Klabu ya soka ya Yanga, ya Jijini Dar es Salaam leo jioni itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya
Soka ya The Express Kutoka nchini Uganda, mchezo utakaochezwa majira ya saa 10
jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika dimba la Uwanja Taifa Jijini Dar es
salaam.
Yanga itapambana na The Express kama sehemu ya mchezo wa maandalizi ya
kujipima nguvu kuelekea pambano la mtani jembe siku ya jumamosi tarehe
13/12/20014 dhidi ya timu ya Simba SC jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa kesho kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo
anatarajiwa kukitumia kikosi chake chote kwa lengo la kutazama maendeleo ya
vijana wake kabla ya mchezo wa Nani Mtani Jembe wiki ijayo.
Mpaka sasa klabu ya Young Africans imefanya usajili wa mchezaji mmoja tu
Emerson De Oliveira kutoka nchini Brazil ambaye anachukua nafasi ya
mshambuliaji Geilson Santana "Jaja" ambaye ameomba kuachwa kutokana
na kushindwa kurejea nchini kwa masuala ya kifamilia.
Wananchama, mashabiki na wapenzi wa Yanga kutoka matawi mbalimbali
wanaombwa kuhudhuriwa kwa wingi uwanjani, ili kutoa hamasa ya ushindi kwa
wachezaji siku ya jumamosi katika uwanja mkuu wa taifa, jijini Dar es salaam.
Yanga inashiriki ligi kuu ya Tanzania bara ikiwa inashika nafasi ya pili
sawa na Azam FC kwa kulingana pointi na magoli ya kufunga na kufunga,
inajaindaa pia na mzunguko wa nane wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya
kimataifa kombe la Shirkisho baranai Afrika mapema mwakani.