Friday, December 5, 2014

MTIBWA SUGAR YASEMA MAZUNGUMZO NA HASANI KESSI YANAKWENDA VIZURI.

Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba upo katika hatua za mwisho za kumalizana na Simba kwa ajili wa beki  wao namba mbili Hassani Ramadhani Kessy licha ya kuripotiwa kuwepo  na ugumu wa mchakato huo wa usajili.
Hata hivyo kumekuwa na taarifa kwamba mazungumzo yako katika hatua nzuri sana na pande zote mbili, yaani Simba na Mtibwa Sugar zimekubali kwamba zimefanya mazungumzo.
Afisa Habari wa Mtibwa Sugar Tobias Kifaru ameweka wazi kuwa Simba wameonyesha nia ya kumtaka mchezajihuyo ambapo mazungumzo yanaendelea vizuri na kila kitu kinakwenda vizuri katika uwezekano wa kumsajili kukamilika ndani ya siku chache zijazo.

TFF YASEMA WACHEZAJI WATAKAO CHEZA NANI MTANI JEMBE LAZIMA WAWE WAMESAJILI RASMI

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza wachezaji watakaotumika katika mechi ya Bonanza ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba dhidi ya Yanga lazima wawe wale waliosajiliwa kwa mujibu wa kanuni.
Yanga au Simba hazitaruhusiwa kumtumia mchezaji yoyote ambaye hayuko kwenye usajili wakati wa mechi hiyo ya Oktoba 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Maana yake, Simba haitaweza kumtumia kiungo wake Mgambia, Omar Mboob hadi hapo itakapomsajili.
Kama itamsajili, itawakosa mmoja kati ya Amissi Tambwe au Pierre Kwizera ambao italazimika kuwatema.
Hadi sasa inaonekana Simba bado inamjaribu, hivyo haitakuwa rahisi kupata uhakika wa kumsajili hadi Desemba.
Hata hivyo, Mboob atapata nafasi nyingine ya kuonyesha uwezo wake, kesho kwenye Uwanja wa Taifa wakati Simba itakapoivaa Express ya Uganda.

MLINZI WA ZAMANI WA SIMBA NA COAST UNION JUM NYOSSO AJIUNGA MBEYA CIT MKATABA WA MWAKA MMOJA

Mlinzi wa kati Juma Nyosso amejiunga na kikosi cha Mbeya City Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja.


Akizungumza mara baada ya kuisaini mkataba  huo kwenye  ofisi za timu zilizopo jengo la Mkapa Hall jijini Mbeya,  Nyoso aliyewahi kucheza kwenye timu za Ashanti United, Simba na Coastal Union, alisema  amekubari kujiunga na City kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa imani kuwa utatosha  kuushawishi uongozi wa timu kumpa mkataba mrefu zaidi mara baada ya huu wa sasa.
“City ni timu nzuri na imekuwa hivyo toka ilipoanzishwa miaka minne iliyopita, matokeo yaliyoo sasa ni sehemu ya soka ambayo timu yoyote inaweza kuyapata, nimekubari kujiunga na timu kwa  mkataba wa mwaka mmoja kwa sababu naamini uwezo wangu  uwanjani utawashawishi viongozi kunipa mkataba mrefu zaidi  pindi huu utakapo malizika na nina amini  hili linawezekana kwa sababu nataka kukaa kwenye timu hii mpaka mpira wangu utakapoisha” alisema Nyosso
Akiendelea zaidi beki huyo aliyewahi pia kucheza  kwenye kikosi cha timu ya Taifa  ‘Taifa Stars’ alisema kuwa  mafanikio iliyopata Mbeya City msimu uliopita yamekuwa sababu kubwa ya yeye kukubari kujiunga na City huku akiamini kuwa amekuja kuongeza nguvu kwenye timu bora ili kuhakikisha mafanikio ya msimu uliopita yanafanikiwa tena.
DSC_0027
K wa upande wake Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe alimshukuru Nyosso kwa kukubari kujiunga na timu hii huku akiamini kuwa uzoefu alionao mchezaji huyo utasaidia kuimarisha safu ya ulinzi kwenye kikosi cha City.
“Tunamshukuru kukubari kujiunga nasi, imani yetu kubwa kwamba uzoefu alionao utasaidia kuimarisha safu yetu ya ulinzi, hasa ukizingatia matokeo tuliyopata katika michezo saba ya mwanzo wa Ligi hii” alisema Kimbe huku   kauli yake hiyo ikiungwa mkono na Kocha Mkuu Juma Mwambusi.
Kwa sasa Nyosso tayari yuko na kikosi cha City kilichosafiri kwenda mjini Songea  kwa ajiri ya michezo ya kirafiki.

TAZAMA MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA KWA MECHI SABA.


MSIMAMO LIGI KUU TZ BARA

Standings

PWDLFAGDPts
1mtibwa_sugarMtibwa Sugar FC7430103715
2Azam_FC_Club_LogoAzam FC741284413
3young_africansYoung Africans SC741296313
4COASTAL UNIONCoastal Union732397211
5KAGERA_SUGAR_FCKagera Sugar FC724164210
6JKT RUVU STARSJKT Ruvu Stars731367-110
7simbaSimba SC71607619
8polisi_morogoroPolisi Morogoro723267-19
9jkt_mgamboMgambo Shooting730357-29
10tffStand United FC723259-49
11JKT RUVU STARSRuvu Shooting FC721447-37
12Tanzania Prisons logoTanzania Prisons713367-16
13ndanda_fcNdanda FC7205812-46
14Mbeya FC LogoMbeya City FC712426-45

Thursday, December 4, 2014

MECHI YA NANI MTANI JEMBE KUCHEZWA TAREHE 13 DISEMBA

Mechi ya Nani Mtani Jembe 2 kati ya Simba na Yanga zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi, Disemba 13, 2014 saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meneja Udhamini wa TBL, George Kavishe amesema kwamba “Tayari Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe 2 (Nani Mtani Jembe 2 Match).
 Pambano hili ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia saini makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Kavishe aliongeza kuwa mechi hii ni maalumu kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 ambayo imeendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Alisema Nani Mtani Jembe 2 inahusisha mashabiki wa klabu za Simba na Yanga ambapo zawadi ya shilingi milioni 100 itatolewa na kugawanywa ifuatavyo.
  • Shilingi Milioni 20 ni zawadi ya mechi ya Nani Mtani Jembe ambapo timu itakayoshinda itapata sh milioni 15 na timu itakayofungwa itapata shilingi milioni 5.
  • Kampeni hii inaendeshwa kwa njia ya sms ambapo mashabiki wanapiga kura kwa njia ya sms na shilingi milioni 80 zimegawanywa kati ya timu hizo mbili ambapo kila timu ilianza na shillingi milioni 40 kwenye benki maalumu mtandaoni.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alisema mashabiki wa Simba na Yanga wanaweza kushiriki kwa kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager yenye ujazo wa mililita 500 ambapo mteja atabandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager na kuona namba maalumu. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo ambayo anatuma kwenda namba 15415 na kwa kufanya hivyo anakuwa amepunguza pesa taslimu shilingi 10,000 kutoka timu pinzani na kuichangia timu yake.
Kikuli pia alizikabidhi timu hizo jezi maalumu itakayovaliwa mahususi kwa ajili ya mechi hiyo na kuwahimiza mashabiki waendelee kuzipigia kura timu zao na kikubwa kuhakikisha wanafika uwanja wa taifa na kujionea wenyewe pambano hilo ambalo lazima mshindi apatikane.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura aliwakaribisha mashabiki na kuwaomba wajitokeze kwa wingi kwani hivi sasa timu hizo ziko kambini zikijiandaa na mtanage huo wa kukata na shoka unaotarajiwa kuwa na msisimko mkubwa.
Alitaja viingilio vya mechi hiyo kuwa ni shilingi 30,000 kwa VIP B, 20,000/= VIP C, 15,000/= kwa viti vya rangi ya chungwa kiingilio kitakuwa ni sh 15,000 huku viti vya bluu na kijani tiketi zikiuzwa kwa sh. 7,000/=.
Wambura alisema pambano hilo litakalosimamiwa na TFF litaanza saa kumi kamili na litachezwa kwa dakika 90 tu ambapo kama muda huo timu hizo hazitafungana basi mikwaju ya penati itapigwa ili mshindi apatikane.
Taji la Nani Mtani Jembe linashikiliwa na Simba ambao waliwafunga mahasimu wao 3-1 katika mechi iliyochezwa Disemba 21, 2013.

Tuesday, December 2, 2014

MANDAWA MCHEZAJI BORA WA VPL NOVEMBA

Mshambuliaji wa timu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa mwezi Novemba mwaka huu ambapo atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja.
Mandawa ambaye kwa mwezi huo alichuana kwa karibu na mshambuliaji Fulgence Maganda wa Mgambo Shooting ya Tanga na nahodha wa Simba, Joseph Owino atakabidhiwa zawadi yake na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom.

Hafla ya kukabidhi zawadi hiyo inatarajiwa kufanyika wakati wa mechi ya raundi ya nane ya ligi hiyo kati ya Simba na Kagera Sugar itakayochezwa Desemba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
KOZI YA UKUFUNZI WA UTAWALA YA FIFA SASA MACHI.
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limesogeza mbele kozi ya ukufunzi ya utawala wa mpira wa miguu iliyokuwa ifanyika Desemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa FIFA, kozi hiyo sasa itafanyika Machi mwakani katika tarehe itakayotangazwa baadaye.

TFF imepokea maombi ya zaidi ya washiriki 40 kwa ajili ya kozi hiyo itakayoshirikisha washiriki 30. Kutokana na maombi kuzidi idadi ya nafasi zilizopo, FIFA itafanya mchujo wa washiriki.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MIKOA MITANO YATAKIWA KUWASILISHA USAJILI COPA 2014

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitaka mikoa mitano kuwasilisha usajili wa wachezaji wake kwa ajili ya mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola 2014 kabla ya Desemba 5 mwaka huu.

Mikoa hiyo ambayo haijawasilisha usajili wake hadi sasa kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza Desemba 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni Arusha, Dodoma, Katavi, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Mjini Magharibi na Simiyu.

Kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya michuano hiyo, mkoa ambao hautawasilisha usajili wake kwa ajili ya uhakiki wa umri wa wachezaji utakaonza Desemba 10 mwaka huu utaondolewa katika fainali hizo zitakazomalizika Desemba 20 mwaka huu.

Wachezaji watakaobainika kuzidi umri hawataruhusiwa kushiriki katika michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 15. Kwa mujibu wa Kanuni ya 29 ya michuano kuhusu idadi ya wachezaji, kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji wasiozidi 20 na wasiopungua 16.

Hivyo, kila timu inatakiwa kuhakikisha inakuwa na idadi hiyo ya wachezaji, kwani kikanuni wakipungua 16 itaondolewa kwenye mashindano.

Timu 16 kwa upande wa wavulana zitashiriki katika fainali hizo wakati kwa upande wa wasichana ni timu nane. Mikoa iliyoingiza timu za wasichana kwenye fainali hizo ni Arusha, Dodoma, Ilala, Kinondoni, Mbeya, Mwanza, Temeke na Zanzibar.