Baada ya kuipa mafanikio ya kutosha Bayern muninch Jupp Heynckes hatimaye amebainisha kuwa hataendelea kufanya kazi hiyo baada ya kuondoka kwa mabingwa wa soka barani Ulaya. Bayern wakiwa chini ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 wamefanikiwa kumaliza msimu kwa mafanikio kwa kunyakuwa mataji matatu ya Bundesliga, DFB-Pokal na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa mafanikio hayo Bayern imekuwa klabu ya saba barani Ulaya kufanikiwa kushinda mataji matatu mfululizo. Hatahivyo Heynckes ameamua kustaafu kufundisha baada ya nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola.
Sunday, June 16, 2013
FIFA YATANGAZA KUWA MZUNGUUKO WA TATU KUFUZU KOMBE LA DUNIA NI MWEZI SEPTEMBER.
SHIRIKISHO la Soka Dunia-FIFA limetangaza kuwa mzunguko wa tatu wa mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 pamoja na hatua ya mtoano kwa nchi za barani Ulaya itafanyika Septemba na Octoba mwaka huu. Ratiba kwa upande wa nchi za Afrika ambazo zitajumuisha washindi kutoka katika makundi 10 itafanyika Septemba 16 jijini Cairo, Misri ambapo nchini tano zilizo juu katika viwango vya ubora vya FIFA ndizo zitaongoza ratiba hiyo. Nchi nane zitakazomaliza katika nafasi ya pili barani Ulaya nazo zitapangiwa ratiba jijini Zurich, Switzerland Octoba 21 huku nchi nne kati ya zilizo juu katika viwango vya FIFA zikiongoza ratiba hiyo. Tanzania inajitupa uwanjani leo kuvukuzia nafasi ya kuingia katika ratiba hiyo kwa kupambana na Tembo wa Ivory Coast katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
SIMBA, YANGA, SUPER FALCOM HAZIENDI SUDAN KWENYE KAGAME:
KLABU za Tanzania hazitakwenda kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame inayofanyika kuanzia wiki ijayo mjini Kigali, Rwanda.
Hiyo inafuatia kuingiliana kwa taarifa za Serikali, awali ilielezea kuzizuiatimu hizo kwenda sudani kutokana na hali ya machafuko, na baadaye ikiziruhusu kwenda baada ya kuhakikishiwa usalama wa klabu hizo na Serikali ya Sudan kuwa zitapata ulinzi wa kutosha.
serikali ilitoa ruhusa kwa timu hizi baada ya kupata uthibitisho kutoka serikali ya sudani huku ukitazama mashindano haya yanaanza Jumanne june 18 ambapo club hazijafanya maandalizi yoyote ya safari.
mbali na hiyo haitoshi baada ya zuio la awali, CECAFA (Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati) likateua timu mbadala kuziba nafasi ya timu tatu za Tanzania.
aidha Timu za bongo kwetu tanzania zilizotarajiwa kushiriki michuano hiyo ni Simba SC, Yanga za Dar es Salaam na Super Falcons ya Zanzibar.
katika hali ya kawaida Sasamichuano hii ya Kagame mwaka huu, haikustahili kufanyika Sudan, ambako kila siku tunasikia watu wanauawa kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, lakini kutokana na sababu zake katibu wa CECAFA Musonye ameamua kuipeleka huko.
Hivyo mtandao huu umefanya mazungumzo mbalimbali za wadau wa michezo hapa nchini ambapo miongoni mwao wamezungumza katika hali ya kawaida endapo machafuko ya kitokea"
inaamaa vilabu vya tanzania ndio vitapata fursa ya kuwa chini ya uangalizi haya yote yanatokana kauli ya serikali ya sudani kuiandikia barua serikali ya tanzania kupitia wizira ya habari utamaduni na michezo kuwa timu za tanzania zitapata ulinzi wa kutoka katika michuani hiyo.
katika hali ya kawaida wadau wamesema haiingii akilini kuzipeleka timu na kwenda kuziangamiza katika nchi ambayo haishiwi vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Hata hivyo katika hali ya kawaida inamaana vilabu vya tanzania ndio vyenye umuhimu katika suala la ulinzi vipi kenya na burundi pamoja na uganda vilabu hivi havihitaji ulinzi?".
Mbali ya yote michuano hii haikustahili kuchezwa Sudani kutokana na sababu ambazo kila mtu anazifamu vita za wenyewe kwa wenyewe ambapo kila siku tunasikia vurugu za hapa na pale.Tukumbuke michezo ni burudani na starehe ya aina yake endapo kutakuwa na vurugu za hapa na pale pasi furaha ya michezo inapotea kabisa Hivyo CECAFA kwa mara nyingine tena tulitazame hili.
RATIBA KOMBE LA KAGAME ILIKUWA HIVI:
KUANZIA JUNI 18 HADI JULAI 2, 2013 (EL-FASHIR NA KADUGLI, SUDAN)
TAREHE TIMU TIMU KUNDI/MUDA UWANJA
18.06.2013. TUSKER SUPER FALCON B - SAA 8:00 MCHANA KADUGLI
AL HILLAL AL NASRI B -SAA 10:00 JIONI KADUGLI
19.06.2013. VITALOO PORTS C - SAA 10:00 JIONI EL-FASHER
20.06.2013. YANGA SC EXPRESS C - SAA 8:00 MCHANA EL-FASHER
20.06.2013. ELMAN FC APR FC A - SAA 10:00 JIONI EL-FASHER
20.06.2013. SUPER FALCON AL NASRI B -SAA 8:00 MCHANA KADUGLI
20.06.2013. TUSKER AL-SHANDY B -SAA 10:00 JIONI KADUGLI
21.06.2013. EL MERREIKH SIMBA SC A -SAA 10:00 JIONI KADUGLI
22.06.2013. EXPRESS FC VITALOO C - SAA 8:00 MCHANA EL-FASHER
PORTS YANGA SC C -SAA 10:00 JIONI EL FASHER
22.06.2013. AL NASRI TUSKER B - SAA 8:00 MCHANA KADUGLI
AL SHANDY AL HILAL B -SAA 10:00 JIONI KADUGLI
23.06.2013 APR SIMBA SC A - SAA 8:00 MCHANA EL-FASHER
EL MERREIKH ELAM FC A -SAA 10:00 JIONI
EL-FASHER
24.06.2013 AL NASRI AL SHANDY B -SAA 8:00 MCHANA KADUGLI
SUPER FALCON AL HILLAL B -SAA 10:00 JIONI KADUGLI
24.06.2013. PORTS EXPRESS FC C -SAA 10:00 JIONI EL-FASHER
25.06.2013. VITALOO YANGA SC C -SAA 10:00 JIONI EL-FASHER
26.06.2013. AL SHANDY SUPER FALCON B -SAA 8:00 MCHANA KADUGLI
AL HILLAL TUSKER B -SAA 10:00 JIONI KADUGLI
26.06.2012. SIMBA SC ELMAN FC A -SAA 8:00 MCHANA EL-FASHER
APR FC EL MERREIK A -SAA 10:00 JIONI EL-FASHER
27.06.2013. MAPUMZIKO MAPUMZIKO MAPUMZIKO
MAPUMZIKO
28.06.2013. (23) B2 VS C2 (24) B1 VS BEST Q UTATANGAZWA KADUGLI
28.06.2013. (25) C1 VS A2 (26) A1 VS B3 UTATANGAZWA EL-FASHER
30.06.2013. WNR 23 VS WNR 25 WIN 24 VS WIN 26 UTATANGAZWA
01.07.2013. MAPUMZIKO MAPUMZIKO MAPUMZIKO MAPUMZIKO
02.07.2013. ILIYOFUNGWA ILIYOFUNGWA MSINDI WA TATU EL-FASHER
ALIYESHINDA 27 ALIYESHINDA 28 FAINALI
TAREHE | TIMU | TIMU | KUNDI/MUDA | UWANJA |
18.06.2013. | TUSKER | SUPER FALCON | B - SAA 8:00 MCHANA | KADUGLI |
AL HILLAL | AL NASRI | B -SAA 10:00 JIONI | KADUGLI | |
19.06.2013. | VITALOO | PORTS | C - SAA 10:00 JIONI | EL-FASHER |
20.06.2013. | YANGA SC | EXPRESS | C - SAA 8:00 MCHANA | EL-FASHER |
20.06.2013. | ELMAN FC | APR FC | A - SAA 10:00 JIONI | EL-FASHER |
20.06.2013. | SUPER FALCON | AL NASRI | B -SAA 8:00 MCHANA | KADUGLI |
20.06.2013. | TUSKER | AL-SHANDY | B -SAA 10:00 JIONI | KADUGLI |
21.06.2013. | EL MERREIKH | SIMBA SC | A -SAA 10:00 JIONI | KADUGLI |
22.06.2013. | EXPRESS FC | VITALOO | C - SAA 8:00 MCHANA | EL-FASHER |
PORTS | YANGA SC | C -SAA 10:00 JIONI | EL FASHER | |
22.06.2013. | AL NASRI | TUSKER | B - SAA 8:00 MCHANA | KADUGLI |
AL SHANDY | AL HILAL | B -SAA 10:00 JIONI | KADUGLI | |
23.06.2013 | APR | SIMBA SC | A - SAA 8:00 MCHANA | EL-FASHER |
EL MERREIKH | ELAM FC | A -SAA 10:00 JIONI |
EL-FASHER
|
24.06.2013 | AL NASRI | AL SHANDY | B -SAA 8:00 MCHANA | KADUGLI |
SUPER FALCON | AL HILLAL | B -SAA 10:00 JIONI | KADUGLI | |
24.06.2013. | PORTS | EXPRESS FC | C -SAA 10:00 JIONI | EL-FASHER |
25.06.2013. | VITALOO | YANGA SC | C -SAA 10:00 JIONI | EL-FASHER |
26.06.2013. | AL SHANDY | SUPER FALCON | B -SAA 8:00 MCHANA | KADUGLI |
AL HILLAL | TUSKER | B -SAA 10:00 JIONI | KADUGLI | |
26.06.2012. | SIMBA SC | ELMAN FC | A -SAA 8:00 MCHANA | EL-FASHER |
APR FC | EL MERREIK | A -SAA 10:00 JIONI | EL-FASHER | |
27.06.2013. | MAPUMZIKO | MAPUMZIKO | MAPUMZIKO |
MAPUMZIKO
|
28.06.2013. | (23) B2 VS C2 | (24) B1 VS BEST Q | UTATANGAZWA | KADUGLI |
28.06.2013. | (25) C1 VS A2 | (26) A1 VS B3 | UTATANGAZWA | EL-FASHER |
30.06.2013. | WNR 23 VS WNR 25 | WIN 24 VS WIN 26 | UTATANGAZWA | |
01.07.2013. | MAPUMZIKO | MAPUMZIKO | MAPUMZIKO | MAPUMZIKO |
02.07.2013. | ILIYOFUNGWA | ILIYOFUNGWA | MSINDI WA TATU | EL-FASHER |
ALIYESHINDA 27 | ALIYESHINDA 28 | FAINALI |
NEYMA AFANYA MAMBO KATIKA KOMBE LAMICHUANO YA KOMBE LA MABARA-UFUNGUZI

MSHAMBULIAJI nyota mpya wa Fc Barcelona,Neymar jana alifanikiwa kung'arisha nyota yake katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mabara, akifunga bao la mapema dakika ya tatu wakati Brazil inailaza 3-0 Japan.
Mshambuliaj huyo nyota wa Brazil, alifunga kwa shuti la nje ya eneo la hatari, akiunganisha pasi ya Fred ambaye naye alipokea krosi ya Marcelo kwa kifua kwanza.
Ushindi huo unaiweka Brazil kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake tatu. Italia na Mexico watamenyana leo katika mechi nyingine ya kundi hilo.
Kikosi cha Brazil jana kilikuwa; Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Oscar, Gustavo, Paulinho, Fred/Jo dk81, Neymar/Lucas Moura dk74 na Hulk/Hernanes dk75.
Japan: Kawashima, Konno, Nagatomo, Uchida, Yoshida, Endo/Hosogai dk77, Honda/Inui dk88, Kiyotake/Maeda dk51,Kagawa, Hasebe na Okazaki.
LUCAS ASEMA SUAREZ AKIONDOKA NI PENGO KUBWA KWA LIVERPOOL

MESSI AMUACHA MARADONA KATIKA ORODHA YA WAFUNGAJI TIMU YA TAIFA
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na club ya fc barcelona Lionel Messi amemuacha nguli wa soka wan chi hiyo Diego Maradona katika orodha ya wafungaji kufuatia mabao matatu aliyofunga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Guatemala ambao walishinda kwa mabao 4-0. Nyota huyo wa Barcelona alifungua karamu ya mabao katika dakika ya 15 ya mchezo kabla ya kuongeza lingine muda mchache kabla ya mapumziko huku bao la tatu akifunga katika dakika ya 52 na kufikisha jumla ya mabao 35 kwa timu ya taifa na kumuacha Maradona ambaye aliwahi kuifungia timu hiyo mabao 34. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Messi kama kawaida yake alidai kumzidi Maradona kwa mabao sio suala muhimu kwake kitu cha msingi ni kwamba walicheza kwa umoja ndio maana wamepata matokeo mazuri. Messi sasa anawakaribia nyota wengine wa nchi hiyo ambao ni Hernan Crespo huku bado akiwa na safari ndefu ya kumfikia kinara wa ufungaji wa nchi hiyo Gabriel Batistuta ambaye kipindi chake akiichezea Argentina alifunga mabao 56.
Friday, June 14, 2013
MAKOCHA STARS, IVORY COAST ANA KWA ANA
Wakati timu ya Ivory Coast imewasili nchini jana usiku (Juni 13 mwaka huu) kwa ndege maalum, kocha wa timu hiyo Sabri Lamouchi na mwenzake wa Taifa Stars, Kim Poulsen watakutana na waandishi wa habari kuzungumzia mechi yao.
Mkutano huo utafanyika kesho (Juni 15 mwaka huu) saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Mkutano huo pia utajumuisha makocha wa timu zote mbili. Ivory Coast inafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Juni 14 mwaka huu) saa 9 alasiri kwenye viwanja vya Gymkhana.
Timu zote kesho (Juni 15 mwaka huu) zitafanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ivory Coast watafanya mazoezi saa 9 kabla ya kuwapisha Stars saa 10 kamili. Maandalizi yanaendelea vizuri ikiwemo kuwasili kwa maofisa wote wa mechi itakayochezwa Jumapili saa 9 kamili alasiri.
Wakati huo huo, mauzo ya tiketi kwa ajili ya mechi hiyo yameanza leo mchana (Juni 14 mwaka huu) katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, City Sports Lounge iliyoko Mtaa wa Samora na Azikiwe, Dar Live Mbagala, BMM Salon iliyoko Sinza Madukani na Uwanja wa Taifa.
Mauzo yataendelea kesho katika vituo hivyo, wakati siku ya mchezo yatafanyika Uwanja wa Taifa. Viingilio katika mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika katika kundi C ni sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B na VIP A sh. 30,000. Pia kuna kadi maalumu 100 kwa viti vya Wageni Maalumu (VVIP) zinazopatikana kwa sh. 50,000 katika ofisi za TFF.
TFF YATOA NOTISI YA MKUTANO MKUU
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ametoa notisi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Shirikisho utakaofanyika Julai 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam ukiwa na ajenda moja ya marekebisho ya Katiba.
Notisi hiyo imetolewa juzi (Juni 12 mwaka huu). Rais ameitisha Mkutano huo kwa mujibu wa Ibara ya 25(1) ya Katiba ya TFF baada ya kupata maagizo kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa barua yake ya Aprili 29 mwaka huu.
Ajenda rasmi na taarifa nyingine zitatumwa kwa wajumbe siku 15 kabla ya Mkutano huo kwa mujibu wa Ibara ya 25(4) ya Katiba ya TFF. Wanachama wa TFF ambao ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu wanatakiwa kutuma majina ya wajumbe halali.
TFF inapenda kuwakumbusha wanachama wake kutuma majina ya wajumbe halali ili kufanikisha maandalizi ya Mkutano huo. Ni vizuri kuhakikisha kuwa jina linalotumwa ni la mjumbe halali wa Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya TFF.
RCL YAINGIA HATUA YA TATU WIKIENDI HII
Mechi za kwanza za hatua ya tatu ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao zinachezwa wikiendi hii kwenye viwanja vinne tofauti.
Mechi za kesho (Jumamosi) ni kati ya Kariakoo ya Lindi na Friends Rangers ya Dar es Salaam utakaochezwa katika Uwanja wa Ilulu mjini Lindi wakati Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Kimondo SC na Njombe Mji.
Timu za Machava FC ya Kilimanjaro na Stand United FC ya Shinyanga, Polisi Jamii ya Mara na Katavi Warriors ya Katavi zilizokuwa zipambane kesho mechi zao zimesogezwa mbele hadi keshokutwa (Jumapili). Mechi hizo zimesogezwa kutokana na viwanja vya Ushirika mjini Moshi na Karume mjini Musoma kuwa na shughuli nyingine za kijamii.
Hata hivyo, TFF imesisitiza kuwa ikibainika kuwa viwanja hivyo havikutumika kwa shughuli za kijamii siku hiyo ya Jumamosi, hatua kali zitachukuliwa kwa wanachama wake (vyama vya mpira wa miguu vya mikoa husika).
Mechi za marudiano za hatua hiyo ya tatu zitachezwa Juni 19 mwaka huu. Hatua ya nne ya RCL itachezwa kati ya Juni 23 na 23 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 29 na 30 mwaka huu.
RAMBIRAMBI MSIBA WA ABDALLAH MSAMBA
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Pan Africans, Simba na Taifa Stars, Abdallah Msamba kilichotokea juzi usiku (Juni 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Msamba akiwa mchezaji, na baadaye kocha wa timu kadhaa alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea na kufundisha ikiwemo Villa Squad, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Msamba, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) na klabu ya Villa Squad na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Maziko ya mchezaji huyo yamefanyika leo (Juni 14 mwaka huu) katika makaburi ya Ndugumbi mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji wakiwemo wachezaji wa zamani na viongozi mpira wa miguu nchini. Mungu aiweke roho ya marehemu Msamba mahali pema peponi. Amina
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Subscribe to:
Posts (Atom)