Monday, June 17, 2013

Sunday, June 16, 2013

JUPP HEYNCKES AWEKA WAZI KUTOFANYA KAZI YA UKOCHA

Baada ya kuipa mafanikio ya kutosha Bayern muninch Jupp Heynckes hatimaye amebainisha kuwa hataendelea kufanya kazi hiyo baada ya kuondoka kwa mabingwa wa soka barani Ulaya. Bayern wakiwa chini ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 wamefanikiwa kumaliza msimu kwa mafanikio kwa kunyakuwa mataji matatu ya Bundesliga, DFB-Pokal na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa mafanikio hayo Bayern imekuwa klabu ya saba barani Ulaya kufanikiwa kushinda mataji matatu mfululizo. Hatahivyo Heynckes ameamua kustaafu kufundisha baada ya nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola.

FIFA YATANGAZA KUWA MZUNGUUKO WA TATU KUFUZU KOMBE LA DUNIA NI MWEZI SEPTEMBER.

SHIRIKISHO la Soka Dunia-FIFA limetangaza kuwa mzunguko wa tatu wa mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 pamoja na hatua ya mtoano kwa nchi za barani Ulaya itafanyika Septemba na Octoba mwaka huu. Ratiba kwa upande wa nchi za Afrika ambazo zitajumuisha washindi kutoka katika makundi 10 itafanyika Septemba 16 jijini Cairo, Misri ambapo nchini tano zilizo juu katika viwango vya ubora vya FIFA ndizo zitaongoza ratiba hiyo. Nchi nane zitakazomaliza katika nafasi ya pili barani Ulaya nazo zitapangiwa ratiba jijini Zurich, Switzerland Octoba 21 huku nchi nne kati ya zilizo juu katika viwango vya FIFA zikiongoza ratiba hiyo. Tanzania inajitupa uwanjani leo kuvukuzia nafasi ya kuingia katika ratiba hiyo kwa kupambana na Tembo wa Ivory Coast katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

SIMBA, YANGA, SUPER FALCOM HAZIENDI SUDAN KWENYE KAGAME:

KLABU za Tanzania hazitakwenda kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame inayofanyika kuanzia wiki ijayo mjini Kigali, Rwanda.
Hiyo inafuatia kuingiliana kwa taarifa za Serikali, awali ilielezea kuzizuiatimu hizo kwenda sudani kutokana na hali ya machafuko, na baadaye ikiziruhusu kwenda baada ya kuhakikishiwa usalama wa klabu hizo na Serikali ya Sudan kuwa zitapata ulinzi wa kutosha.

serikali ilitoa ruhusa kwa timu hizi baada ya kupata uthibitisho kutoka serikali ya sudani huku ukitazama mashindano haya yanaanza Jumanne june 18 ambapo club hazijafanya maandalizi yoyote ya safari.
mbali na hiyo haitoshi baada ya zuio la awali, CECAFA (Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati) likateua timu mbadala kuziba nafasi ya timu tatu za Tanzania.
aidha Timu za bongo kwetu tanzania zilizotarajiwa kushiriki michuano hiyo ni Simba SC, Yanga za Dar es Salaam na Super Falcons ya Zanzibar.

katika hali ya kawaida Sasamichuano hii ya Kagame mwaka huu, haikustahili kufanyika Sudan, ambako kila siku tunasikia watu wanauawa kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, lakini kutokana na sababu zake katibu wa CECAFA  Musonye ameamua kuipeleka huko.
Hivyo mtandao huu umefanya mazungumzo mbalimbali za wadau wa michezo hapa nchini ambapo miongoni mwao wamezungumza katika hali ya kawaida endapo machafuko ya kitokea"
inaamaa vilabu vya tanzania ndio vitapata fursa ya kuwa chini ya uangalizi haya yote yanatokana kauli ya serikali ya sudani kuiandikia barua serikali ya tanzania kupitia wizira ya habari utamaduni na michezo kuwa timu za tanzania zitapata ulinzi wa kutoka katika michuani hiyo.
katika hali ya kawaida wadau wamesema haiingii akilini kuzipeleka timu na kwenda kuziangamiza katika nchi ambayo haishiwi vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Hata hivyo katika hali ya kawaida inamaana vilabu vya tanzania ndio vyenye umuhimu katika suala la ulinzi vipi kenya na burundi pamoja na uganda vilabu hivi havihitaji ulinzi?".
Mbali ya yote michuano hii haikustahili kuchezwa Sudani kutokana na sababu ambazo kila mtu anazifamu vita za wenyewe kwa wenyewe ambapo kila siku tunasikia vurugu za hapa na pale.Tukumbuke michezo ni burudani na starehe ya aina yake endapo kutakuwa na vurugu za hapa na pale pasi furaha ya michezo inapotea kabisa Hivyo CECAFA kwa mara nyingine tena tulitazame hili.

RATIBA KOMBE LA KAGAME ILIKUWA HIVI:
KUANZIA JUNI 18 HADI JULAI 2, 2013 (EL-FASHIR NA KADUGLI, SUDAN)

TAREHETIMUTIMUKUNDI/MUDAUWANJA
18.06.2013.TUSKERSUPER FALCONB - SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
AL HILLALAL NASRIB -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
19.06.2013.VITALOOPORTSC - SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
20.06.2013.YANGA SCEXPRESSC - SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
20.06.2013.ELMAN FCAPR FCA - SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
20.06.2013.SUPER FALCONAL NASRIB -SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
20.06.2013.TUSKERAL-SHANDYB -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
21.06.2013.EL MERREIKHSIMBA SCA -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
22.06.2013.EXPRESS FCVITALOOC - SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
PORTSYANGA SCC -SAA 10:00 JIONIEL FASHER
22.06.2013.AL NASRITUSKERB - SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
AL SHANDYAL HILALB -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
23.06.2013APRSIMBA SCA - SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
EL MERREIKHELAM FCA -SAA 10:00 JIONI
EL-FASHER
24.06.2013AL NASRIAL SHANDYB -SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
SUPER FALCONAL HILLALB -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
24.06.2013.PORTSEXPRESS FCC -SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
25.06.2013.VITALOOYANGA SCC -SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
26.06.2013.AL SHANDYSUPER FALCONB -SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
AL HILLALTUSKERB -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
26.06.2012.SIMBA SCELMAN FCA -SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
APR FCEL MERREIKA -SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
27.06.2013.MAPUMZIKOMAPUMZIKOMAPUMZIKO
MAPUMZIKO
28.06.2013.(23) B2 VS C2(24) B1 VS BEST QUTATANGAZWAKADUGLI
28.06.2013.(25) C1 VS A2(26) A1 VS B3UTATANGAZWAEL-FASHER
30.06.2013.WNR 23 VS WNR 25WIN 24 VS WIN 26UTATANGAZWA
01.07.2013.MAPUMZIKOMAPUMZIKOMAPUMZIKOMAPUMZIKO
02.07.2013.ILIYOFUNGWAILIYOFUNGWAMSINDI WA TATUEL-FASHER
ALIYESHINDA 27ALIYESHINDA 28FAINALI

NEYMA AFANYA MAMBO KATIKA KOMBE LAMICHUANO YA KOMBE LA MABARA-UFUNGUZI

Neymar
MSHAMBULIAJI nyota mpya wa Fc Barcelona,Neymar jana alifanikiwa kung'arisha nyota yake katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mabara, akifunga bao la mapema dakika ya tatu wakati Brazil inailaza 3-0 Japan.
Mshambuliaj huyo nyota wa Brazil, alifunga kwa shuti la nje ya eneo la hatari, akiunganisha pasi ya Fred ambaye naye alipokea krosi ya Marcelo kwa kifua kwanza.
NeymarPaulinho alifunga la pili dakika ya 48 kwa pasi ya Dani Alves na Jo akafunga la tatu dakika ya 90.
Ushindi huo unaiweka Brazil kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake tatu. Italia na Mexico watamenyana leo katika mechi nyingine ya kundi hilo.
Kikosi cha Brazil jana kilikuwa; Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Oscar, Gustavo, Paulinho, Fred/Jo dk81, Neymar/Lucas Moura dk74 na Hulk/Hernanes dk75.
Japan: Kawashima, Konno, Nagatomo, Uchida, Yoshida, Endo/Hosogai dk77, Honda/Inui dk88, Kiyotake/Maeda dk51,Kagawa, Hasebe na Okazaki.

LUCAS ASEMA SUAREZ AKIONDOKA NI PENGO KUBWA KWA LIVERPOOL

KIUNGO wa klabu ya Liverpool Lucas Leiva ameweka wazi kuwa litakuwa pengo kubwa kama Luis Suarez ataondoka katika klabu hiyo kwenye kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay tayari ameweka wazi kusudio lake la kuachana na Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya kudai vyombo vya habari nchini humo vikiandama maisha yake binafsi. Suarez ambaye amefunga mabao 30 katika mashindano yote akiwa na Liverpool msimu uliopita pia alidai ndoto zake zitatimia kama akisajiliwa na klabu ya Real Madrid ya Hispania. Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil anadhani kuwa kama Brendan Rodgers akishindwa kuhakikisha anambakisha nyota huyo basi itakuwa ni ndoto kwa klabu hiyo kuwekwa katika kundi la timu ambazo zinaweza kunyakuwa taji la ligi msimu ujao.

MESSI AMUACHA MARADONA KATIKA ORODHA YA WAFUNGAJI TIMU YA TAIFA

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na club ya fc barcelona Lionel Messi amemuacha nguli wa soka wan chi hiyo Diego Maradona katika orodha ya wafungaji kufuatia mabao matatu aliyofunga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Guatemala ambao walishinda kwa mabao 4-0. Nyota huyo wa Barcelona alifungua karamu ya mabao katika dakika ya 15 ya mchezo kabla ya kuongeza lingine muda mchache kabla ya mapumziko huku bao la tatu akifunga katika dakika ya 52 na kufikisha jumla ya mabao 35 kwa timu ya taifa na kumuacha Maradona ambaye aliwahi kuifungia timu hiyo mabao 34. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Messi kama kawaida yake alidai kumzidi Maradona kwa mabao sio suala muhimu kwake kitu cha msingi ni kwamba walicheza kwa umoja ndio maana wamepata matokeo mazuri. Messi sasa anawakaribia nyota wengine wa nchi hiyo ambao ni Hernan Crespo huku bado akiwa na safari ndefu ya kumfikia kinara wa ufungaji wa nchi hiyo Gabriel Batistuta ambaye kipindi chake akiichezea Argentina alifunga mabao 56.