DANY LYANGA AIPA YANGA UBINGWA LEO NA KULETA SHANGWE JANGWANI"
Katika mechi ya ligi kuu iliochezwa leo katika dimba la uwanja wa mkwakwani jijini tanga kati ya wawakilishi wa tanzania waliobaki katika michuano ya kombe la shirikisho barani africa azam fc wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wagosi wa kaya coastal union katika mchezo uliokuwa na upinzani wa hali ya juu.
Katika mchezo huo azam fc ndio wa kwanza kupata bao kupitia waliokuwa wa klililowekwa kimiani na beki Aggrey Morris kwa njia ya mkwaju wa penalti dakika ya 60, baada ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Gaudence Mwaikimba kuchezewa rafu katika eneo la hatari na beki Yussuf Chuma na refa Andrew Shamba wa Pwani kuamuru penalti.
Kwa upande wa coastal union lilipata bao kunako dakika ya 72 mshambuliaji wao hatari dany lyanga aliechukuwa nafasi ya mzenji suileman kassim selembe nakupelea kuleta furaha za ubingwa kwa wanajangwani dar es salaam yanga afrika.
Kwa Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Azam FC waliokuwa washindani wakuu wa Yanga SC yenye pointi 56, kamwe hawawezi kufikisha pointi hizo ambazo wanazo mabingwa hao wapya, kwani hata wakishinda mechi zao nyingine mbili zilizobaki, watamaliza na pointi 54.
MECHI ZILIZOBAKI KWA VIGOGO
AZAM FC:
Mei 11, 2013; Vs Mgambo JKT (Chamazi)
Mei 18, 2013; Vs JKT Oljoro (Arusha)
P W D L GF GA GD Pts
2 Azam FC 24 14 5 4 41 19 22 48
SIMBA SC:
Aprili 28, 2013; Vs Polisi Moro (Taifa)
Mei 5, 2013; Vs Ruvu Shooting (Taifa)
Mei 8, 2013; Vs Mgambo JKT (Taifa)
Mei 18, 2013; Vs Yanga SC (Taifa)
P W D L GF GA GD Pts
4 Simba SC 22 9 9 4 32 21 11 36
YANGA SC:
Mei 1, 2013; Vs Coastal Union (Taifa)
Mei 18, 2013; Vs Simba SC (Taifa)
P W D L GF GA GD Pts
1 Yanga SC 24 17 5 2 44 13 31 56
MSIMAMO VPL
3 Kagera Sugar 23 11 7 5 25 18 7 40
4 Simba SC 22 9 9 4 32 21 11 36
5 Mtibwa Sugar 24 9 9 6 27 23 4 36
6 Coastal Union 24 8 10 6 24 21 3 34
7 Ruvu Shooting 22 8 6 8 21 21 0 30
8 JKT Oljoro 24 7 7 10 22 27 -5 28
9 Prisons 24 6 8 10 14 21 -7 26
10 JKT Ruvu 24 7 5 12 20 37 -17 26
11 Mgambo JKT 23 7 4 12 16 23 -7 25
12 Toto African 25 4 10 11 22 34 -12 22
13 Polisi Moro 23 3 10 10 12 22 -10 19
14 African Lyon 24 5 4 15 16 36 -20 19
ORODHA TIMU ZILIZOTWAA UBINGWA WA LIGI KUU:
1965 : Sunderland (simba)
1966 : Sunderland (simba)
1967 : Cosmopolitans (Dar es Salaam)
1968 : Yanga
1969 : Yanga
1970 : Yanga
1971 : Yanga
1972 : Yanga
1973 : Simba
1974 : Yanga
1975 : Mseto SC (Morogoro)
1976 : Simba
1977 : Simba
1978 : Simba
1979 : Simba
1980 : Simba
1981 : Yanga
1982 : Pan African
1983 : Yanga
1984 : Simba
1985 : Yanga
1986 : Tukuyu Stars (Mbeya)
1987 : Yanga
1988 : Coastal Union (Dar es Salaam)
1989 : Yanga
1990 : Simba
1991 : Yanga
1992 : Yanga
1993 : Yanga
1994 : Simba
1995 : Simba
1996 : Yanga
1997 : Yanga
1998 : Yanga
1999 : Mtibwa Sugar (Morogoro)
2000 : Mtibwa Sugar (Morogoro)
2001 : Simba
2002 : Yanga
2003 : Simba
2004 : Simba
2005 : Yanga
2006 : Yanga
2007 : Simba (Ligi Ndogo)
2008 : Yanga
2009: Yanga
2010: Simba SC
2011: Yanga SC
2012: Simba SC
2013: Yanga SC