Howard Webb Mwamuzi wa
Uingereza amedai kuwa waamuzi wana imani kubwa na mfumo mpya wa
teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli ambao utatumika katika
michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Hakuna
bao lolote kati ya mabao 68 yaliyofungwa katika michuano ya Kombe la
Shirikisho lililohitaji teknologia hiyo ambayo ndio ilikuwa imeanza
kutumika kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo. Lakini
Webb aliwaambia waandishi wa habari jijini Rio de Janeiro kwamba
uhakika wa mfumo huo unawapa faida kubwa na waamuzi wana imani kwa kiasi
kikubwa na mfumo huo ambao umefungwa na kampuni ya Kijerumani
iliyoshinda zabuni hiyo ya GoalControl. Webb
amesema hawana shaka na uthabiti wa mfumo huo na umeonekana kufanya
kazi vyema hivyo anadhani utaendelea kufanya kazi hata katika michuano
ya Kombe la Dunia mwakani. Webb
ambaye alichezesha mchezo wa fainali kati ya Kombe la Dunia mwaka 2010
kati ya Hispania na Uholanzi nchini Afrika Kusini ni mmoja katika orodha
ya waamuzi 52 ambao watachujwa kwa ajili ya michuano hiyo mwakani.