Timu ya soka ya Anzhi Makhachkala ya Urusi kwa mara nyingine haitacheza mechi zake za Europa League msimu ujao mbali na uwanja wao wa nyumbani baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka barani-UEFA humo kwasababu za kiusalama. Katika taarifa ya UEFA iliyotumwa katika mtandao wake imedai kuwa baada ya kufanya utafiti wa usalama katika mji wa Kaskazini wa Caucasus ambao klabu hiyo inatoka wamegundua kuwepo usalama mdogo hivyo hawatoruhusu timu hiyo kucheza mechi zake nyumbani. UEFA imeitaka klabu hiyo kutafuta uwanja mbadala kwa ajili ya mechi zake za nyumbani za Europa League msimu wa 2013-2014. Anzhi walimaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Urusi msimu uliopita na kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Thursday, June 20, 2013
Wednesday, June 19, 2013
BPL HADHARANI MAN U KUUMANA NA SWANSEA CITY
HATIMAYE RATIBA ya Ligi Kuu nchini Uingereza BPL kwa ajili ya msimu wa 2013-2014 imetoka huku mabingwa wa ligi hiyo Manchester United wakipangwa kufungua msimu na timu ya Swansea City. Ratiba hiyo itamshuhudia David Moyes akianza kibarua chake katika mechi ya kwanza kama bosi wa United dhidi ya timu hiyohiyo ambayo Sir Alex Ferguson alikutana nayo katika mchezo wake wa mwisho kabla ya kustaafu. Washindi wa pili wa ligi hiyo Manchester City watawakaribisha Newcastle United wakati Hull City ambayo imepanda daraja msimu huu itakuwa na safari ngumu pale watakapoifuata Chelsea, Stamford Bridge. Mechi nyingine Crystal Palace ambao nao wamepanda daraja msimu huu watawakaribisha Tottenham Hotspurs katika mchezo wa mahasimu wa jijini la London huku Arsenal wakiwakaribisha Aston Villa wakati Stoke City watakuwa wenyeji wa Liverpool. Nyingine ni Norwich watakuwa wenyeji wa Everton, Sunderland watakwaana na Fulham, West Bromwich na Southampton huku West Ham United wakichuana na Cardiff City.
PUYOL MBIONI KUFANYI UPOASUAJI WA GOTI LAKE"
Beki mahiri na mwenye nguvu za kukaba wa klabu ya Barcelona, Carles Puyol anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti lake la kulia ambao utamuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu mpaka nne. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika mtandao wa klabu hiyo mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania anatarajiwa kufanyiwa upasuaji huo leo. Puyol mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara katika miaka ya karibuni ukiwemo upasuaji wa mguu huohuo mara mbili, kuvunjika mfupa wa taya na pia kuteuka kiwiko cha mkono wake. Majeraha hayo yalimlazimu nyota huyo kukosa michuano ya Euro 2012 ambapo Hispania walitawadhwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo na pia kuenguliwa katika kikosi cha nchi hiyo kilichopo nchini Brazil kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
FABRIGAS AFUNGUKA KUHUSU REAL MADRID-USAJILI BALE
Kiungo nyota wa klabu ya Barcelona na timu ya Tifa ya hispain Cesc Fabregas ametanabisha kuwa klabu ya Real Madrid ya Hispania watakuwa wametwanga maji kwenye kinu mtungi endapo kama wakivunja rekodi ya usajili kwa kulipa euro milioni kwa kumsajili mshambuliaji nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Gareth Bale. ambaye ni Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Wales amekuwa akihusishwa kwenda Santiago Bernabeu huku kukiwa na tetesi kuwa ada ya uhamisho wake inafikia paundi milioni 85 ambayo itavunja rekodi ya sasa ya euro milioni 94 ambazo Madrid aliipa Manchester United kwa ajili ya Cristiano Ronaldo. Hatahivyo, Fabregas haelewi kwanini klabu hiyo inajiandaa kulipa kiasi hicho kikubwa cha pesa huku wakijua kuwa kuna tatizo kubwa la mdodoro wa kiuchumi unaizikumba baadhi ya nchi wakiwemo wao. Fabregas pia alirejea kauli yake kwamba angependa kuendelea kubakia Barcelona na kushangaa baadhi ya watu wakizungumza kwamba anataka kurejea katika Ligi Kuu nchini Uingereza.
AVB AWAKANA PARIS SAINT GERMAN-UKOCHA
Andre Villas-Boas kocha wa Tottenham ameripotiwa kuitupilia mbali ofa ya kuifundisha club Paris Saint-Germain lengo kuu likiwa ni kubaki ndani ya White Hart Lane {Tottenham}.
Mabingwa hao wa Ufaransa walimhitaji AVB Mreno huyo kurithi mikoba ya Carlo Ancelotti ambaye anatarajiwa kuelekea nndani ya Bernebeu Real Madrid lakini sasa mawzo yote yamehamia kwa Fabio Capello.
Inafahamika Villas-Boas alipewa ofa ya Mkataba wa miaka mitatu na mabilionea wa Qatari wanaoimiliki PSG baada ya majadiliano na wakala wake, Carlos Goncalves, lakini mwalimu huyo kijana wa miaka 35 anataka kufanya mambo makubwa katika club ya Spurs ambapo walimchukuwa msimu uliopita akitokea katika club ya chelsea baada ya kutupiwa virago Chelsea.
Katika Taarifa za jana usiku nchini Ufaransa zimesema kuwa kocha wa zamani wa England, Capello atakuwa mwalimu mpya wa PSG kwa Mkataba wa mwaka mmoja.
Kocha wa zamani wa England, Capello anatazamiwa kuwa mpango B wa PSG, licha ya kwamba bado ana Mkataba wa mwaka mmoja Urusi.
Urusi ipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil,na kuna uwezekano Capello akarejea katika timu hiyo ya taifa baada ya msimu mmoja na PSG kukamilisha majukumu yake katika Kombe la Dunia.
KESHI AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUWA MAKINI LANGONI

Katika mchezo huo uliopigwa huko Belo Horizonte mashabiki waliohudhuria mchezo huo walionyesha kuwa upande wa Tahiti na mabao ya Nigeria hayakuonyesha kuwakuna mashabiki hao lakini Keshi hajali suala hilo. Keshi amesema unapokuwa mchezaji wa kulipwa mambo kama hayo ni ya kawaida kukutana nayo kitu cha msingi ni kuhakikisha unapata matokeo muhimu ili uweze kusonga mbele. Michuano hiyo inaendelea tena kesho ambapo wenyeji Brazil watakwaana na Waamerika Kusini wenzao Mexico katika Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro.
BENZEMA VS RIBERY KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA NGONO"
Wanandinga wa Kimataifa wa Ufaransa, Franck Ribery na Karim Benzema wamefikishwa mahakamani leo jijini Paris wakituhumiwa kutembea na mwanamke anayejiuza mwenye umri mdogo. Ribery ambaye anacheza katika klabu ya Bayern Munich na Benzema anayekipiga katika klabu ya Real Madrid watakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini inayozidi euro 45,000 kama wakikutwa na hatia ya kutenda kosa hilo. Nyota hao wote wawili walikana tuhuma hizo huku mwanamke huyo aitwaye Zahia Dehar alitoa ushahidi kuwa wote wawili hawakuwa wakijua kama hajafikisha umri huo wakati wakifanya naye mapenzi mwaka 2008 na 2009. Pamoja na kwamba umri halali ni miaka 15 nchini Ufaransa lakini kumlipa mwanamke anayejiuza chini ya umri wa miaka 18 ni kosa.
Subscribe to:
Posts (Atom)