Thursday, May 16, 2013

KIM ATAJA 26 STARS WA KUIVAA MOROCCO MJINI MARRAKECH.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.

Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.

Wapya aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud Cholo na Issa Rashid.

Kikosi kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;

Makipa ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Mudathiri Yahya (Azam) na Salum Abubakar (Azam).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Juma Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Zahoro Pazi (JKT Ruvu).

Kocha Kim amesema kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na wachezaji 24 ambapo Samata na Ulimwengu watajiunga na timu jijini Marrakech, lakini wachezaji atakaondoka nao Dar es Salaam kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo ataacha kipa mmoja na mchezaji mmoja wa ndani.

Awali TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu dhidi ya Algeria, Libya au Misri. Lakini baadaye Algeria ikasema itacheza na Togo, wakati Misri ilitaka mechi hiyo ichezwe Juni 4 jijini Cairo, jambo ambalo lisingewezekana kwa Stars kwani ina mechi ya mashindano Juni 8 mwaka huu.

Kwa upande wa Libya mechi hiyo ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni 2 mwaka huu. Lakini baadaye Libya ikataka mechi hiyo ichezewe jijini Tripoli ambapo TFF ilikataa kutokana na sababu za kiusalama.

TANZANIA YAJIONDOA MICHUANO YA COSAFA
Tanzania (Taifa Stars) imejitoa kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) itakayofanyika nchini Zambia kuanzia Julai 2-26 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah amesema Stars ambayo iliingizwa katika michuano hiyo kama timu mwalikwa imejitoa kutokana na mwingiliano wa ratiba kati ya michuano hiyo na mechi za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Amesema awali Tanzania ilithibitisha kushiriki michuano kwa matarajio kwamba Uganda ingekubali ombi la TFF la kubadilisha ratiba ya mechi za CHAN, lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) likagoma kwa vile kipindi ambacho kilipendekezwa lenyewe litakuwa na uchaguzi wa viongozi wao.

Taifa Stars itacheza na Uganda (The Cranes) katika mechi za CHAN ambapo mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu wakati ya marudiano itafanyika jijini Kampala kati ya Julai 26-28 mwaka huu.

Akizungumzia michuano ya COSAFA, Kocha Kim amesema angependa kushiriki michuano hiyo kwani ingekuwa kipimo kizuri kwa kikosi chake, lakini kwa sasa malengo makubwa ya Stars kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambayo fainali zake zitafanyika mwaka 2015.

TIKETI SIMBA, YANGA KUANZA KUUZWA KESHO
Tiketi kwa ajili ya pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Yanga litakalochezwa keshokutwa (Jumamosi) kwenye Uwanja wa Taifa zitaanza kuuzwa kesho (Ijumaa) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Vituo vitakavyouza tiketi hizo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni ni Uwanja wa Taifa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, OilCom Ubungo, kituo cha mafuta Buguruni, BMM Barbershop Sinza Madukani, Dar Live Mbagala na Sokoni Kariakoo.

Tiketi hizo zitakuwa zikiuzwa katika magari maalumu yaliyoegeshwa katika vituo hivyo. Viingilio katika mechi hiyo ya kufunga msimu ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani, sh. 7,000 viti vya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B n ash. 30,000 kwa VIP A.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Wednesday, May 15, 2013

MFAHAMU KWA UNDANI ZAIDI NEYMAR KATIKA HARAKATI ZA SOKA

                             NEYMAR
Neymar celebrating (cropped).jpg

Taarifa kuhusu yeye
Full nameNeymar da Silva Santos Júnior
Date of birth5 February 1992 (age 21)
Place of birthMogi das CruzesBrazil
Height1.74 m (5 ft 9 in)[1]
Playing positionForward

Timu ya sasa
Current clubSantos
Number11

Timu za ujana
1999–2003Portuguesa Santista
2003–2009Santos

Timu ya wakubwa
mwakaTimumechigoli
2009–Santos102(54)
Timu ya taifa
2009Brazil U173(1)
2011Brazil U207(9)
2012Brazil U237(4)
2010–Brazil32(20)

MATAJI NA CLUB KLABU HIZI

SANTOS
Campeonato Paulista (3): 2010, 2011, 2012
Copa kufanya Brasil (1): 2010
Copa Libertadores (1): 2011
Recopa Sudamericana (1): 2012
timu ya taifa ya
  
TIMU YA TAIFA BRAZIL
Amerika ya Kusini Vijana michuano ya (1): 2011
Superclásico de las Amerika (2): 2011, 2012
Olimpiki Silver Medali (1): 2012


TUZO BINAFSI.
Best Young Mchezaji wa Campeonato Paulista (1): 2009
Bora Mbele ya Campeonato Paulista (3): 2010, 2011, 2012
Bora Mbele ya Campeonato Brasileiro Serie A (3): 2010, 2011, 2012
Mchezaji bora wa Campeonato Paulista (3): 2010, 2011, 2012
Mchezaji bora wa michuano ya Vijana ya Amerika ya Kusini (1): 2011
Mchezaji bora wa Copa Libertadores (1): 2011
Mchezaji bora wa Campeonato Brasileiro Serie A (1): 2011
Mchezaji bora wa Recopa Sudamericana (1): 2012
Vijana Mchezaji wa Mwaka (1): 2011
Campeonato Brasileiro Serie kikosi michuano ya (3): 2010, 2011, 2012
Copa Libertadores michuano Squad (1): 2012
tuzo ya Arthur Friedenreich (2): 2010, 2012
Armando Nogueira nyara (2): 2011, 2012
mchezaji  bora katika Ligi ya Brazil na gazeti Placar mpira wa  Dhahabu (1): 2011 -
Mpira wa Fedha (2): 2010, 2011 - Best Mbele katika Ligi ya Brazil na gazeti Placar
Fedha mpira hors Concours (1): 2012
Kiatu cha Dhahabu {2): 2010, 2011, 2012 - Wengi malengo katika kila ushindani katika Brazil
Copa Brasil mfungaji  bora (1): 2010
Amerika ya Kusini Vijana michuano mfungaji  bora(1): 2011
FIFA Kombe la Dunia Bronze mpira (1): 2011
Amerika ya Kusini Mchezaji wa Mwaka (2): 2011, 2012
FIFA Puskás tuzo (1): 2011
Campeonato Paulista  mfungaji bora (1): 2012
Copa Libertadores mfungaji bora (1): 2012

CHELSEA VS ARSEANAL ENDAPO MAMBO YATAKUWA SIYO

Kamati ya BPL, ligi kuu uingereza imethibitisha kuwa yawezekana
ikawepo Mechi ya Mchujo yakupata Mshindi wa 3 endapo Chelsea na 
Arsenal zitamaliza Msimu hapo Jumapili zikiwa zimelingana kila kitu.

Hivyo ikitokea  jumapili Chelsea na everton zikitoka sare ya bila 
kufungana 0-0 na arsenal kuifunga Newcastle United 2-1 timu hizo 
zitakuwa sawa kwa pointi na tofauti ya magoli ya kufunga na
kufungwa Sababu kubwa ya kuwepo kwa mtange huo wa mchujo 
kupata msindi wa tatu wa
BPL ambapo timu tatu za juu zitacheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI"

MSIMAMO: BPL FAHAMU MAN U TAYARI NI BINGWA" 4 KUCHEZA UEFA.
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Man Utd
37
43
88
2
Man City
37
33
78
3
Chelsea
37
35
72
4
Arsenal
37
34
70
5
Tottenham
37
19
69
6
Everton
37
16
63
7
Liverpool
37
27
58
8
West Brom
37
-4
48
9
Swansea
37
-1
46
10
West Ham
37
-10
43
11
Stoke
37
-11
41
12
Norwich
37
-18
41
13
Newcastle
37
-22
41
14
Southampton
37
-11
40
15
Fulham
37
-13
40
16
Aston Villa
37
-22
40

17
Sunderland

37

-12

39
18
Wigan
37
-26
35
19
Reading
37
-28
28
20
QPR
37
-29
25
Matokeo yafuatayo ndio yatafanya Chelsea na Arsenal zimalize 
Msimu zikiwa sawa kwa kila kitu:
Chelsea 0-0; Arsenal washindi 2-1
Chelsea 1-1; Arsenal washindi 3-2
Chelsea 2-2; Arsenal washindi 4-3
Chelsea 3-3; Arsenal washindi 5-4
Wasimamizi hao wa BPL wamefafanua kuwa Mechi hiyo ya Mchujo itachezwa
kwenye Uwanja ambao si Stamford Bridge wala Emirates kwenye Tarehe
ambayo itapangwa.


TIMU ZA ULAYA:
UCL:
-Man United
-Man City
-2 kati ya Chelsea, Tottenham & Arsenal
Timu 3 za Juu BPL huanza Makundi na 
Timu iliyo nafasi ya 4 huanzia Raundi ya Mchujo.
EUROPA LIGI:
*Swansea City
*Wigan  athletic
Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye BPL
Huenda ikaongezeka 1 nyingine ikiwa England itakuwemo 3 Bora ya UEFA
Respect Fair Play League.
BPL: RATIBA-MECHI ZA MWISHO MSIMU HUU
Jumapili 19 Mei
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Everton
Liverpool v QPR
Man City v Norwich
Newcastle v Arsenal
Southampton v Stoke
Swansea v Fulham
Tottenham v Sunderland
West Brom v Man United
West Ham v Reading
Wigan v Aston Villa

SCOLARI AMUWEKEA KIFUA NEYMAR KUFUTIA TUHUMA ZA KUSHUKA KIWANGO.

KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Luis Felipe Scolari amuwekea kifua Neymar kufuatia tuhuma za mshambuliaji huyo kushuka kiwango katika klabu klabu yake kwa miezi ya karibuni. Nyota huyo anayekipiga katika klabu ya Santos ni miongoni mwa wachezaji walioitwa katika kikosi kitakachoshiriki Kombe la Shirikisho mwezi ujao na kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 amedai kuwa kiwango chake ndicho kilichopelekea kumuita katika kikosi chake. Scolari amesema Neymar amekuwa akicheza vyema katika ngazi ya klabu ingawa wengi hawatakubaliana name kwenye hilo lakini kwa maono yetu ya kiufundi hatuoni tatizo lolote kuwa naye kwenye kikosi. Scolari pia alitetea uamuzi wake wa kuwaacha nyota wengine wakongwe kama Ronaldinho na Kaka akidai kuwa bado wana nafasi ya kuwemo katika kikosi katika siku zijazo kama wataimarisha viwango vyao kuliko ilivyo hivi sasa.

FRANK LAMPARD BADO NIPO NIPO SANA CHELSEA SAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA.

KIUNGO mkongwe wa timu ya taifa england na klabu ya Chelsea, Frank Lampard amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja utakaomuweka Stamford Bridge kwa msimu mmoja zaidi. Nyota huyo ambaye ana rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi Chelsea mustakabali wake umekuwa gumzo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita lakini sasa ameamua kubakia hapo kwa msimu mwingine. Lampard ambaye mkataba wake wa zamani ulikuwa umalizike mwishoni mwa msimu huu alikuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia katika Ligi Kuu nchini Marekani kwenye klabu ya Los Angeles Galaxy kabla Chelsea hawajampatia mkataba huo mpya wa miezi 12. Mashabiki wa soka wa Chelsea wamekuwa wakipeperusha mabango katka mechi za timu hiyo wakitaka nyota huyo aliyefunga mabao 203 na kuipita rekodi ya Bobby Tambling aendelee kuwepo hapo. Lampard anatarajiwa kuwa nahodha wa kikosi cha Chelsea ambacho kitajitupa uwanjani baadae kucheza na Benfica ya Ureno katika fainali ya michuano ya Europa League jijini Amsterdam.

    FRANK LAMPARD KATIKA KATIKA HARAKARI ZA SOKA DUNIANI

Jina :Frank Lampard
Urefu
1.83 m (6 ft 0 in)
Playing position
[Midfielder]
TIMU YA SASA
Current club
                       TIMU YA UKUBWA
Miaka
Timu
Apps
(Gls)
1994–2001
148
(24)
2001-
363
(125)
Timu ya Taifa ya Kandanda
1999
90
(23)

FIFA YAONYA MAOFISA WA JIJI LA SAO PAULO KUHUSU KUPOTEZA HAKI YA KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2014

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeonya maofisa wa jiji la Sao Paulo kwamba wanaweza kupoteza haki ya kuandaa baadhi ya mechi za Kombe la Dunia 2014 kwasababu ya kuchelewa kukamilika kwa uwanja. Tishio hilo limeleta hasira kwa wamiliki wa kiwanja cha Corinthians ambao wamedai kuwa FIFA wanaweza kuwanyima haki hiyo kama wakitaka lakini hawawezi kufanya kazi chini shinikizo. Katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke amesema shirikisho hilo haliwezi kukubali kitu chochote ambacho kitapelekea uwanja huo ambao utachezwa mechi sita ikiwemo ile ya ufunguzi, kushindwa kufikia tarehe ya mwisho waliyowekewa. Mafundi tayari wameonya kuwa uwanja huo hautarajiwa kuwa tayari mpaka mwishoni mwa Februari mwakani. Valcke amesema kuanzia sasa mpaka hapo tiketi zitakapoanza kuuzwa wana uwezo wa kubadilisha mechi hizo katika viwanja vingine vilivyo tayari, hivyo wanasubiri mpaka Agosti mosi ili kuangalia uwezekano wa kubadilisha viwanja.