kutokana katika mechi 23 alizoichezea Simba SC hadi sasa za
mashindano yote na kirafiki, amefunga mabao 17.
Kwa sasa, Tambwe ndiye mchezaji anayeongoza kwa mabao katika
Ligi Kuu, akiwa amefunga mabao 15 na anafuatiwa kwa mbali na mshambuliaji wa
AzamFC, Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast, mwenye mabao
10.
Tambwe amekuwa kipenzi cha wana Msimbazi kutokana na kuweza
pia kutikisa nyavu za mahasimu, Yanga SC katika mechi mbili mfululizo
baina ya timu hizo.
Tambwe alikuja Simba SC kwa pamoja na Mrundi mwenzake, beki
Gilbert Kazewakitokea wote Vital’O msimu huu, baada ya kung’ara katika
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame nchini Sudan wakiiwezesha
klabu yao kutwaa taji la michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika
historia yake.
Hata hivyo, Kaze amepoteza namba katika kikosi cha kwanza
tangu ujio wa kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic, ambaye amekuwa akimpanga
beki Mkenya, Donald Mosoti aliyetokea naye Gor Mahia ya Kenya.