SUAREZ BADO AENDELEZA VITUKO KATIKA SOKA WADAU WAMSHANGAA
BOSI wa Liverpool, Brendan Rodgers, amekiri kutoona tukio la Straika
wake mahili Luis Suarez wakati akimng’ata Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic
bila Refa Kevin Friend kuona, FA imesema itapitia Mkanda huo na Ripoti
ya Refa ili kutoa mwelekeo huku Wachambuzi wa Soka huko England
wakilaani vikali kitendo hicho.
Brendan Rodgers ameahidi kupitia Mkanda
wa Video wa tukio hilo na kutoa tamko lakini Meneja wa zamani wa
Liverpool, Graeme Souness, amelaani vikali tukio hilo na kusema umefika
wakati wa Mchezaji huyo kutoka Uruguay kuondolewa Liverpool.
Souness ameng’ang’ania kuwa Liverpool ni
Klabu kubwa yenye hadhi kama Barcelona, Real Madrid a Manchester
United, na Mchezaji huyo anatia dosari sifa ya Klabu.
Tukio hilo la Suarez kumng’ata Ivanovic
lilitokea kwenye Mechi ya BPL, Barclays Premier League, iliochezwa
Anfield na Liverpool kutoka sare 2-2 na Chelsea huku Suarez akishika
makusudi na Chelsea kupata Penati waliyofunga na ni yeye Suarez ndie
alieisawazishia Liverpool katika Dakika za majeruhi.
MATUKIO YA MAKALI YA SUAREZ KATIKA SOKA LA DUNIA:
Akiwa Nahodha wa Ajax alifungiwa na Klabu yake baada ya kupigana na mwenzake Albert Luque wakati wa Haftaimu kwenye Mechi.
Julai 2010
Afrika na Dunia nzima itamkumbuka
Suarez, ambae ni Mchezaji wa Uruguay, kwa kuikatili Ghana huko Afrika
Kusini kwenye mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia alipoushika mpira
kwa makusudi kwenye mstari wa goli dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza
na kuwanyima Ghana goli la wazi la ushindi.
Kwa kitendo hicho, Suarez aliwashwa Kadi
Nyekundu na Ghana kupewa penati lakini Asamoah Gyan, ambae aliwahi kuwa
Ligi Kuu England na Timu ya Sunderland, alikosa kufunga penati hiyo.
Novemba 2010
Alipata Kifungo cha Mechi 7 akiwa huko
Uholanzi na Klabu ya Ajax baada ya kumng’ata meno Mchezaji wa PSV
Eindhoven Otman Bakkal kwenye mechi ya Ligi huko Uholanzi.
Octoba 2011
Wakicheza na Everton, alivunga amechezewa faulo na Jack Rodwell na kujidondosha na Rodwell akapewa Kadi Nyekundu.
Octoba 2011
Suárez alimkashifu Kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United na kufungiwa Mechi 7 na kupigwa Faini Pauni 40,000.
Decemba 2011
Akiwa kwenye mashitaka ya kumkashifu
Kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United na kabla hajahukumiwa
alionekana kutoa ishara ya matusi kwa Mashabiki wa Fulham kitendo
ambacho kilimpa Kifungo cha Mechi 1.
Februari 2012
Man United na Liverpool walikutana tena
Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu tukio la Suarez kumkashifu
Kibaguzi Evra na Suarez, bila kutarajiwa, aligoma kumpa mkono Evra.
October 2012
Alishangilia Goli lake kwa kujirusha
mbele ya Meneja wa Everton, David Moyes, ambae kabla ya Mechi hiyo na
Liverpool alitamka Wachezaji wadanganyifu kama Suarez wnaohadaa Marefa
wanafanya Mashabiki waikatae Soka ya England.
Januari 2013
Alipoza mpira kwa mkono na kufunga Bao
la ushindi kwa Liverpool kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP dhidi ya
Timu ya Daraja la chini Mansfield.
Machi 2013
Akiichezea Nchi yake Uruguay kwenye
Mechi ya Mchujo ya kuwania kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil
Mwaka 2014, Suarez alionekana kumtandika ngumi Beki wa Chile Gonzalo
Jara bila Refa kuona.
FIFA wanachunguza tukio hili.
RATIBA- BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE:
Jumatatu Aprili 22
[Saa 4 Usiku]
Man United v Aston Villa
MSIMAMO==BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
NA | TIMU | P | GD | PTS |
1 | Man Utd | 33 | 40 | 81 |
2 | Man City | 33 | 29 | 68 |
3 | Arsenal | 34 | 30 | 63 |
4 | Chelsea | 33 | 31 | 62 |
5 | Tottenham | 33 | 17 | 61 |
6 | Everton | 34 | 13 | 56 |
7 | Liverpool | 34 | 19 | 51 |
8 | West Brom | 33 | -1 | 45 |
9 | Swansea | 33 | 1 | 42 |
10 | West Ham | 34 | -7 | 42 |
11 | Fulham | 34 | -8 | 40 |
12 | Southampton | 34 | -7 | 39 |
13 | Norwich | 34 | -20 | 38 |
14 | Sunderland | 34 | -7 | 37 |
15 | Stoke | 34 | -11 | 37 |
16 | Newcastle | 34 | -17 | 37 |
17 | Aston Villa | 33 | -24 | 34 |
18 | Wigan | 33 | -23 | 31 |
19 | QPR | 34 | -27 | 24 |
20 | Reading | 34 | -28 | 24 |
YANGA INANAFASI KUBWA KUTWAA UBINGWA POINT 1 TU
Vinara wa ligi kuu vodacom tanzania bara yanga sasa imefikisha pointi 56 baada ya kuitandika bao 3-0 Jkt ruvu wakifuatiwa na Azam FC wenye Pointi 47 na waliobakisha Mechi 3.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
MECHI WALIZOBAKISHA YANGA:
Mei 1: YANGA v COASTAL UNION [UWANJA wa TAIFA]
Mei 18: YANGA v SIMBA [UWANJA wa TAIFA]
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Lakini ikiwa Azam FC watatoa sare au
kufungwa Mechi yao inayofuata huko Mkwakwani hapo Aprili 27 dhidi ya
Coastal Union, basi Yanga watachukua Ubingwa bila ya kucheza Mechi yao
inayofuata.
RATIBA:
Jumatano Aprili 24
African Lyon v JKT Ruvu
Alhamisi Aprili 25
Simba v Ruvu Shooting
Jumamosi Aprili 27
Coastal Union v Azam FC
Jumapili Aprili 28
Simba v Polisi Moro
MSIMAMO:
NA | TIMU | P | W | D | L | GD | PTS |
1 | Yanga | 24 | 17 | 5 | 2 | 31 | 56 |
2 | Azam FC | 23 | 14 | 5 | 4 | 22 | 47 |
3 | Kagera Sugar | 23 | 11 | 7 | 5 | 8 | 40 |
4 | Simba SC | 22 | 9 | 9 | 4 | 11 | 36 |
5 | Mtibwa Sugar | 24 | 9 | 9 | 6 | 3 | 36 |
6 | Coastal Union | 23 | 8 | 9 | 6 | 3 | 33 |
7 | Ruvu Shooting | 22 | 8 | 6 | 8 | 0 | 30 |
8 | JKT Oljoro | 24 | 7 | 7 | 10 | -5 | 28 |
9 | Prisons FC | 24 | 6 | 8 | 10 | -7 | 26 |
10 | Mgambo Shooting | 23 | 7 | 4 | 12 | -7 | 25 |
11 | JKT Ruvu | 23 | 6 | 5 | 12 | -18 | 23 |
12 | Toto African | 25 | 4 | 10 | 11 | -12 | 22 |
13 | Police M | 23 | 3 | 10 | 10 | -10 | 19 |
14 | African Lyon | 23 | 5 | 4 | 14 | -19 | 19 |