Wednesday, May 15, 2013

FRANK LAMPARD BADO NIPO NIPO SANA CHELSEA SAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA.

KIUNGO mkongwe wa timu ya taifa england na klabu ya Chelsea, Frank Lampard amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja utakaomuweka Stamford Bridge kwa msimu mmoja zaidi. Nyota huyo ambaye ana rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi Chelsea mustakabali wake umekuwa gumzo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita lakini sasa ameamua kubakia hapo kwa msimu mwingine. Lampard ambaye mkataba wake wa zamani ulikuwa umalizike mwishoni mwa msimu huu alikuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia katika Ligi Kuu nchini Marekani kwenye klabu ya Los Angeles Galaxy kabla Chelsea hawajampatia mkataba huo mpya wa miezi 12. Mashabiki wa soka wa Chelsea wamekuwa wakipeperusha mabango katka mechi za timu hiyo wakitaka nyota huyo aliyefunga mabao 203 na kuipita rekodi ya Bobby Tambling aendelee kuwepo hapo. Lampard anatarajiwa kuwa nahodha wa kikosi cha Chelsea ambacho kitajitupa uwanjani baadae kucheza na Benfica ya Ureno katika fainali ya michuano ya Europa League jijini Amsterdam.

    FRANK LAMPARD KATIKA KATIKA HARAKARI ZA SOKA DUNIANI

Jina :Frank Lampard
Urefu
1.83 m (6 ft 0 in)
Playing position
[Midfielder]
TIMU YA SASA
Current club
                       TIMU YA UKUBWA
Miaka
Timu
Apps
(Gls)
1994–2001
148
(24)
2001-
363
(125)
Timu ya Taifa ya Kandanda
1999
90
(23)