ISCO ASEMA LENGO KUU NI KUISAIDIA MADRID KUTWAA UEFA
Baada ya kusajiliwa katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi na club ya
Real Madrid Isco ametanabaisha na kusama kuwa lengo lake kubwa ni kukisaidia kikosi cha timu
hiyo kinachonolewa na kocha Carlo Ancelotti kushinda taji la Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu ujao. Kocha
aliyeoondoka Jose Mourinho ameinoa klabu hiyo kwa kipindi cha miaka
mitatu na kuisadia klabu hiyo kufika nusu fainali ya ligi hiyo mara tatu
lakini bado wamekuwa na kiu ya muda mrefu ya kulisubiria taji lao 10
katika michuano hiyo. Akijiunga
na Madrid kwa mkataba wa miaka mitano kutokea Malaga, Isco sasa ana
malengo ya kuiwezesha klabu hiyo kuendeleza historia yake kwa kunyakuwa
taji hilo mapema iwezekanavyo. Akihojiwa
katika utambulisho rasmi, Isco amesema watu wote wanahusiana na klabu
hiyo wamekuwa na kiu ya taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na ni mategemeo
yake kwamba msimu unaokuja taji hilo litatua Santiago Bernabeu.