Katika taarifa za takwimu za
ofisi ya msajili jijini La paz, Bolivia miaka 17 ijayo vijana wengi wa
kiume wanaoishi katika mji huo watakuwa wakiitwa jina la mshambuliaji mpya wa fc barca Neymar. Katika
taarifa iliyotolewa na gazeti moja nchini humo watoto 20 kati ya 100
wanaozaliwa katika mji mkuu huo wan chi hiyo wamepewa jina la nyota huyo
mpya wa Barcelona ambaye amewateka mashabiki dunia nzima kutokana na
kiwango cha hali ya juu alichokionyesha katika michuano ya Kombe la
Shirikisho. Ofisa
mmoja aliyetambulika kwa jina la Remigio Condori amesema wazazi wengi
katika mji huo wanachagua jina la Neymar kwakuwa ndio liko katika
fasheni ambapo miaka 17 ijayo vijana wengi wa kiume watakuwa wakiitwa
jina hilo. Neymar
ambaye amsajili na Barceona kwa ada ya euro milioni 57, alifunga mabao
mawili katika ushindi wa mabao 4-0 iliyopata Brazil dhidi ya Bolivia
April mwaka huu.
Wednesday, July 3, 2013
ARSENAL KATIKA MVUTANO NA REAL MADRID-HIGUAIN"

Klabu hizo mbili zimekuwa katika mvutano kuhusu ada ya uhamisho wa nyota huyo ambapo Arsenal wameonekana kuwa tayari kutoa kitita cha euro milioni 25, wakati Madrid wao wanataka ada iwe euro milioni 25.5. Kumekuwa na taarifa kuwa Arsenal wameshafikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo ambapo ataanza na mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki, mshahara ambao utamfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa zaidi kwenye klabu hiyo wakiwemo Theo Walcott na Thomas Vermaelen. Higuain ambaye nia raia wa Argentina inasenekana alikuwa akilipwa kiasi cha paundi 64,000 kwa wiki akiwa Madrid.
Tuesday, July 2, 2013
BRAZIL HAINA UBAVU DHIDI YA HISPAIN IJAPO KUWA IMESHINDA 3-0

NGULI wa soka Duniani Raia wa Argentina, Diego Maradona anaamini kuwa Hispania wasingepoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Brazil kama wangecheza katika uwanja huru. Mabingwa hao wa Ulaya na Dunia walitandikwa mabao 3-0 katika Uwanja wa Maracana na Maradona mwenye umri wa miaka 52 anaamini kuwa mazingira yalikiathiri kikosi cha Hispania kinachonolewa na Vincente Del Bosque. Akihojiwa na waandishi wa habari katika ziara ya nchini Indonesia Maradona amesema Hispania hawakuwa na bahati kwakuwa walikuwa wakicheza nchini Brazil na anaamini kuwa nchi hiyo isingewafunga kama mchezo huo ungechezwa katika uwanja huru. Maradona pia hakusita kumsifia Lionel Messi na kudai kuwa bado ni mchezaji bora na mahasimu wake Cristiano Ronaldo na Neymar bado hawajafikia ubora wake.
NEYMAR NA ALBA KUFANYIWA UPASUAJI WA MAFINDIFINDO YA SHIGONI"TOSEZI"

Mkali mpya wa FC Barcelona, Neymar na beki Jordi Alba wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mafindofindo Ijumaa na wanatarajiwa kupona baada ya siku 10. Upasuaji huo ulipangwa kufanyika baada ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho iliyofanyika jijini Rio de Janeiro Jumapili iliyopita ambapo Brazil iliisambaratisha Hispania kwa mabao 3-0. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo Neymar anatarajiwa kufanyiwa upasuaji huo huko Rio na baadhi ya madaktari wa Barcelona wanakuwepo kusaidia. Wakati Alba mwenye miaka 24 yeye atafanyiwa upasuaji wake siku hiyohiyo lakini katika kliniki iliyopo karibu na jiji la Barcelona na wote wanatarajiwa kupona ndani siku 10 baada ya upasuaji huo.
ARSENAL SASA YAJIWEKA KAMILI GADO KWA MSIMU MPYA WA BPL NCHINI UINGEREZA"
Wakiwa chini ya kocha Mfaransa, Aserne Wenger Timu ya soka ya Arseanal wamefanikiwa kuinasa saini ya nyota kinda wa kimataifa
kutoka nchini Ufaransa, Yaya Sanogo kwa kumpa mkataba mrefu Emirates.
Kinda
huyo kwa sasa yupo na timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya umri
wa miaka 20m katika fainali za Kombe la Dunia la vijana chini ya umri
wa miaka 20 huku akiwa amefumania nyavu mara mbili kati ya matatu ya
timu yake nchini Uturuki.
Akicheza
ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa, Sanogo amefunga mabao tisa
katika mechi 13 huku akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara.

Mtu mwenye dili kwa sasa: Sanogo amejijengee nafasi nzuri sana katika taifa la Ufaransa

Nyota
wengine wa kutua Emirates? Higuain (kushoto) na Rooney (kulia) pia wapo
katika rada za Wenger ambaye anataka kupata nyota wakali wa kuimarisha
kikosi chake msimu ujao
Gonzalo
Higuain na Wayne Rooney wameripotiwa kuwa katika mipango ya Wenger
msimu ujao, lakini kocha huyo raia wa Ufaransa amevutiwa na kinda
Sanogo.
‘Sanogo
ni mchezaji mzuri sana atakayesaini kwetu, ameonesha kiwango kikubwa
katika klabu yake ya Auxerre na katika kikosi cha timu ya taifa chini ya
umri wa miaka 20″. Alisema Wenger.
MTIBWA SUGAR YAJIPANGA KUJIWEKA SAWA NA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA WA LIGI KUU TZ BARA"
![]() |
Kikosi cha mtibwa sukari |
Mwenyekiti
mwenye dhamana ya kuiongoza timu hiyo kubwa nchini Tanzania yenye
historia ya kuzisumbua Simba na Yanga na kutwaa taji miaka ya nyuma,
Jamal Baiser amesema kwa sasa wanafanya mipango ya kusajili wachezaji wa
kuziba nafasi zilizoachwa wazi kufuatia baadhi ya wachezaji kutimka
klabuni hapo.
“Mpaka
sasa hatujasajili wachezaji, lakini mipango yetu ni kusajili wachezaji
wapatao watano, na baada ya kukamilisha taratibu zote, tutawajulisha
mashabiki wetu. Kikubwa ni kwamba, tunahitaji kuwa na timu nzuri zaidi
kuliko misimu mitatu iliyopita”. Alisema Baiser.
Baiser
alisema kwa muda mrefu sasa, Mtibwa sugar haifanyi vizuri sana wala
vibaya sana, lakini kwa msimu ujao wanajiandaa kuwa timu bora zaidi,
huku wakichanganya damu changa na kongwe katika kikosi chao.
Mwenyekiti
huyo alisema timu yao amepoteza baadhi ya wachezaji akiwemo Issa Rashid
“Baba Ubaya” aliyejiunga na wekundu wa Msimbazi Simba pamoja na Hussein
Javu anayesemekana kusaini yanga, lakini wana wachezaji wengine wa
kuziba nafasi zao na wengine watawasajili.
“Walikuwa
wachezaji muhimu sana, lakini hatuna jinsi, soka ni ajira yao, hatuna
uwezo wa kuwabania nafasi ya kucheza klabu nyingine, ila kiuhakika
tunao wachezaji wengi sana wa kuziba nafasi zao nab ado tunatafuta nyota
wengine wa kuwasainisha”. Alisema Baiser.
Akizungumzia
suala la Javu kusaini Yanga, Baiser alisema Mtibwa Sugar ilikuwa na
mkataba naye, lakini Yanga waliomba ruhusa ya kuzungumza naye na wao
wakakubali.
“Walituomba
kuongea na Javu, tuliwaruhusu. Kama wamekubaliana na kumpa mkataba sisi
bado hatuna taarifa ofisini, Yanga bado hawajaja kufanya taratibu za
uhamishoi, kwahiyo hatujui kama wameshamalizana naye, hivyo sitaki
kulizungumzia sana kwa sasa, wakati utafika nitazungumza”. Alisema
Baiser.
Baiser alisema Javu alikuwa mchezaji muhimu sana, lakini wanajipanga kutafuta mbadala wake.
WEBB ASEMA WAAMUZI WANAIMANI KUBWA NA MFUMO MPYA WA TEKNOLOGIA YA MSTARI WA GOLI
Howard Webb Mwamuzi wa
Uingereza amedai kuwa waamuzi wana imani kubwa na mfumo mpya wa
teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli ambao utatumika katika
michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Hakuna
bao lolote kati ya mabao 68 yaliyofungwa katika michuano ya Kombe la
Shirikisho lililohitaji teknologia hiyo ambayo ndio ilikuwa imeanza
kutumika kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo. Lakini
Webb aliwaambia waandishi wa habari jijini Rio de Janeiro kwamba
uhakika wa mfumo huo unawapa faida kubwa na waamuzi wana imani kwa kiasi
kikubwa na mfumo huo ambao umefungwa na kampuni ya Kijerumani
iliyoshinda zabuni hiyo ya GoalControl. Webb
amesema hawana shaka na uthabiti wa mfumo huo na umeonekana kufanya
kazi vyema hivyo anadhani utaendelea kufanya kazi hata katika michuano
ya Kombe la Dunia mwakani. Webb
ambaye alichezesha mchezo wa fainali kati ya Kombe la Dunia mwaka 2010
kati ya Hispania na Uholanzi nchini Afrika Kusini ni mmoja katika orodha
ya waamuzi 52 ambao watachujwa kwa ajili ya michuano hiyo mwakani.
Subscribe to:
Posts (Atom)