WAKALI wa Darajani Club ya soka ya Chelsea imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa klabu ya Vitesse Arnhem ya Uholanzi, Marco van Ginkel. Kiungo
huyo mwenye miaka 20 ambaye ametokea katika shule ya watoto ya Vitesse
kabla ya kupata namba katika kikosi cha kwanza April mwaka 2010
atajiunga na Chelsea baada ya kukamilisha taratibu za vipimo vya afya. Van
Ginkel amekuwa akicheza katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini
ya miaka 21 ya Uholanzi na mara moja ameshaitwa katika kikosi cha timu
ya wakubwa akiingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya
Ujerumani Novemba mwaka jana. Kiungo
huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na meneja mpya wa Chelsea Jose
Mourinho kufuatia kusajiliwa kwa mshambuliaji Andre Schuerrle ktoka
Leverrkusen mwezi uliopita.