Saturday, May 18, 2013

ATHLETICO MADRID YATWAA UBINGWA YAICHALAZA REAL MADRID 2-1.

CLUB ya  soka ya  Atletico Madrid usiku wa jana ilifanikiwa kuifunga Read Madrid kwa goli 2-1 na kuchukua kombe la Copa del Rey katika fainal iliyopigwa Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Uhispania.
Read Madrid ndio iliyokua ya kwanza kupata goli kupita kwa Ronaldo katika dakika ya 14 kabla ya kiungo Diego Costa kuisawazishia Atletico dakika ya 35 nakufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka dakika 90 zinamalizika.
Alikuwa ni beki wa kibrazil Miranda alipeleka kilio kwa kikosi cha Jose Mourinho mara baada ya kufunga goli la pili na la ushindi kwa timu yake katika dakika ya 99 mara kuwa zimeongezwa dakika 120.
Fainali hiyo ya jana iligubikwa na vitendo vibaya vilivyooneshwa na wachezaji kutoka timu zote mbili na muhamuzi kutoa jumla ya kadi za njano 13 na nyekundu 2 kwa timu zote mbili.
Nyota wa Real Madrid Ronaldo ye akipata kadi nyekundu katika dakika ya 114 huku akiwa na kadi ya njano kabla na Fernandez wa Atletico pia akipewa nyekundu dakika ya mwisho ya 120 baada ya awali kuwa na kadi ya njano.