Wednesday, April 9, 2014

UCL:CHELSEA YAIPAPATUA PSG 2-0 YACHUPA NUSU FAINALI.

Matokeo Marudio.
Jumanne Aprili 8
aprilChelsea 2 Paris Saint-Germain 0 [3-3, Chelsea wamesonga kwa Bao la Ugenini]
Borussia Dortmund 2 Real Madrid 0 [2-3]
CHELSEA FC 2 PARIS SAINT-GERMAIN 0
-Stamford Bridge, London
Club ya Chelsea imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL baada ya Bao la Demba Ba la Dakika ya 87 kuwapa ushindi wa Bao 2-0 katika Mechi ya Marudiano iliyochezwa Stamford Bridge na kufanya Jumla ya Mabao kuwa Bao 3-3 katika Mechi mbili na wao kutinga hatua inayofuata ya Nusu fainali kwa  Bao la Ugenini.
Bao la Kwanza la Chelsea lilifungwa na Andre Schurrle, alieingizwa kumbadili Eden Hazard alieumia, katika Dakika ya 32.
Demba Ba ambae alitokea Benchi na Bao lake la ushindi kwa Chelsea lilimfanya Meneja wao Jose Mourinho ashangilie kwa aina ya kipekee.
VIKOSI:
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Luiz, Lampard, Willian, Oscar, Hazard, Eto'o.
Akiba: Schwarzer, Cole, Kalas, Mikel, Schurrle, Ba, Torres.
PSG: Sirigu, Jallet, Alex, Silva, Maxwell, Verratti, Motta, Matuidi, Lucas, Cavani, Lavezzi.
Akiba: Douchez, Marquinhos, Digne, Van der Wiel, Cabaye, Menez, Pastore.
REFA: Pedro Proença (Portugal) 

UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
Marudiano
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumatano Aprili 9
Bayern Munich v Manchester United [1-1]
Atletico Madrid v Barcelona [1-1]
DONDOO MUHIMU:
-DROO YA NUSU FAINALI: 11 Aprili
-Mechi kuchezwa 22 & 23 Aprili na Marudiano 29 & 30 Aprili
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
WASHINDI [Miaka ya karibu]:
MSIMU MSHINDI NCHI MSHINDI WA PILI NCHI GOLI
2012-13 Bayern Munich Germany Borussia Dortmund Germany 2-1
2011-12 Chelsea England Bayern Munich Germany 1-1 (4–3)
2010-11 Barcelona Spain Manchester United England 3-1
2009-10 Internazionale Italy Bayern Munich Germany 2-0
2008-09 Barcelona Spain Manchester United England 2-0
2007-08 Man United England Chelsea
England
1-1 (6–5)

Tuesday, April 8, 2014

VPL: AZAM VS RUVU SHOOTING MLANDIZI,YANGA VS KAGERA SUGAR U/TAIFA.

TIMU TATU FDL ZARUDI LIGI YA MKOA
Timu tatu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zitacheza Ligi ya Mkoa katika mikoa yao msimu ujao baada ya kushika nafasi za mwisho katika makundi yao, hivyo kushuka daraja.

Transit Camp imekata nafasi ya mwisho katika A wakati Mkamba Rangers imeshuka daraja kwa kukamata mkia katika kundi B. Nayo Pamba SC imerudi kucheza Ligi ya Mkoa wa Mwanza baada ya kuwa ya mwisho kwenye kundi C.
Timu zilizopanda daraja kutoka FDL kwenda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao ni Ndanda SC ya Mtwara kutoka kundi A, Polisi Morogoro ya kundi B na Stand United ya Shinyanga iliyoibuka kinara katika kundi C.

AZAM, YANGA KUTIMULIANA VUMBI VPL
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 9 mwaka huu) huku timu za Azam na Yanga ambazo zipo nafasi mbili za juu zikiendelea kuchuana.

Azam itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani. Nayo Yanga itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika Uwanja wa Taifa jijini.

Yanga, Azam, Ruvu Shooting na Kagera Sugar zote zimeshinda mechi zao za raundi ya 23 wakati mechi za kesho zitakuwa kwa ajili ya kukamilisha raundi ya 24 ya ligi hiyo ambayo inatarajia kukamilika Aprili 19 mwaka huu.

Ligi hiyo itaingia raundi ya 25 Aprili 12 na 13 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa viwanjani. Aprili 12 mwaka huu itakuwa Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting (Manungu, Morogoro), Coastal Union vs JKT Ruvu (Mkwakwani, Tanga), na Tanzania Prisons vs Rhino Rangers (Sokoine, Mbeya).

Aprili 13 mwaka huu ni Mgambo Shooting vs Kagera Sugar (Mkwakwani, Tanga), Simba vs Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mbeya City vs Azam (Sokoine, Mbeya) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).

TFF YAAFIKA UAMUZI WA KAMATI YA MAADILI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubaliana na uamuzi uliofanywa na Kamati ya Maadili katika malalamiko mawili ambayo iliyawasilisha mbele yake, hivyo haitakata rufani.

Katibu Mkuu wa TFF aliwasilisha mashauri mawili mbele ya Kamati hiyo iliyoongozwa na William Erio. Malalamiko ya kwanza yalikuwa dhidi ya waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Oden Mbaga na Samwel Mpenzu na wakufunzi wa waamuzi Riziki Majala na Mchungaji Army Sentimea.

Wote aliwalalamikia kwa kuwafanyisha mitihani (wakufunzi), na waamuzi kufanya mitihani hiyo kinyume na utaratibu pamoja na kughushi matokeo.

Kamati katika uamuzi wake iliiagiza waamuzi hao kufanya upya mtihani huo katika robo inayofuata ambapo wakifaulu waendelee kuchezesha mechi. Waamuzi wa FIFA hufanya mitihani hiyo mara nne kwa mwaka.

Kwa upande wa shauri dhidi ya Ofisa Takwimu wa TFF, Sabri Mtulla ambaye alilalamikiwa kwa kuidanganya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi dhidi ya mchezaji Emmanuel Okwi, Kamati iliagiza suala hilo liwasilishwe upya pamoja na ushahidi wa kuthibitisha malalamiko hayo.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Monday, April 7, 2014

NGORONGORO HEROES KUINGIA KAMBINI ALHAMISI

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngongoro Heroes) imereja nchini leo mchana (Aprili 7 mwaka huu) kutoka Kenya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya wenyewe, na itaingia kambini Alhamisi.
Ngorongoro Heroes ambayo imewasili saa 8.25 kwa ndege ya Kenya Airways ilitoka suluhu na Kenya katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kanyetta uliopo katika mji wa Machakos.
Kocha John Simkoko amesema benchi lake la ufundi linafanyika kazi upunguzi uliojitokeza ili wafanye vizuri kwenye mechi ya marudiano itakayochezwa Aprili 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Iwapo Ngorongoro Heroes itaitoa Kenya, raundi inayofuata itacheza na Afrika Kusini. Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 zitafanyika mwakani nchini Senegal.

TIMU YA WATOTO WA MITAANI YATWAA UBINGWA WA DUNIA-BRAZIL

STREET_CHILD-TANZANIA_BINGWA
Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada ya jana (Aprili 6 mwaka huu) kuilaza Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Mshambuliaji Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Fedh
a wa Uingereza, George Osborne.
STREET_CHILD
Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.
Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.
Timu ya Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.

NGORONGORO YA KAZA MBELE YA WAKENYA, DAKIKA 90 NGOMA 0-0

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye Fainali za Afrika mwakani nchini Senegal, baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Kenya Uwanja wa Kenyatta, Machakos nchini Kenya jana katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza. Ngorongoro sasa inahitaji hata ushindi wa 1-0 katika mchezo wa marudiano Dar es Salaam ili kusonga mbele. katika mchezo vijanawa Heroes wameonekana kabisa kuwa wana kiu ya kwenda senegal mwakani baaa ya kutandaza soka la nguvu lenye kuvutia mbele ya vijana wa kenya.

Sunday, April 6, 2014

MGAMBO YAIBAMIZA COASTAL UNION ,YANGA YAIPIGA 5-1 JKT RUVU


RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Aprili 6
Yanga 5 vs JKT Ruvu 1
Coastal Union 0 vs Mgambo JKT 2
JKT Oljoro 2 v Tanzania Prisons 1
Rhino Rangers 0 v Mtibwa Sugar 1
Jumatano Aprili 9
Ruvu Shooting v Azam FC
MABINGWA wa VPL-Ligi Kuu Vodacom, Yanga, Leo wameweka hai matumaini yao ya kutetea Ubingwa wao baada ya kuitandika Ruvu JKT Bao 5-1 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaa huku Straika wao, Mrisho Ngassa, akipiga Hetitriki.
Hadi Mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa Bao za Ngassa, Dakika ya 8 na 15, na Didier Kavumbagu, Dakika ya 38.
Kipindi cha Pili, Ngassa alipiga Bao jingine kwenye Dakika ya 49 na Javu kupiga Bao la 5 katika Dakika ya 52.
Bao pekee la Ruvu JKT lilifungwa na Iddi Mbaga katika Dakika 84.
Ushindi huu umeifanya Yanga iwe na Pointi 49 kwa Mechi 33 na wako Nafasi ya Pili huku Azam FC wakiendelea kuongoza Ligi wakiwa na Pointi 53 kwa Mechi 23.
Timu ya Tatu ni Mbeya City yenye Pointi 46 kwa Mechi 24.

Mgambo Shooting leo ikicheza katika mechi dhidi ya Coastal Union, imeibuka na ushindi wa mabao 2-0, hivyo kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu Bara.
Kabla ya hapo, Mgambo ilizitungua Yanga na Simba kwenye uwanja huo wa Mkwakwani.
 Mechi nyingine mjini Arusha, wenyeji JKT Oljoro wamewaonyesha Prisons ‘rigwaride’ baada ya kuwachapa mabao 2-

STREET CHILD WORLD CUP-RIO 2014: TANZANIA YATINGA FAINALI KUIVAA BURUNDI.

TIMU YA WATOTO WA MITAANI YATINGA FAINALI BRAZIL
Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetinga fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani baada ya kuichapa Marekani mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa jana (Aprili 5 mwaka huu) jijini Rio de Janeiro, Brazil.
STREET_CHILD
Hadi mapumziko Tanzania ilikuwa mbele kwa mabao 4-0. Bao pekee la Marekani katika mchezo huo ambayo hadi nusu fainali ilikuwa haijafungwa lilifungwa dakika za mwisho.
Kwa matokeo hayo, Tanzania inacheza Fainali na Burundi. Mechi hiyo inachezwa leo (Aprili STREET_CHILD-TANZANIA6 mwaka huu) ambapo Burundi imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika nusu fainali ya pili.
Mchezo huo wa fainali unachezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense katikati ya Jiji la Rio de Janeiro huku mgeni rasmi  akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne.
Katika mechi ya kwanza katika kundi B la michuano hiyo, Tanzania ilicheza na Burundi na kutoka sare ya mabao 2-2.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF