INJINI ya Yanga Sc beki Kevin
Patrick Yondan amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 na kuzawadiwa kitita cha Sh. Milioni
5. Hata hivyo,
katika hafla ya kutoa zawadi za washindi wa Ligi Kuu msimu uliopita
kutoa wadhamini, Vodacom Tanzania zilizofanyika katika hoteli ya Double
Tree, Dar es Salaam jana usiku, Yondan hakuwepo na tuzo yake alipokelewa
na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, kutoka kwa mgeni rasmi,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara. Yondan
ambaye alikuwa katika msimu wake wa kwanza Yanga SC, yuko kwenye kambi
ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo
dhidi ya Uganda Julai 13, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kipa
chipukizi wa Tanzania Prisons FC ya Mbeya, David Burhan alishinda tuzo
ya kipa bora wa Ligi Kuu na kupewa Sh. Milioni 5, wakati mfungaji bora,
Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast wa Azam FC alipewa Milioni 5
pia na Fully Maganga wa JKT Mgambo alipewa tuzo ya mchezaji mwenye
nidhamu na kuzawadiwa Milioni 5. Kocha
mpya wa Simba, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ ameshinda
tuzo ya kocha bora kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa na Kagera Sugar
msimu uliopita na kuzawadiwa Milioni 7.5 sawa na refa bora, Simon
Mbelwa. Yanga SC
pamoja na kuzawadiwa Sh. Milioni 70 za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu,
waliongezewa Milioni 15 kwa kuwa timu yenye nidhamu zaidi kwenye ligi
hiyo msimu uliopita, hivyo kuondoka na jumla ya kiasi cha Sh. Milioni
85. Azam FC
washindi wa pili kwa msimu wa pili mfululizo, walizawadiwa Sh. Milioni
35, Simba SC washindi wa tatu Milioni 25 na Kagera Sugar washindi wa nne
walipewa Milioni 20. Kwa
upande wa zawadi za wachezaji wa timu za vijana za klabu za Ligi Kuu,
Hamisi Saleh (JKT Ojoro), Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), Hassan
Dilunga (Ruvu Shooting), Chande Magoja (Mgambo JKT), Tonny Kavishe
(Mgambo JKT) na Rajab Zahir (Mtibwa Sugar), wote wamezawadiwa Sh.
Milioni 1 kila mmoja. Zawadi
za wachezaji wa timu za vijana, walizozawadiwa kwa kuzichezea mechi
nyingi timu zao za wakubwa katika Ligi Kuu, zimetoka Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF).
Rajab Zahir amesaini Yanga SC na tayari amejiunga nayo.
Rajab Zahir amesaini Yanga SC na tayari amejiunga nayo.