WAKALI wa Darajani Club ya soka ya Chelsea imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa klabu ya Vitesse Arnhem ya Uholanzi, Marco van Ginkel. Kiungo
huyo mwenye miaka 20 ambaye ametokea katika shule ya watoto ya Vitesse
kabla ya kupata namba katika kikosi cha kwanza April mwaka 2010
atajiunga na Chelsea baada ya kukamilisha taratibu za vipimo vya afya. Van
Ginkel amekuwa akicheza katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini
ya miaka 21 ya Uholanzi na mara moja ameshaitwa katika kikosi cha timu
ya wakubwa akiingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya
Ujerumani Novemba mwaka jana. Kiungo
huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na meneja mpya wa Chelsea Jose
Mourinho kufuatia kusajiliwa kwa mshambuliaji Andre Schuerrle ktoka
Leverrkusen mwezi uliopita.
Thursday, July 4, 2013
YONDAN AWA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU TZ 2012-2013
INJINI ya Yanga Sc beki Kevin
Patrick Yondan amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 na kuzawadiwa kitita cha Sh. Milioni
5. Hata hivyo,
katika hafla ya kutoa zawadi za washindi wa Ligi Kuu msimu uliopita
kutoa wadhamini, Vodacom Tanzania zilizofanyika katika hoteli ya Double
Tree, Dar es Salaam jana usiku, Yondan hakuwepo na tuzo yake alipokelewa
na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, kutoka kwa mgeni rasmi,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara. Yondan
ambaye alikuwa katika msimu wake wa kwanza Yanga SC, yuko kwenye kambi
ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo
dhidi ya Uganda Julai 13, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kipa
chipukizi wa Tanzania Prisons FC ya Mbeya, David Burhan alishinda tuzo
ya kipa bora wa Ligi Kuu na kupewa Sh. Milioni 5, wakati mfungaji bora,
Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast wa Azam FC alipewa Milioni 5
pia na Fully Maganga wa JKT Mgambo alipewa tuzo ya mchezaji mwenye
nidhamu na kuzawadiwa Milioni 5. Kocha
mpya wa Simba, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ ameshinda
tuzo ya kocha bora kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa na Kagera Sugar
msimu uliopita na kuzawadiwa Milioni 7.5 sawa na refa bora, Simon
Mbelwa. Yanga SC
pamoja na kuzawadiwa Sh. Milioni 70 za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu,
waliongezewa Milioni 15 kwa kuwa timu yenye nidhamu zaidi kwenye ligi
hiyo msimu uliopita, hivyo kuondoka na jumla ya kiasi cha Sh. Milioni
85. Azam FC
washindi wa pili kwa msimu wa pili mfululizo, walizawadiwa Sh. Milioni
35, Simba SC washindi wa tatu Milioni 25 na Kagera Sugar washindi wa nne
walipewa Milioni 20. Kwa
upande wa zawadi za wachezaji wa timu za vijana za klabu za Ligi Kuu,
Hamisi Saleh (JKT Ojoro), Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), Hassan
Dilunga (Ruvu Shooting), Chande Magoja (Mgambo JKT), Tonny Kavishe
(Mgambo JKT) na Rajab Zahir (Mtibwa Sugar), wote wamezawadiwa Sh.
Milioni 1 kila mmoja. Zawadi
za wachezaji wa timu za vijana, walizozawadiwa kwa kuzichezea mechi
nyingi timu zao za wakubwa katika Ligi Kuu, zimetoka Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF).
Rajab Zahir amesaini Yanga SC na tayari amejiunga nayo.
Rajab Zahir amesaini Yanga SC na tayari amejiunga nayo.
Wednesday, July 3, 2013
USAJILI WAPAMBA MOTO BARANI ULAYA
Stoke City wamemsaini Beki wa Kimataifa wa Timu ya Spain U-21 Marc Muniesa anaecheza Barcelona kwa Uhamisho wa bure.
Muniesa, Miaka 21, ni mmoja wa Wachezaji
wa Spain ambayo ilitwaa Ubingwa wa EURO 2013 kwa U-21 hivi karibuni na
anajiunga na Stoke kwa Mkataba wa Miaka minne.
Huyu ni Mchezaji wa pili kuchukuliwa na
Meneja mpya wa Stoke, Mark Hughes, baada ya Wiki iliyopita kumsaini Erik
Pieters kutoka PSV Eindhoven.
SWANSEA YAKUBALIANA NA LIVERPOOL KUHUSU JONJO
Swansea City imeafikiana na Liverpool
Ada ya Pauni Milioni 6 ya kumhamisha Kiungo Jonjo Shelvey na Mchezaji
huyo sasa atakutana na Swansea ili kukamilisha makubaliano ya Maslahi
yake binafsi.
Jonjo Shelvey, Miaka 21, alisainiwa na
Liverpool kutoka Charlton Athletics kwa Dau la Pauni 1.7 Miaka mitatu
iliyopita lakini akiwa Anfield kupata namba kwake kumekuwa nadra na
Meneja Brendan Rodgers amemruhusu kutafuta Klabu nyingine.
Shelvey aliichezea England kwa mara ya
kwanza Novemba Mwaka jana ilipofungwa na Sweden na pia amecheza Mechi 17
za Ligi huko Anfield Msimu uliopita.
Jana Swansea ilitangaza kuwasaini
Wachezaji watatu wengine ambao ni Alejandro Pozuelo, Miaka 21, kutoka
Real Betis ya Spain, Kipa wa Miaka 17, Gregor Zabret kutoka Klabu ya
Slovenia NK Domzale na Alex Gogic, Kiungo wa Miaka 19 kutoka Klabu ya
Greece, Olympiakos.

Katika azma yao ya kukiimarisha Kikosi
chao kuwa na nguvu na Misuli inayostahili kwa ajili ya Msimu mpya, Klabu
ya Arsenal imemuajiri Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Ireland wa
Mchezo wa Raga, Jerry Flannery, kuwa Kocha wao mpya wa kujenga nguvu,
musili na stamina kwa Wachezaji wao.
Flannery, Miaka 34, alistaafu mapema kucheza Raga baada ya kuumia Misuli za Mguu.
MOURINHO AZUNGUMZA NA MARCO VAN GINKEL
Chelsea imefanya mazungumzo na Kiungo wa Vitesse Arnhem, Marco van Ginkel, ili ahamie Stamford Bridge.
Van Ginkel, Miaka 20, ameshakutana na Jose Mourinho na Alhamisi ataongea na Klabu yake ya Uholanzi ili apate baraka za Uhamisho.
Marco van Ginkel alijiunga na Vitesse
Arnhem akiwa na Miaka 7 tu na kupanda kwenye Vyuo vya Klabu hiyo hadi
Aprili 2010 alipocheza Timu ya Kwanza kwa mara ya kwanza.
Van Ginkel anathaminiwa kuwa na Dau la Pauni Milioni 8 na Mkataba wake na Klabu yake unamalizika Juni 2015.
Ikiwa Uhamisho huu utakamilika, huu
utakuwa ni usajili wa pili kwa Jose Mourinho baada ya Wiki iliyopita
kumnasa Mchezaji wa Kimataifa wa Germany, Andre Schurrle, kutoka Klabu
ya Bundesliga, Bayer Leverkusen.
MESSI ASEMA BARCELONA ILIFANYA SAHIHI KUMNASA NEYMAR
Mshambuliaji nyota duniani wa
kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi anaamini kuwa
klabu hiyo ilifanya jambo sahihi kumsajili Neymar katika kampeni yao ya
kutetea taji La Liga na kufanya vyema katika michuano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu ujao. Neymar
mwenye umri wa miaka 21 alikamilisha usajili wake uliogharimu kiasi cha
euro milioni 57 akitokea Santos Juni mwaka huu ingawa hatahivyo
wakosoaji wanadai Barcelona ilifanya makosa kutumia fedha nyingi
kumsajili nyota huyo ambaye hajawahi kucheza Ulaya.
Lakini baada ya kufunga mabao manne katika michuano ya Kombe la Shirikisho ilikiwemo bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa wa Dunia Hispania wakooaji hao watakuwa wameshapata majibu ya maswali yao na Messi anategemea nyota huyo kufanya makubwa zaidi atakapokuwa Barcelona. Messi amesema anategemea Neymar ataleta mchango mkubwa katika klabu hiyo kama akiendelea kucheza katika kiwango cha juu kama ilivyo kwa timu yake ya taifa na Santos. Barcelona ilifanikiwa kunyakuwa taji la La Liga msimu uliopita lakini walipata kipigo kikubwa kutoka Bayern Munich kwenye mechi za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo waling’olewa kwa kufungw ajumla ya mabao 7-0 katika mechi mbili walizocheza.
Lakini baada ya kufunga mabao manne katika michuano ya Kombe la Shirikisho ilikiwemo bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa wa Dunia Hispania wakooaji hao watakuwa wameshapata majibu ya maswali yao na Messi anategemea nyota huyo kufanya makubwa zaidi atakapokuwa Barcelona. Messi amesema anategemea Neymar ataleta mchango mkubwa katika klabu hiyo kama akiendelea kucheza katika kiwango cha juu kama ilivyo kwa timu yake ya taifa na Santos. Barcelona ilifanikiwa kunyakuwa taji la La Liga msimu uliopita lakini walipata kipigo kikubwa kutoka Bayern Munich kwenye mechi za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo waling’olewa kwa kufungw ajumla ya mabao 7-0 katika mechi mbili walizocheza.
KUNANI HAPO?BOLOVIA MIAKA 17 IJAYO VIJANA KUITWA NEYMAR"
Katika taarifa za takwimu za
ofisi ya msajili jijini La paz, Bolivia miaka 17 ijayo vijana wengi wa
kiume wanaoishi katika mji huo watakuwa wakiitwa jina la mshambuliaji mpya wa fc barca Neymar. Katika
taarifa iliyotolewa na gazeti moja nchini humo watoto 20 kati ya 100
wanaozaliwa katika mji mkuu huo wan chi hiyo wamepewa jina la nyota huyo
mpya wa Barcelona ambaye amewateka mashabiki dunia nzima kutokana na
kiwango cha hali ya juu alichokionyesha katika michuano ya Kombe la
Shirikisho. Ofisa
mmoja aliyetambulika kwa jina la Remigio Condori amesema wazazi wengi
katika mji huo wanachagua jina la Neymar kwakuwa ndio liko katika
fasheni ambapo miaka 17 ijayo vijana wengi wa kiume watakuwa wakiitwa
jina hilo. Neymar
ambaye amsajili na Barceona kwa ada ya euro milioni 57, alifunga mabao
mawili katika ushindi wa mabao 4-0 iliyopata Brazil dhidi ya Bolivia
April mwaka huu.
ARSENAL KATIKA MVUTANO NA REAL MADRID-HIGUAIN"

Klabu hizo mbili zimekuwa katika mvutano kuhusu ada ya uhamisho wa nyota huyo ambapo Arsenal wameonekana kuwa tayari kutoa kitita cha euro milioni 25, wakati Madrid wao wanataka ada iwe euro milioni 25.5. Kumekuwa na taarifa kuwa Arsenal wameshafikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo ambapo ataanza na mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki, mshahara ambao utamfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa zaidi kwenye klabu hiyo wakiwemo Theo Walcott na Thomas Vermaelen. Higuain ambaye nia raia wa Argentina inasenekana alikuwa akilipwa kiasi cha paundi 64,000 kwa wiki akiwa Madrid.
Tuesday, July 2, 2013
BRAZIL HAINA UBAVU DHIDI YA HISPAIN IJAPO KUWA IMESHINDA 3-0

NGULI wa soka Duniani Raia wa Argentina, Diego Maradona anaamini kuwa Hispania wasingepoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Brazil kama wangecheza katika uwanja huru. Mabingwa hao wa Ulaya na Dunia walitandikwa mabao 3-0 katika Uwanja wa Maracana na Maradona mwenye umri wa miaka 52 anaamini kuwa mazingira yalikiathiri kikosi cha Hispania kinachonolewa na Vincente Del Bosque. Akihojiwa na waandishi wa habari katika ziara ya nchini Indonesia Maradona amesema Hispania hawakuwa na bahati kwakuwa walikuwa wakicheza nchini Brazil na anaamini kuwa nchi hiyo isingewafunga kama mchezo huo ungechezwa katika uwanja huru. Maradona pia hakusita kumsifia Lionel Messi na kudai kuwa bado ni mchezaji bora na mahasimu wake Cristiano Ronaldo na Neymar bado hawajafikia ubora wake.
Subscribe to:
Posts (Atom)