RAIS wa Real Madrid Florentino Perez leo usiku ametangaza kuondoka kwa Kocha wao Mkuu Jose Mourinho kufuatia makubaliano ya pande zote mbili.
Akihutubia Wanahabari walioshuhudia Perez amesema Tumeamua kumaliza uhusiano wet na mtu spechu. Hakuna Mtu aliemfukuzwa kazi bali ni makubaliano ya pande mbili.
Real madrid ikiwa imebakisha Mechi 2 za La Liga, Real Madrid wako Nafasi ya Pili na Pointi 13 nyuma ya Mabingwa FC Barcelona na Ijumaa iliyopita walitwangwa 2-1 kwenye Fainali ya Copa del Rey na Mahasimu wao Atletico Madrid.
MOURINHO NA MATAJI YAKE:
UCL: 2004 (Porto), 2010 (Inter Milan)
UEFA CUP: 2003 (Porto)
BPL: 2005, 2006 (Chelsea)
FA CUP: 2007 (Chelsea)
LEAGUE CUP: 2005, 2007 (Chelsea)
LA LIGA: 2012 (Real Madrid)
COPA DEL REY: 2011 (Real Madrid)
SERIE A: 2009, 2010 (Inter Milan)
COPPA ITALIA: 2010 (Inter Milan)
PRIMEIRA LIGA: 2003, 2004 (Porto)
TACA DE PORTUGAL: 2003 (Porto)

ikumbukwe kabla Mourinho kutua Real Madrid, Klabu hiyo ilikaa Miaka miwili bila Taji lolote n baada ya kufika yeye walitwaa Copa del Rey Mwaka 2011 na kufuatia Ubingwa wa Spain wa La Liga Mwaka 2012 lakini Msimu huu ametoka mikono mitupu ukiachia Super Cup.
katika tetesi zilizopo kwa taarifa mbalimbali inaaminika kuwa Mourinho anarejea katika Klabu yake ya zamani ya jijini london club ya Chelsea, na kwa Real inaaminika akatatua Carlo Ancelotti kutoka PSG ingawa bado uthibitisho rasmi haukutolewa mbali ya PSG kumkatalia Ancelotti kuhama.