Beki mahiri na mwenye nguvu za kukaba wa klabu ya Barcelona, Carles Puyol anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti lake la kulia ambao utamuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu mpaka nne. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika mtandao wa klabu hiyo mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania anatarajiwa kufanyiwa upasuaji huo leo. Puyol mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara katika miaka ya karibuni ukiwemo upasuaji wa mguu huohuo mara mbili, kuvunjika mfupa wa taya na pia kuteuka kiwiko cha mkono wake. Majeraha hayo yalimlazimu nyota huyo kukosa michuano ya Euro 2012 ambapo Hispania walitawadhwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo na pia kuenguliwa katika kikosi cha nchi hiyo kilichopo nchini Brazil kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Wednesday, June 19, 2013
FABRIGAS AFUNGUKA KUHUSU REAL MADRID-USAJILI BALE
Kiungo nyota wa klabu ya Barcelona na timu ya Tifa ya hispain Cesc Fabregas ametanabisha kuwa klabu ya Real Madrid ya Hispania watakuwa wametwanga maji kwenye kinu mtungi endapo kama wakivunja rekodi ya usajili kwa kulipa euro milioni kwa kumsajili mshambuliaji nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Gareth Bale. ambaye ni Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Wales amekuwa akihusishwa kwenda Santiago Bernabeu huku kukiwa na tetesi kuwa ada ya uhamisho wake inafikia paundi milioni 85 ambayo itavunja rekodi ya sasa ya euro milioni 94 ambazo Madrid aliipa Manchester United kwa ajili ya Cristiano Ronaldo. Hatahivyo, Fabregas haelewi kwanini klabu hiyo inajiandaa kulipa kiasi hicho kikubwa cha pesa huku wakijua kuwa kuna tatizo kubwa la mdodoro wa kiuchumi unaizikumba baadhi ya nchi wakiwemo wao. Fabregas pia alirejea kauli yake kwamba angependa kuendelea kubakia Barcelona na kushangaa baadhi ya watu wakizungumza kwamba anataka kurejea katika Ligi Kuu nchini Uingereza.
AVB AWAKANA PARIS SAINT GERMAN-UKOCHA
Andre Villas-Boas kocha wa Tottenham ameripotiwa kuitupilia mbali ofa ya kuifundisha club Paris Saint-Germain lengo kuu likiwa ni kubaki ndani ya White Hart Lane {Tottenham}.
Mabingwa hao wa Ufaransa walimhitaji AVB Mreno huyo kurithi mikoba ya Carlo Ancelotti ambaye anatarajiwa kuelekea nndani ya Bernebeu Real Madrid lakini sasa mawzo yote yamehamia kwa Fabio Capello.
Inafahamika Villas-Boas alipewa ofa ya Mkataba wa miaka mitatu na mabilionea wa Qatari wanaoimiliki PSG baada ya majadiliano na wakala wake, Carlos Goncalves, lakini mwalimu huyo kijana wa miaka 35 anataka kufanya mambo makubwa katika club ya Spurs ambapo walimchukuwa msimu uliopita akitokea katika club ya chelsea baada ya kutupiwa virago Chelsea.
Katika Taarifa za jana usiku nchini Ufaransa zimesema kuwa kocha wa zamani wa England, Capello atakuwa mwalimu mpya wa PSG kwa Mkataba wa mwaka mmoja.
Kocha wa zamani wa England, Capello anatazamiwa kuwa mpango B wa PSG, licha ya kwamba bado ana Mkataba wa mwaka mmoja Urusi.
Urusi ipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil,na kuna uwezekano Capello akarejea katika timu hiyo ya taifa baada ya msimu mmoja na PSG kukamilisha majukumu yake katika Kombe la Dunia.
KESHI AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUWA MAKINI LANGONI

Katika mchezo huo uliopigwa huko Belo Horizonte mashabiki waliohudhuria mchezo huo walionyesha kuwa upande wa Tahiti na mabao ya Nigeria hayakuonyesha kuwakuna mashabiki hao lakini Keshi hajali suala hilo. Keshi amesema unapokuwa mchezaji wa kulipwa mambo kama hayo ni ya kawaida kukutana nayo kitu cha msingi ni kuhakikisha unapata matokeo muhimu ili uweze kusonga mbele. Michuano hiyo inaendelea tena kesho ambapo wenyeji Brazil watakwaana na Waamerika Kusini wenzao Mexico katika Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro.
BENZEMA VS RIBERY KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA NGONO"
Wanandinga wa Kimataifa wa Ufaransa, Franck Ribery na Karim Benzema wamefikishwa mahakamani leo jijini Paris wakituhumiwa kutembea na mwanamke anayejiuza mwenye umri mdogo. Ribery ambaye anacheza katika klabu ya Bayern Munich na Benzema anayekipiga katika klabu ya Real Madrid watakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini inayozidi euro 45,000 kama wakikutwa na hatia ya kutenda kosa hilo. Nyota hao wote wawili walikana tuhuma hizo huku mwanamke huyo aitwaye Zahia Dehar alitoa ushahidi kuwa wote wawili hawakuwa wakijua kama hajafikisha umri huo wakati wakifanya naye mapenzi mwaka 2008 na 2009. Pamoja na kwamba umri halali ni miaka 15 nchini Ufaransa lakini kumlipa mwanamke anayejiuza chini ya umri wa miaka 18 ni kosa.
Tuesday, June 18, 2013
MAKALA KUHUSU UCHAMBUZI WA TAIFA STARS""
TAIFA Stars timu ya soka ya Taifa ya Tanzania,imefanikiwa kulala ikiwa nyumbani baada ya kufungwa mabao 4-2 dhidi ya Ivory Coast na kuzima harakati za hapa na pale za kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil.
Amini watanzania
wengi na wadau wa michezo nchini waliweka matumaini na kudhani Taifa Stars ingeweza kusonga mbele katika
harakati hizo za kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014, lakini sasa ukweli
kila kitu kipo wazi na ukweli umejionyesha.
Asilimia kubwa ya watanzania Sasa
wamekubaliana na uhalisia wa mambo kwamba Timu ya Taifa ifike tunako taka inahitaji muda kidogo kuona
Taifa Stars ikisonga mbele katika kuelekea kufuzu Kombe la Dunia na siyo rahisi
kama ilivyodhaniwa hapo kabla.
Ni
mambo mengi yaliyotokea katika mchezo dhidi ya Ivory Coast ambayo yaliigharimu
Taifa Stars licha ya uwanja kujaa idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa
wakiishangilia timu yao bila kuchoka.
Jambo
la msingi ni kwamba, Taifa Stars ikiwa katika harakati za kuhakikisha inafuzu
Kombe la Dunia wengi tulisahau kwamba kiukweli ilikuwa ngumu kwa Taifa
Stars kufuzu fainali hizo japokuwa kwa mapenzi tulidhani timu hii ingeweza
kufuzu kwa kuanza na vipigo kwa timu za Morocco na Ivory Coast.
Tukitazama
mchezo kati ya Taifa Stars na Ivory Coast kuna baadhi ya mambo yalionekana
kwamba bado tuna safari ndefu ya kufuzu Kombe la Dunia kama kweli tuna nia ya
kufanya hivyo.
Mambo
mengi mno yalijitokeza katika mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast
na haya ni machache kati ya mengi yake.
1.Umakini wa safu ya ulinzi ulikuwa hafifu -katika kudhibiti kasi ya Salomon Kalou pamoja na Gevinho walikuwa mwiba katika safu ya ulinzi ya tanzania.

Hapa katika hali ya kawaida ilionekana upande wa mchezaji Erasto Nyoni unaweza kubeba lawama nzito lakini halikuwa kosa lake kwani alilazimika kwenda katikati kuongeza nguvu na kusawazisha makosa ya mabeki wa kati ambapo ilipelekea kusahau nafasi yake na majukumu aliyopewa.
Katika hali ya kawaida kiukweli ilionekana‘njia’ tangu dakika za mwanzo, beki Erasto Nyoni inaonekana
hakupata ushauri wa kutosha kuhusu kutulia na kucheza soka kwani hata makelele
ya mashabiki yalimfanya aonekane mtu asiyefa hatuweza kumlaumu.
2.Nguvu ndogo ya wachezaji wa Taifa Star-
2.Nguvu ndogo ya wachezaji wa Taifa Star-
Safu
ya kiungo- kwa upande wa Ivory Coast ikisimamiwa vilivyo na Yaya Toure licha ya mchezo wa jana kucheza safu ya ushambuliaji aliweza kutimiza majukumu aliyopewa na kocha wake kiukweli kiungo huyu wa Club ya Man city alionyesha uwezo wake na kuwazidi wachezaji wa Taifa Star Abubakar Sure boy ambaye ni mfupi na mwenye umbo dogo alionekana mchezaji wa kawaida mbele ya Yaya Toure ambapo pia Frank domayo pamoja na Mwinyi
Kazimoto licha ya kucheza vizuri lakini maumbo yao walionekana kutoweza kuhimili mikimikiya Traore Lucina na Jean Jacques ambao wote ni
watu wenye miili mikubwa pia hilo lilikuwa moja ya jambo lililoigharimu timu.
4.Umakini Mbovu wa Safu ya Ushambuliaji- Licha ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu Mbwana Samata ,Tomas Ulimwengu pamoja na Amri Kiemba kwa kushirikiana kwa pamoja na kuweza kupata Mabao Mawili" Hapa wachezaji hawa walionekana kutopeana nafasi na kujipanga vizuri kuhakikisha wanajipatia nafasi nzuri za kutupia mabao wavuni.
5.Mbali ya yote'' Taifa star inastahili pongezi kwa kuweza kumiliki mpira na kuonyesha kandanda safi katika mchezo huo hivyo kubwa zaidi watanzania tuamini kabisa katika michuano ya CHAN inayo kuja lazima tutashiriki kutokana na ubora wa kocha wetu Kim Poulsen ambaye kiukweli ameweza kuitengeneza timu kucheza kwa kujiamini licha ya kupoteza mchezo ule" Hivyo kubwa zaidi ni kuipa Support Timu yetu ya Taifa. Ahsanteni.
3.Ubora wa wachezaji wa Ivory Coast-Kila mtu anafahamu Kabisa kuwa kikosi cha Timu ya hiyo kinawachezaji wengi wenye uzoefu wanaocheza katika ligi mbalimbali Barani ulaya wemeonekana kujiamini mbele ya wachezaji wa Taif Star na kujipa Matumaini kuwa wataibuka na ushindi katika mchezo ule. kwa ufupi tu kwa haraka haraka kila mdau wa michezo anafahamu uwezo wa Yaya Toure,Solomon Kalou,Gervinho na wengineo kina Bakari Kone nk.

5.Mbali ya yote'' Taifa star inastahili pongezi kwa kuweza kumiliki mpira na kuonyesha kandanda safi katika mchezo huo hivyo kubwa zaidi watanzania tuamini kabisa katika michuano ya CHAN inayo kuja lazima tutashiriki kutokana na ubora wa kocha wetu Kim Poulsen ambaye kiukweli ameweza kuitengeneza timu kucheza kwa kujiamini licha ya kupoteza mchezo ule" Hivyo kubwa zaidi ni kuipa Support Timu yetu ya Taifa. Ahsanteni.
PONGEZI KWA WASHABIKI KUIUNGA MKONO STARS
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawashukuru washabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa juzi (Jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwitikio wa washabiki katika mechi hiyo ilikuwa ni moja ya chachu ya kiwango kilichoonyeshwa na Taifa Stars, kwani walishangilia mwanzo hadi mwisho licha ya kupoteza kwa mabao 4-2.
Ni matarajio utakuwepo mwitikio kama huo huo katika mechi ijayo ya Taifa Stars ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) dhidi ya Uganda (The Cranes) itakayochezwa Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu. Stars itaingia tena kambini Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.
RWIZA KUHUDHURIA SEMINA YA MAKAMISHNA CAF
Kamishna Alfred Kishongole Rwiza ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuhudhuria semina ya makamishna itakayofanyika kuanzia Julai 6-7 mwaka huu katika makao makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, Misri.
Semina hiyo inashirikisha baadhi ya makamishna wa CAF walioko kwenye orodha ya makamishna ya shirikisho hilo kwa mwaka 2012-2014.
Rwiza ni mmoja wa makamishna wa CAF kutoka Tanzania, na mechi ya mwisho kusimamia ilikuwa ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa Mei mwaka huu nchini Msumbiji.
CAF tayari imeshamtumia tiketi Rwiza, na anatarajia kuondoka nchini Julai 4 mwaka huu kwenda Cairo kwa ndege ya EgyptAir.
MTANZANIA APEWA ITC ACHEZE YEMEN

Mtumwa ambaye anatoka katika kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji cha Rollingstone cha Arusha aliombewa hati hiyo na Chama cha Mpira wa Miguu cha Yemen (YFA) kwa ajili ya kucheza nchini humo.
TFF inamtakia kila la kheri Mtumwa katika safari yake ya Yemen, na ni matarajio yetu kuwa atakuwa balozi mzuri wa Tanzania nchini humo ili wachezaji wengine wa Tanzania nao wapate fursa ya kucheza mpira wa miguu nchini Yemen.
KLABU THAILAND YASAKA WACHEZAJI TANZANIA
Klabu ya Thai Port Football ya Thailand inatafuta wachezaji nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu nchini humo na katika nchi nyingine barani Ulaya.
Kupitia kwa wakala wake, klabu hiyo imetuma taarifa kupitia Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) ikitaka wachezaji wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 28 kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ambapo watakaofuzu watacheza nchini humo na katika klabu nyingine za Ulaya ambazo wana ushirikiano nazo.
Wachezaji wenye nia ya kufanya majaribio wanatakiwa kutuma taarifa za wasifu wao (CV) kwa klabu hiyo kwa njia ya emaili, wawe na pasi ya kusafiria pamoja na pasi ya mchezaji (player passport).
Wakala atapitia vitu hivyo, na kwa wachezaji atakaowahitaji atawatumia tiketi za ndege na viza kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio nchini humo, na watakaofanikiwa kabla ya kusaini nao mikataba watawasiliana na klabu zao nchini (kwa wale wenye klabu).
Wakala atapitia vitu hivyo, na kwa wachezaji atakaowahitaji atawatumia tiketi za ndege na viza kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio nchini humo, na watakaofanikiwa kabla ya kusaini nao mikataba watawasiliana na klabu zao nchini (kwa wale wenye klabu).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Subscribe to:
Posts (Atom)