
Timu hiyo yenye msafara wa watu 37
ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku
(Julai 15 mwaka huu) na imefikia hoteli ya Sapphire. Amajimbos itafanya
mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo
kutoka Shelisheli wakiongozwa na Allister Barra tayari wamewasili
nchini. Kamishna wa mechi hiyo ni Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy
kutoka Madagascar.
Makocha wa timu za Seregenti Boys
na Amajimbos pamoja na manahodha wao watakuwa na mkutano na waandishi wa
habari kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000. Tiketi zitauzwa uwanjani katika magari maalumu siku ya mechi.
SAMATA, ULIMWENGU WATUA, MWINYI KAZIMOTO KESHO
Washambuliaji Mbwana Samata na
Thomas Ulimwengu wamewasili nchini leo asubuhi (Julai 16 mwaka huu)
kutoka Tunisia kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya
Msumbiji itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao wamefikia hoteli ya
Courtyard, Seaview Upanga na leo (Julai 16 mwaka huu) watafanya mazoezi
kwa programu maalumu waliyopewa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij
wakati wakiwasubiri wenzao.

Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itawasili Dar es Salaam kesho (Julai 17 mwaka
huu) saa 3.20 asubuhi kwa ndege ya Fastjet kutoka Mbeya tayari kwa
maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Msumbiji.
RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa
habari Ijumaa (Julai 18 mwaka huu).