RAIS wa club ya Paris St-Germain amemthibitishia meneja wa timu hiyo CarloAncelotti hataruhusiwa kuihama Klabu hiyo kwenda Real Madrid huko Jijini Madrid huku Uongozi wa Real madrid upo katika mipango ya kumtimua Jose Mourinho huku wakiwa na Mechi mbili za La Liga kumalizia Msimu.
Inaaminika leo Bodi ya Real Madrid inafanya Kikao na inategemewa kutoa tamko la kumtimua Jose Mourinho na hatua hii inakuja hasa baada ya Ijumaa kunyukwa kwenye Fainali ya Copa del Rey Bao 2-1 na Atletico Madrid na kuhakikisha Msimu huu wanamaliza bila Taji kubwa ukiondolea mbali Super Cup.
Jumamosi ijayo Real Madrid wanapepetana na Real Sociedad katika Mechi ya La Liga ya kukamilisha Ratiba tu kwa vile wao wameshakamata Nafasi ya Pili na Bingwa tayari ni Mahasimu wao FC Barcelona ambao wamewavua Ubingwa.
tetesi zilizopo Jose Mourinho yuko mbioni kurudi Klabu yake ya zamani Chelsea.
Na huko Paris, Rais wa PSG kutoka Nchini Qatar, Nasser al-Khelaifi, amemkatalia Carlo Ancelotti kuondoka Klabu hiyo baada ya Meneja huyo kuomba kufanya hivyo.
Ancelotti, Miaka 53, amesema: “Nimeomba kuondoka na hivyo nasubiri jibu!”
Nae Rais Nasser al-Khelaifi amejibu: “Ameomba kuondoka kwenda Real. Haiwezekani kwa vile bado ana Mkataba wa Mwaka mmoja, hivyo huo ni uamuzi wetu
ANCELOTTI-Mafanikio:
Juventus: Intertoto Cup 1999
AC Milan: Coppa Italia 2003, UCL 2003 & 2007, UEFA SUPER CUP 200 & 2007; Serie A 2004; Supercoppa Italiana 2004; Fifa Club World Cup 2007
Chelsea: Ngao ya Jamii 2009; BPL 2010; FA CUP 2010
PSG: Ligue 1 2013