Sunday, February 16, 2014

BUNDESLIGA: BAYERN, DORTMUND ZATOA DOZI YA BAO 4 KILA MMOJA

Bayern Munich, Mabingwa Watetezi na Vinara wa Bundesliga, wameendelea kukwea kileleni mwa Ligi hiyo baada ya Bundasliga baaada ya kuichalaza Freiburg Bao 4-0.
Bao za Bayern Munich zilifungwa na Dante, Xherdan Shaqiri, Bao 2, na Claudio Pizarro.
Kwa upande wa Borussia Dortmund wameinyamazisha  Eintracht Frankfurt Bao 4-0 kwa Bao za Pierre Emerick Aubameyang, Bao 2, Robert Lewandowski, kwa Penati, na Jojic.
Ushindi huu umewafanya Dortmund waikaribie Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 1 nyuma ya Bayer Leverkusen ambayo Jana ililala kwa Bao 2-1 na Schalke.

RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Februari 14
FSV Mainz 2 Hannover 0
Jumamosi Februari 15
Bayern Munich 4 SC Freiburg 0
BV Borussia Dortmund 4 Eintracht Frankfurt 0
SV Werder Bremen 1 Borussia Mönchengladbach 1
Eintracht Braunschweig 4 Hamburger SV 2
TSG Hoffenheim 4 VfB Stuttgart 1
Bayer 04 Leverkusen 1 Schalke 2
[Saa za Bongo]
Jumapili Februari 16
1730 FC Augsburg v FC Nuremberg
1930 Hertha Berlin v VfL Wolfsburg

MSIMAMO-Timu za Juu:
NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Bayern Munich 21 19 2 0 57 9 48 59
2 Bayer 04 Leverkusen 21 14 1 6 38 26 16 43
3 BV Borussia Dortmund 21 13 3 5 51 24 27 42
4 Schalke 04 21 12 4 5 41 30 11 40
5 Borussia Mönchengladbach 21 10 4 7 37 26 11 34
6 VfL Wolfsburg 20 10 3 7 33 24 9 33
7 FSV Mainz 05 21 10 3 8 31 35 -4 33
8 Hertha Berlin 20 9 4 7 31 24 7 31
9 FC Augsburg 20 9 4 7 30 29 1 31

LA LIGA: BARCA YAITANDIKA 6-0 RAYO VALLECANO

FC Barcelona Mabingwa Watetezi wa La Liga huko SPAIN,Jana Usiku wakiwa katiak dimba la Nou Camp, waliichalaza Rayo Vallecano Bao 6-0 na kuendelea kukaa kileleni mwa Ligi hiyo wakifungana kwa Pointi na Atletico Madrid lakini wao wako juu kwa ubora wa Magoli.
Goli za Barca kwenye Mtanange huo yamewekwa kimiani na Neymar, Lionel Messi, Bao 2, Pedro, Sanchez na Adriano.
Nao, Atletico Madrid, mapema hiyo Jana waliichapa Real Valladolid Bao 3-0 kwa Bao za Raul Garcia Escudero
, Diego Costa na Diego Godin.
Leo hii Real Madrid, ambao wako Ugenini kucheza na Getafe, wana nafasi ya kuzikamata Barca na Atletico ikiwa watashinda lakini watamkosa Supastaa wao Cristiano Ronaldo ambae atakuwa akitumikia Mechi ya Pili ya Kifungo chake cha Mechi 3.
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Ijumaa Februari 14
Elche CF 0 Osasuna 0
Jumamosi Februari 15
Atletico de Madrid 3 Real Valladolid 0
Levante 1 UD Almeria 0
FC Barcelona 6 Rayo Vallecano 0
Villarreal CF 0 Celta de Vigo 2
Jumapili Februari 16
1400 Granada CF v Real Betis
1900 Getafe CF v Real Madrid CF
2100 Athletic de Bilbao v RCD Espanyol
2300 Sevilla FC v Valencia
Jumatatu Februari 17
2400 Malaga CF v Real Sociedad
MSIMAMO-Timu za Juu:

NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 FC Barcelona 24 19 3 2 69 17 52 60
3 Atletico Madrid 24 19 3 2 59 16 43 60
2 Real Madrid CF 23 18 3 2 65 24 41 57
4 Athletic Bilbao 23 13 5 5 42 28 14 44
5 Villarreal CF 24 12 4 8 44 29 15 40
6 Real Sociedad 23 10 7 6 42 34 8 37
7 Sevilla FC 23 8 7 8 42 41 1 31
8 Valencia 23 9 4 10 36 35 1 31

JK AWAPA RUNGU CCM, AWATAKA KUACHA UNYONGE DHIDI YA CHADEMA".

MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amewapa rungu wana-CCM akiwataka  kuacha kujifanya wanyonge dhidi ya vitendo vya fujo ambavyo hufanyiwa na  Chadema hasa nyakati za uchaguzi.




Rais Kikwete amesema hayo leo, wakati akiongoza kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini Dodoma.

“Uchaguzi wa Kalenga ndiyo huo upo mbele yetu, hadi sasa hakuna tatizo lililojitokeza kama Arumeru mambo yapo shwari kabisa, lakini tujue tu kwamba pale tunaenda kushindana na watu (Chadema) ambao wao silaha yao ya kwanza ni vujo.. ninaagiza sasa lazima wana CCM kukabiliana na fujo zao. Unyonge basi.”, alisema Rais Kikwete na kuongfeza;

“CCM kuendelea kujifanya wanyonge kila mara sasa basi. Haiwezekazi watu wanafanya vujo hadi kuwatoboa watu macho ninyi nmanyongea tu, hili haliwezekani. Tazama pale Ingunga  mtu wenu alimwagiwa tindikali hadi leo ana  ulemavu wa kudumu kisa uchaguzi tu, aah haiwezekani kabisa”, alisema Rais Kikwete.

Mapema Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete alipongeza wana CCM na viongozi wao katika Kata zote zilizofanya uchaguzi mdogo wa Udiwani na hatimaye CCM kuibuka na ushindi wa Kata 23, Chadema ikiambulia tatu na NCCR Mageuzi kimoja.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-brGp3ubKcaSU7smoXfjTAApUg9f-YwbT3atmCqVx6i5JXWg8q23PhU_rOCHS91U3LbUya0oXNUJ93VIe3GyKWlXoqePApyka_4M8sqa37GHHhi73ftK2h3rYFcUf6wh4kx3U6iR6777q/s1600/13.jpg
Hata hivyo Rais Kikwete alisema, licha ya CCM kuzoa kata nyingi kwenye uchaguzi huo, viti vinne kwenda kwa upinzani bado ni doa hivyo lazima CCM Kihakikishe inazikomboaata hizo nyakati za chaguzi zijazo.

“Ni kweli tumezoa kata nyingi, lakini kwa kuwa lengo letu CCM kila wakati ni kushinda tu, hatua hiyo ya kuzikosa kata nne bado ni doa lazima kuzikomboa kata hizo chaguzi zijazo”, alisema, Rais Kikwete.

Pia alipongeza CCM, kwa ushindi iliopata kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Kimbesamaki na kwamba CCM inaona fahari kulirejesha jimbo hilo mikononi mwake, kwa kuwa ilikuwa imelazimika kumfuza mwakilishi wake wa awali kwenye jimbo hilo kwa kuwa alikuwa msaliti aiyefaa kuendelea kuwemo ndani ya Chama

Saturday, February 15, 2014

VPL: MBEYA CITY YATOKA SARE 1-1 VS SIMBA DIMBANI SOKOINE

VPL_2013-2014-FPLigi Kuu Vodacom tanzania Bara  imeendelea leo katika Viwanja mbalimbali lakini mchakamchaka ulikuwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya ambapo Wagonga Nyondo Mbeya City waliumana uso kwa uso na Simba na matokeo kuwa Sare ya Bao 1-1.
Mbeya City ndio walikuwa wa kwanza kutikisa Nyavu  katika Dakika ya 14 kwa Penati ya Deogratius Julius na Amisi Tambwe kuisawazishia Simba katika Dakika ya 50.
Simba na Mbeya City sasa zimecheza Mechi mbili zaidi ya Vinara Azam FC, wenye Pointi 36, na Timu ya Pili Yanga, wenye Pointi 35.
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Februari 15
Rhino Rangers 1 Mgambo JKT 1
Ashanti United 0 Kagera Sugar 0
Mtibwa Sugar 0 Tanzania Prisons 1
JKT Oljoro 0 JKT Ruvu 0
Mbeya City 1 Simba 1
Ruvu Shooting 1 Coastal Union 0
­­MSIMAMO  VPL:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
16
10
6
0
19
36
2
Yanga SC
16
10
5
1
22
35
3
Mbeya City
18
9
8
1
10
35
4
Simba SC
18
8
8
2
17
32
5
Ruvu Shooting
17
6
7
4
3
25
6
Kagera Sugar
18
5
8
5
0
23
7
Coastal Union
18
4
10
4
3
22
8
Mtibwa Sugar
18
5
7
6
-1
22
9
JKT Ruvu
17
6
1
10
-8
19
10
Ashanti United
17
3
5
9
-14
14
11
JKT Oljoro
18
2
8
8
-14
14
11
Mgambo
18
3
5
10
-18
14
14
Prisons FC
15
2
7
6
-9
13
12
Rhino Rangers
18 3 6 9 -10 13

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano Februari 19
Tanzania Prisons v JKT Ruvu
Jumamosi Februari 22
Ruvu Shooting v Yanga
Kagera Sugar v Rhino Rangers
Mtibwa Sugar v Ashanti United
Coastal Union v Mbeya City
JKT Oljoro v Mgambo JKT
Azam FC v Tanzania Prisons
Jumapili Februari 23
Simba v JKT Ruvu