Wednesday, April 23, 2014

MTIBWA IPO MBIONI KUTOLEA MACHO WANANDINGA WAPYA

Timu ya soka ya Mtibwa Sugar Mabingwa wa zamani wa Tanzania kwa mwaka 1999 na 2000wamekiri kukumbana na changamoto kubwa msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu Tanzania bara uliomalizika aprili 19 mwaka huu .
 Afisha habari wa klabu hiyo, Tobias Kifaru Lugalambwike ameueleza mtandao huu kuwa kitu kikubwa walichojifunza ni maandalizi makubwa ya baaadhi ya timu zinazoshiriki ligi kuu toafuti na wao.
“Sisi ni wakongwe katika ligi hii, lakini tumeshindwa kuonesha cheche kutokana na kuwepo kwa timu zenye kiwango kizuri. Mbeya City fc wametikisa kweli, sio kwetu tu hata Simba na Yanga wamekumbana na upinzani na ndio maana wamekosa ubingwa ”.
“Kikubwa tumebaini changamoto zetu ikiwemo kukosa wachezaji muhimu kikosini. Tunataka kufanya usajili mzuri ili tuanze maandalizi ya mapema”.

BURUNDI KUTUA KESHO NCHINI KUIKABILI STARS

Timu ya Taifa ya Burundi (Intamba Mu Rugamba) inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Intamba Mu Rugamba it
Burundi-CECAFA-Teamakuwa na msafara wa watu 28 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, na itafikia hoteli ya Accomondia. Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10 jioni
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000. Mechi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

MALINZI AWAPA PONGEZI SUKER, LEKJAA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewapongeza marais Davor Suker na Fouzi Lekjaa kwa kuchaguliwa tena hivi karibuni kuongoza mashirikisho ya mpira wa miguu katika nchi zao.
Suker amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Croatia (CFF) wakati Lekjaa amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRFM).
Katika salamu zake za pongezi, Rais Malinzi amesema ushindi waliopata ni uthibitisho kuwa familia ya mpira wa miguu katika nchi zao ina imani kubwa kwao katika kuendeleza mchezo huo ndani na nje ya nchi hizo.
Rais Malinzi amesema Lekjaa na Suker wana uwezo wa kuendeleza kazi nzuri ambayo tayari imefanyika, lakini vilevile kuja na mawazo mapya ambayo yatakuwa changamoto kwa ustawi wa mchezo huo nchini Morocco na Croatia kwa ujumla.

Tuesday, April 22, 2014

JUMAMOSI TAIFA STARS NA BURUNDI KIINGILIO BUKU TANO

DSC_0178Katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba) itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kiingilio cha chini ni sh. 5,000.
Mechi hiyo itakuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa wa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari ipo kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka nchini Kenya.
Burundi inatarajia kuwasili nchini keshokutwa (Aprili 22 mwaka huu) tayari kwa ajili ya mechi hiyo inayotajiwa kuwa ya kusisimua. Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 10 jioni.

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/04/tff_LOGO12.jpg Wachezaji wa Taifa Stars waliopo kambini ni Deogratias Munishi, Mwadili Ali, Aidan Michael, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Hassan Mwasapili, Kelvin Yondani, Said Moradi, Amri Kiemba, Frank Domayo, Himid Mao, Jonas Mkude, Athanas Mdamu, Haruna Chanongo, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Ramadhan Singano na Simon Msuva.
Wengine ni Benedicto Mlekwa, Emma Simwanda, Joram Mgeveje, Omari Kindamba, Edward M
ayunga, Shiraz Sozigwa, Yusuf Mlipili, Said Ally, Abubakar Mohamed, Hashim Magona, Omari Nyenje, Chunga Zito, Mohammed Saidi, Ayoub Lipati, Abdurahman Ally na Paul Bundara
 BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Monday, April 21, 2014

VPL YAMALIZIKA IKIWA NA CHANGAMOTO ZAKE AZAM IKITWAA UBINGWA HUO.



MSIMU wa VPL Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara umefikia tamatu jumamosi ya aprili 19 mwaka huu kwa Azam FC kutawazwa kuwa mabingwa wapya baada ya kumaliza na pointi 62 dhidi ya 56 za waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya mechi zote 26.
 
Licha ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine Aprili 13, mwaka huu,


Azam FC pia inakuwa timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa Bara tangu mwaka 2000 Mtibwa Sugar ilipofanya hivyo
Azam inakuwa timu ya saba nje ya Si


mba SC kutwaa taji la Ligi Kuu, baada ya Cosmo mwaka 1967, Mseto mwaka 1975, Pan Africans mwaka 1982, Tukuyu Stars mwaka 1986, Coastal Union 1988 na Mtibwa Sugar mara mbili mfululizo 1999 na 2000.

Ashanti United ya Ilala, Dar es Salaam inayomaliza ligi na pointi 25, inaungana na JKT Oljoro ya Arusha iliyomaliza na pointi 19 na Rhino Rangers ya Tabora pointi 16 kuipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu msimu wa 2013/2014 na nafasi zao kuchukuliwa na Ndanda FC ya Mtwara, Polisi ya Morogoro na Stand United ya Shinyanga zilizopanda kwa ajili ya msimu ujao. 

Mbali na Azam kumaliza kileleni na pointi 62, Yanga SC pointi 56 nafasi ya pili, Mbeya City ya Mbeya imemaliza nafasi ya tatu kwa pointi zake 49, Simba SC ya nne pointi 38, Kagera Sugar ya tano pointi 38 pia, Ruvu Shooting ya sita pointi 38, Mtibwa Sugar ya saba pointi 31, JKT Ruvu ya nane pointi 31 Coastal Union ya tisa pointi 29, Prisons ya 10 pointi  28 na JKT Mgambo ya 11 pointi 26. 
Huku tunahitimisha pazia la Ligi Kuu pamoja na kufurahia kufika salama, lakini ukweli ni kwamba kuna mapungufu mengi yaliyojitokeza ndani ya msimu huu ambayo yangeweza hata kusababisha athari kubwa.

Miongoni mwa hayo ni suala la uchezeshaji wa marefa, mfumo na muundo mzima wa ligi yetu ikiwa ni pamoja na kanuni kutozingatiwa, au kuwa na kanuni ambazo hazikidhi vigezo vya kimataifa.

Kanuni ya tano ya Ligi Kuu inasema kifungu cha (1) Uwanja wa nyumbani ni ule ul
iochaguliwa na timu husika na Uwanja wa ugenini ni ule ambao timu pinzani imekaribishwa kucheza.
Kifungu cha (2) Kutokana sababu za kiusalama au Uwanja, kutofikika au sababu nyingine yeyote ya msingi, TFF kwa kushauriana na timu husika, endapo timu yoyote haina Uwanja wa nyumbani unaofaa kwa mashindano ya Ligi, timu husika inaweza kuchagua kwa idhini ya TFF, Uwanja mwingine wowote, hata nje ya mji huo au Mkoa ili mradi Uwanja huo uwe jirani na mkoa wa timu husika ndani ya Tanzania Bara na uwe na sifa zinazokubalika,”.


Kuna tatizo katika kanuni hii, ukipitia kanuni nyingine nyingi duniani, zinaweka wazi kwamba timu itakuwa na Uwanja mmoja tu wa nyumbani, lakini kanuni hii ya ligi yetu imefumbwa na matokeo yake timu kama Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar Azam FC na Prisons msimu huu zimetumia Uwanja zaidi ya mmoja wa nyumbani.
Ruvu, Mtibwa na Azam zimeruhusiwa kutumia viwanja vyao kwa mechi zote za Ligi Kuu isipokuwa zile zinazohusu Simba na Yanga, kwa sababu timu zote za Kariakoo, Dar es Salaam zina mashabiki wengi.   

WANACHAMA WA CLUB YA COASTAL UNION WATOA NENO KUHUSU UONGOZI WAO.


Coastal union  ambayo imemaliza Ligi Kuu Bara ikishika nafasi ya tisa na alama 29 ambapo ilikuwa sio matarajio ya wanachama wa club hiyo nao wametoa neno.
Wanachama ambao wa club hiyo kutoka jiji la Tanga walitoa ujumbe kwa uongozi wao wakionyesha kupinga mambo kadhaa yanayoonekana kutokwenda sawa.
Lakini kilichoonyesha kweli mambo hayo hayako vizuri ni wachezaji kwenda kuwaunga mkono wanachama hao mara baada ya mechi hiyo kwisha.
Uongozi wa Coastal Union, umekuwa ukishutumiwa kukataa kutoa kadi mpya za wachama, huku Kassim El Siagi ambaye ni katibu mkuu akielezwa kuwa chanzo.
Siagi amekuwa akisisitiza kwamba lazima kabla ya kuwakubali wanachama wapya, basi wawahakiki kwanza kwa kuwajadili.
Lakini katiba ya Coastal Union haina kipengele hicho.