi morogoro,Toto african kuzipisha Mbeya city kutoka mbeya tanzania, Ashanti united ya Dar es saalam bila kusahau Rhino Rangers ya Tabora kucheza VPL Msimu ujao.

MSIMAMO: 
*YANGA =BINGWA
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
yanga
26
18
6
2
47
14
33
60
2
azam fc
26
15
6
4
45
20
25
54
3
simba sc
26
12
9
5
38
25
13
45
4
kagera sugar
26
11
8
6
26
19
8
44
5
mtibwa sugar
26
10
9
6
29
25
5
39
6
coastal union
26
8
11
6
25
24
2
35
7
ruvu shooting
26
8
8
9
22
26
-2
32
8
jkt oljoro
26
7
8
10
21
26
-5
29
9
tanzania prisons
26
7
8
10
16
23
-6
29
10
jkt ruvu
26
7
5
13
21
38
-18
29
11
mgambo shooting
26
7
4
14
16
27
-11
28
12
polisi morogoro
26
4
10
11
13
23
-11
25
13
toto african
26
4
10
11
21
33
-13
25
14
african lyon
26
5
4
16
16
38
-22
19