Azam FC imefungwa mabao 2-0 na wenyeji wake Ferreviario ya
Msumbuji maarufu kama Wamakonde katika mechi iliyopigwa hii leo mjini Beira.
Katika mechi ya kwanza Azam FC ilishinda bao 1-0 kwenye Uwanja
wa Azam Complex, Chamzi jijini Dar. Mfungaji akiwa Kipre Tchetche.
Kutokana na kipigo cha leo, maana yake Azam FC imetolewa kwa
jumla ya mabao 2-1 na kuifanya kutoka mapema zaidi katika michuano hiyo ndani
ya misimu mitatu.