Sunday, February 16, 2014

LA LIGA: BARCA YAITANDIKA 6-0 RAYO VALLECANO

FC Barcelona Mabingwa Watetezi wa La Liga huko SPAIN,Jana Usiku wakiwa katiak dimba la Nou Camp, waliichalaza Rayo Vallecano Bao 6-0 na kuendelea kukaa kileleni mwa Ligi hiyo wakifungana kwa Pointi na Atletico Madrid lakini wao wako juu kwa ubora wa Magoli.
Goli za Barca kwenye Mtanange huo yamewekwa kimiani na Neymar, Lionel Messi, Bao 2, Pedro, Sanchez na Adriano.
Nao, Atletico Madrid, mapema hiyo Jana waliichapa Real Valladolid Bao 3-0 kwa Bao za Raul Garcia Escudero
, Diego Costa na Diego Godin.
Leo hii Real Madrid, ambao wako Ugenini kucheza na Getafe, wana nafasi ya kuzikamata Barca na Atletico ikiwa watashinda lakini watamkosa Supastaa wao Cristiano Ronaldo ambae atakuwa akitumikia Mechi ya Pili ya Kifungo chake cha Mechi 3.
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Ijumaa Februari 14
Elche CF 0 Osasuna 0
Jumamosi Februari 15
Atletico de Madrid 3 Real Valladolid 0
Levante 1 UD Almeria 0
FC Barcelona 6 Rayo Vallecano 0
Villarreal CF 0 Celta de Vigo 2
Jumapili Februari 16
1400 Granada CF v Real Betis
1900 Getafe CF v Real Madrid CF
2100 Athletic de Bilbao v RCD Espanyol
2300 Sevilla FC v Valencia
Jumatatu Februari 17
2400 Malaga CF v Real Sociedad
MSIMAMO-Timu za Juu:

NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 FC Barcelona 24 19 3 2 69 17 52 60
3 Atletico Madrid 24 19 3 2 59 16 43 60
2 Real Madrid CF 23 18 3 2 65 24 41 57
4 Athletic Bilbao 23 13 5 5 42 28 14 44
5 Villarreal CF 24 12 4 8 44 29 15 40
6 Real Sociedad 23 10 7 6 42 34 8 37
7 Sevilla FC 23 8 7 8 42 41 1 31
8 Valencia 23 9 4 10 36 35 1 31