Wednesday, May 15, 2013

FAINALI EUROPA LIGI- LEO JUMATANO CHELSEANI VS BENFICA DIMBANI


Katika mechi ya kukata na shoka kesho jumatano mei 15 ni fainali ya europa ligi  kati ya chelsea wakitinga katika jijini  la amsterdam huko uholanzi  kukipiga  benfica  ya ureno huku chelsea ikiwazakuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kabisa kuweza kutwaa ubingwa wa uefa championz ligi na europa ligi mfululizo.
endapo chelsea wataibuka na ushindi basi itakuwa klabu ya nne barani uaya kuweza kutwaa makombe yote makubwa wakifuatiwa na juventus ,afc ajax na fc bayen munich ambazo zimeshawahi kushinda kombe la washindi mwaka 1970-71 na 1997-98.
FAINALI:EUROPA LIGI 
REKODI KWA TIMU HIZI"
Benfica

1989/90 Klabu Bingwa Ulaya: Walifungwa 1-0 na  AC Milan
1987/88 Klabu Bingwa Ulaya: Walifungwa Penati 6-5 na PSV Eindhoven (Sare 0-0)
1982/83 UEFA Cup: Walifungwa Jumla Bao 2-1 kwa Mechi 2 na  RSC Anderlecht 
1967/68 Klabu Bingwa Ulaya: Walifungwa 4-1 na Manchester United
1964/65 Klabu Bingwa Ulaya: Walifungwa 1-0 na FC Internazionale Milano
1962/63 Klabu Bingwa Ulaya: Walifungwa 2-1 na AC Milan
1961/62 Klabu Bingwa Ulaya: Washindi 5-3 na Real Madrid CF
1960/61 Klabu Bingwa Ulaya: Washindi 3-2 na FC Barcelona
Chelsea:
2011/12 UEFA Champions League: Washindi Penati 4-3 na Bayern Münich (1-1)
2007/08 UEFA Champions League: Walifungwa 6-5 na Man United FC (Sare 1-1)
1997/98 Kombe la Washindi: Washindi 1-0 na VfB Stuttgart
1970/71 Kombe la Washindi: Washindi 2-1 na Real Madrid (sare 1-1)
Timu hizi mbili zote zimetinga Fainali hii baada ya kutolewa katika hatua za
 Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, na hatimaye kushiriki EUROPA LIG.
EUROPA LIGI-WAFUNGAJI BORA:
-8 Libor Koza [Lazio]
-7 Edinson Cavabi [Napoli]
-6 Oscar Cardozo [Benfica]
-6 Rodrigo Palacio [Inter Milan]
-5 Fernando Torres [Chelsea]
Chelsea na benfica zilikutana kwa mara ya kwanza kwenye Mashindano ya Klabu Barani Ulaya 
Mwaka jana kwenye Robo Fainali ya UCL na Chelsea, chini ya Meneja Roberto Di Matteo,
iliifunga Benfica nje ndani, 1-0 huko Lisbon na 2-1 Stamford Bridge, wakiwa njiani kulitwaa Kombe hilo.
Kwa Benfica, hii itakuwa Fainali yao ya 9 Barani Ulaya na kwa Chelsea ni ya 5 lakini Chelsea wameshinda Fainali hizo 3 na Benfica 2 huku Benfica wakiwa wapo kwenye wimbi la kufungwa katika Fainali 6 tangu washinde ile ya Klabu Bingwa Ulaya Mwaka 1962 ila hii ni Fainali yao ya kwanza baada ya Miaka 23.
DONDOO ZA MAKOCHA WOTE WAWILI.


-Akiwa Liverpool, Rafael Benitez wa Chelsea alisimamia Mechi 4 dhidi ya Benfica 
na kushinda 1 tu na kufungwa 3.
-Katika Mechi za UEFA, Bernitez amesimamia Mechi 138 na Jorge Jesus wa Benfica 
Mechi 74 Baada ya kutwaa Taji hili na Valencia Mwaka 2003/04,
Benitez anaweza kuwa Kocha wa Pili, baada ya Giovanni Trapattoni ambae ameshinda mara 3,
kulitwaa na Klabu mbili tofauti Wengine waliotwaa mara mbili ni Luis Molowny akiwa
(Real Madrid, 1985 na 1986) na Juande Ramos (Sevilla FC, 2006 na 2007).