Thursday, July 17, 2014

STARS YAREJEA DAR, KAZIMOTO NDANI

Kikosi cha Taifa Stars kimerejea jijini Dar es Salaam leo kutoka Mbeya ambapo Jumapili (Julai 20 mwaka huu) kitapambana na Msumbiji (Mambas) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Benchi la Ufundi la Taifa Stars pamoja
na wachezaji kesho (Julai 19 mwaka huu) saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Courtyard iliyopo Upanga Seaview jijini Dar es Salaam.
Naye mchezaji Mwinyi Kazimoto amewasili leo 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways kutoka Qatar ambapo anacheza mpira wa miguu katika klabu ya Al Markhiya ya huko. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi katika hoteli ya Protea Courtyard.
SERENGETI BOYS MORALI JUU
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Hababuu Ali Omari amesema morali ya wachezaji wake ipo juu kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) itakayochezwa kesho (Julai 18 mwaka huu).
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 itafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo, Kocha Hababuu amesema nia ya kikosi chake ni kuhakikisha wanafika kwenye fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Niger.
Kikosi-cha-Serengeti-Boys-Under-20“Tunaiheshimu Afrika Kusini, lakini hatuiogopi. Morali ya wachezaji ipo juu na wanajiamini. Kimsingi wanajua kuwa hii ndiyo njia ya wao kutokea kwenye mpira wa miguu, kwa hiyo lengo ni kushinda,” amesema Kocha Hababuu.
Naye Kocha wa Afrika Kusini, Molefi Ntseki amesema anaziheshimu timu za Tanzania, na changamoto aliyonayo ni kuhakikisha kuwa anashinda mechi hiyo kwani mara ya mwisho kwa timu yake kushiriki fainali za Afrika ilikuwa miaka sita iliyopita.
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000 na tiketi zitapatikana uwanjani kwenye magari maalumu.
MSUMBIJI KUTUA MCHANA DAR
Timu ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) inawasili Dar es Salaam kesho (Julai 18 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mambas itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.30 mchana kwa ndege ya LAM ikiwa na TFF_LOGO12msafara wa watu 37 ambapo kati ya hao, 25 ni wachezaji.
Wachezaji kwenye msafara huo ni Almiro Lobo, Apson Manjate, Bone Mario Uaferro, Dario Ivan Khan, Edson Sitoe, Eduardo Jumisse, Gelicio Aurelio Banze, Helder Pelembe, Josemar Machaisse, Elias Pelembe, Isac Carvalho na Jeffrey Constatino.
Wengine ni Manuel Fernandes, Manuel Uetimane, Mario Sinamunda, Momed Hagi, Reginaldo Fait, Reinoldo Mandava, Ricardo Campos, Saddan Guambe, Simao Mate Junior, Soares Victor Soares, Stelio Ernesto, Vando Justino na Zainadine Junior.
Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Accomondia, na itaondoka Jumapili mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mahmoud Ashour.
LINA KESSY AUTEULIWA KUWA OFISA MICHEZO AU
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Lina Kessy ameteuliwa kuwa Ofisa Michezo wa Umoja wa Afrika (AU).
Uteuzi huo umefanywa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Nkozasana Dlamini-Zuma, na Lina atatumikia nafasi hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu katika makao makuu ya AU yaliyopo Addis Ababa, Ethiopia.
Lina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) amewashukuru wote ambao kwa michango yao ya hali na mali imemwezesha kufika hapo.
Ameishukuru TFF kwa kumlea na kumjenga. Shukrani nyingine amezitoa kwa Serikali kupitia Kurugenzi ya Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).
TFF inampongeza kwa uteuzi huo, na tunaamini ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania ikiwemo kuwa chachu ya maendeleo ya michezo kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Wednesday, July 16, 2014

CHELSEA YAMNASA MBADALA WA COLE KUTOKA ATLETICO.

KLABU ya Atletico Madrid imetangaza kuwa imefikia makubaliano na Chelsea kuhusu uhamisho wa Filipe Luis. Chelsea kwa kipindi kirefu amekuwa wakihusishwa na kutaka kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 huku mwezi Juni wakiipa taarifa Atletico kuwa wako tayari kutoa paundi milioni 20 zilizowekwa katika mkataba wake. Atletico wamethibitisha rasmi kuwa wameshakubaliano juu ya uhamisho huo na kilichobakia ni mchezaji huyo kufanyiwa vipimo vya afya na Chelsea. Luis anatarajiwa kuziba nafasi ya Ashley Cole aliyeruhusiwa kuondoka kwenda Roma kama mchezaji huru kufuatia kumalizika kwa mkataba wake. Beki huyo wa kushoto atajiunga na mchezaji mwenzake Diego Costa ambaye naye alikamilisha usajili wake kutoka Atletico uliogharimu kiasi cha paundi milioni 35 mapema wiki hii. Luis anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Chelsea katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi baada ya kusajiliwa kwa Costa, Cesc Fabregas na kiungo chipukizi Mario Pasalic.



NBA: DENG AENDA KUZIBA PENGO LA LEBRON JAMES.

MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu kutoka nchini Uingereza, Luol Deng amejiunga na timu ya Miami Heat kama mchezaji huru. Deng ambaye amezichezea timu za Cleveland Cavaliers na Chicago Bulls msimu
uliopita anatarajiwa kuchukua nafasi ya LeBron James ambaye amehamia Cavaliers wiki iliyopita. Rais wa Heat, Pat Riley amesema Deng ni mmoja ya mchezaji muhimu waliomsajili katika historia ya timu hiyo. Deng ambaye ni mzaliwa wa Sudan aliiwakilisha Bulls kutoka mwaka 2004 mpaka 2014 na mara mbili amefanikiwa kuchaguliwa katika kikosi cha wachezaji nyota wa mchezo huo nchini Marekani, aliuzwa Cavaliers Januari mwaka huu. Heat wamefanikiwa kutinga fainali nne zilizopita za Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani-NBA ambapo walishinda mwaka 2012 na 2013 lakini walichapwa na San Antonio Spurs msimu uliopita.

GARETH BALE LEO ATIMIZA MIAKA 25 AKIWA NDANI YA REAL MADRID


 
Gareth Bale
 


Kuhusu yeye binafsi
Full name

Gareth Frank Bale
Date of birth
16 July 1989 (age 25)
Place of birth
Cardiff, Wales
Height
1.83 m (6 ft 0 in)
Playing position
Timu ya sasa
Current team
Number
11
Timu za Vijana
2005–2006
Timu za ukubwa
Years
Team
  Mechi
(Goli)
2006–2007
40
(5)
2007–2013
146
(42)
2013–
27
(15)
Timu ya Taifa
2005–2006
7
(1)
2006
1
(1)
2006–2008
4
(2)
2006–
44
(12)

AFRIKA KUSINI YAWASILI KUIVAA SERENGETI BOYS


tff_LOGO1Afrika Kusini (Amajimbos) imewasili nchini kuikabili Tanzania (Serengeti Boys) katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 itakayochezwa keshokutwa (Julai 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo yenye msafara wa watu 37 ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku (Julai 15 mwaka huu) na imefikia hoteli ya Sapphire. Amajimbos itafanya mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo kutoka Shelisheli wakiongozwa na Allister Barra tayari wamewasili nchini. Kamishna wa mechi hiyo ni Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar.
Makocha wa timu za Seregenti Boys na Amajimbos pamoja na manahodha wao watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000. Tiketi zitauzwa uwanjani katika magari maalumu siku ya mechi.
SAMATA, ULIMWENGU WATUA, MWINYI KAZIMOTO KESHO
Washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wamewasili nchini leo asubuhi (Julai 16 mwaka huu) kutoka Tunisia kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao wamefikia hoteli ya Courtyard, Seaview Upanga na leo (Julai 16 mwaka huu) watafanya mazoezi kwa programu maalumu waliyopewa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij wakati wakiwasubiri wenzao.
IMG_0750Naye kiungo Mwinyi Kazimoto anayecheza mpira wa miguu katika klabu ya Almarhiya ya Qatar atawasili nchini kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili Dar es Salaam kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 3.20 asubuhi kwa ndege ya Fastjet kutoka Mbeya tayari kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Msumbiji.

RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari Ijumaa (Julai 18 mwaka huu).