Saturday, March 29, 2014

KITENDALIWI BADO KIPO KUTWAA UBINGWA VPL NANI KATI YA AZAM au YANGA.

Utata wa klabu gani itatwaa Ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu hakichateguliwa kwasasa, na hapo kesho kutakuwa na  mechi muhimu kwa timu zinazopigiwa upatu  wa kutwaa ubingwa, Yanga na Azam fc.Vinara Azam fc watakuwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kukabiliana na kikosi cha Simba, wakati mabingwa watetezi, Young Africans watakuwa na kibarua kizito mbele ya wapiga kwata wa Mgambo JKT, kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani, jijini Tanga.
SAM_2252
Mechi ya Azam fc dhidi ya Simba sc itakuwa ngumu kwa klabu zote, lakini kwa Wana Lambalamba ina uzito wa hali ya juu katika mbio zao za kutwaa ubingwa.
Kama watapoteza mechi hiyo, halafu Yanga wakapata ushindi jijini Tanga, Azam watajiweka mazingira magumu zaidi ya kubeba mwari wao wa kwanza tangu waingie  ligi kuu msimu wa 2008/2009.
SAM_2257Yanga nao watatakiwa kuwa na mipango mizuri ya uwanjani dhidi ya Magambo kesho, kwasababu rekodi ya nyuma inaonesha wapinzani wao wamekuwa wagumu kufungwa Mkwakwani.
Hukutakuwa na sababu yoyote kwa kikosi cha Yanga kuwadharau Mgambo kwakuwa wapo katika mstari mwekundu wa kushuka daraja.
Maskari hawa wa  Jeshi la kujenga Taifa wanahitaji ushindi kwa nguvu zote kwasababu ndio matokeo pekee yanayowafaa kwasasa.
VPL-LIGI KUU VODACOM
RATIBA:
Jumamosi Machi 29
Ashanti United v JKT Oljoro
Jumapili Machi 30
Mbeya City v Tanzania Prisons
Kagera Sugar v Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar v Coastal Union
JKT Ruvu v Rhino Rangers
Azam FC v Simba
Mgambo JKT v Yanga 
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
22
14
8
0
30
50
2
Yanga SC
21
13
7
1
27
46
3
Mbeya City
22
11
9
2
12
42
4
Simba SC
22
9
9
4
16
36
5
Kagera Sugar
21
8
8
5
3
32
6
Coastal Union
22
6
11
5
2
29
7
Ruvu Shooting
20
7
7
6
-4
28
8
Mtibwa Sugar
21
6
8
7
-1
26
9
JKT Ruvu
22
8
1
13
-15
25
10
Prisons FC
21
3
10
8
-9
19
11
Ashanti United
21
4
6
11
-18
18
12
Mgambo JKT
21
4
6
11
-19
18
13
JKT Oljoro
22
2
9
11
-17
15
14
Rhino Rangers
22
2
7
13
-17

13

KONGAMANO LA VIJANA ELIMU YA JUU KUFANYIKA KESHO DAR

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yenye jukumu la kusimamia sekta ya Vijana nchini imeandaa Kongamano la Vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano Wetu Miaka 50 tangu kuzaliwa kwake. 
 Kongamano hili la Vijana kuhusu Muungano linafanyika Jumapili Machi 30, 2014  kuanzia Saa  5:00 Asubuhi katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam na litarushwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa, TBC One na TBC Taifa.
Kongamano hili ni sehemu ya sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu kuasisiwa kwake na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Aprili 26, 1964.
 Kauli mbiu ya sherehe za Miaka 50 ya Muungano ni “UTANZANIA WETU NI MUUNGANO WETU, TUULINDE, TUUIMARISHE NA KUUDUMISHA”.
Lengo la Kongamano hili ni kuzungumzia Wajibu wa Vijana katika kuimarisha Muungano ambao mwezi  ujao unafikisha miaka 50.
Washiriki wa Kongamano hili  ni vijana  300 kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo Tanzania Bara na Zanzibar. 
BAVICHAWashiriki wa Kongamano hili watapata fursa ya kuwasikia watoa mada ambao ni Wahadhiri wa Vyuo Vikuu Prof. Gaudens Mpangala atakayewasilisha mada kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano, Miaka 50 tangu kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Aidha mada kuhusu Mapendekezo ya Katiba Mpya kwa Mustakabali wa Muungano wetu itawasilishwa na Prof. Issa Shivji.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari nchini wanakaribishwa kushiriki kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu kongamano hili.
Imetolewa na Idara ya Habari –  MAELEZO
29 Machi 2014

Friday, March 28, 2014

BODI YA LIGI YASEMA SINGANO LAZIMA ALE KIBANO

Wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likisubiri taarifa kutoka serikalini kuhusu thamani ya kioo cha mlango kilichovunjwa na winga wa Simba, Ramadhan Singano ‘Messi’, Bodi ya Ligi imesema kuwa lazima Messi akumbane na rungu jingine kutoka kwao.
Bodi hiyo imesema kuwa inataka kutoa adhabu hiyo ili iwe kama fundisho kwa wengine kwani kilikuwa ni kitendo cha kudhamiria.
Messi alivunja kioo hicho Jumapili iliyopita baada ya timu yake kuchezea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo hasira za kufungwa akazihamishia kwenye mlango wa vyumba vya kubadilishia nguo kwa kuupiga teke.
Ofisa Mtendaji wa Bodi la Ligi, Silas Mwakibinga alisema licha ya mchezaji huyo kulipa fidia za kioo hicho, bodi watakaa kuangalia ni adhabu gani atatakiwa kupewa kama onyo.
“Lilikuwa tukio ambalo kila mmoja aliliona, siyo kusema ilikuwa bahati mbaya, hivyo baada ya mambo mengine kumalizika, suala lake haliwezi kuachwa hivihivi, kuna adhabu nyingine itatolewa kama fundisho kwa wote,” alisema Mwakibinga.
Tayari mchezaji huyo ameomba radhi kwa kitendo chake kwa kile alichosema zilikuwa ni hasira za kukosa mabao ya wazi, hususan dakika ya mwisho alipobaki na mlinda mlango wa Coastal.

BPL:ARSENAL KUIKARIBISHA MAN CITY UWANJANI EMIRATES".

Kesho Jumamosi Ligi Kuu nchini uingereza inaingia tena kilingeni kwa michezo 7 kuanzia Mechi ya Saa Tisa na dakika 45 katika uwanja wa Old Trafford kati ya Manchester United na Aston Villa na kumalizika Usiku kwa Bigi Mechi Uwanjani Emirates kati ya Arsenal na Man City.
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumamosi Machi 29
15:45 Man United v Aston Villa
18:00 Crystal Palace v Chelsea
18:00 Southampton v Newcastle
18:00 Stoke v Hull
18:00 Swansea v Norwich
18:00 West Brom v Cardiff
20:30 Arsenal v Man Cit
Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, licha ya kukaririwa kukiri kwamba wao hawana nafasi ya kutwaa Ubingwa, ametamka kwamba bado lengo lao ni kuwa Mabingwa.
Amesema: “Hatuna kitu kingine zaidi ya kuwa Bingwa! Hiyo ndio azma yetu ya kwanza!”
Lakini Arsenal wanapambana na Man City ambayo iliwakung’uta Bao 6-3 Mwezi Desemba katika Mechi ya Ligi Uwanjani Etihad.
Wenger amesisitiza ni muhimu kwao kuonyesha nguvu Nyumbani kwao na hilo ndio litakalodhihirisha kama wana nafasi ya Ubingwa.
MSIMAMO:
NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Chelsea 31 21 6 4 62 23 39 69
2 Liverpool 31 21 5 5 84 39 45 68
3 Man City 29 21 3 5 79 27 52 66
4 Arsenal 31 19 6 6 54 35 19 63
5 Everton 30 16 9 5 46 30 16 57
6 Tottenham 31 17 5 9 40 40 0 56
7 Man United 31 15 6 10 48 37 11 51
8 Newcastle 31 14 4 13 38 43 -5 46
9 Southampton 31 12 9 10 45 40 5 45
10 Stoke 31 9 10 12 36 45 -9 37
11 West Ham 31 9 7 15 34 41 -7 34
12 Aston Villa 30 9 7 14 33 42 -9 34
13 Hull 31 9 6 16 33 39 -6 33
14 Norwich 31 8 8 15 26 48 -22 32
15 Swansea 31 7 9 15 41 47 -6 30
16 West Brom 30 5 13 12 33 45 -12 28
17 Crystal Palace 30 8 4 18 19 39 -20 28
18 Sunderland 29 6 7 16 27 45 -19 25
19 Cardiff 31 6 7 18 26 58 -32 25
20 Fulham 31 7 3 21 30 70 -40 24
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumapili Machi 30
1530 Fulham v Everton
1800 Liverpool v Tottenham
Jumatatu Machi 31
2200 Sunderland v West Ham