MWANADADA nyota dunia katika
tenisi kutoka Marekani, Serena Williams ametolewa nje katika michuano ya
Wimbledon baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Sabine Lisicki wa
Ujerumani kwa 6-2 1-6 6-4. Williams
ambaye mbali na kupewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji hilo pia alikuwa
bingwa mtetezi wa michuano hiyo aliyonyakuwa mwaka jana. Kwa
upande mwingine bingwa wa zamani wa michuano hiyo Petra Kvitova
alifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya
kumgaragaza Carla Suarez wa Hispania kwa 7-5 6-3. Mashindano
ya Wimbledon mwaka huu yamekuwa sio mazuri kwa nyota wengi wanaoshika
nafasi za juu katika orodha za ubora wa mchezo huo duniani baada ya
Maria Sharapova anayeshika namba mbili kuenguliwa katika mzunguko wa
pili huku Victoria Azarenka anayeshika namba tatu yeye akijitoa baada ya
kupata majeraha.