Tuesday, May 28, 2013

KING KIBADEN MPUTA AANZA KUINOA RASMI SIMBA SC LEO KATIKA UWANJA WA KINESI

KOCHA mpya wa wekundu wa msimbazi simba sc alhaj abdallah athumani seif "King kibaden mputa" leo asubuhi ameanza rasmi kazi ya kuinoa timu hiyo katika uwanja wa kinesi Urafiki jijini Dar es salaam.

Kabla ya kuanza usaili Kibadeni alianza kutoa mazoezi kwa wachezaji wa simba mara baada ya hapo usaili ukafuata kwa wachezaji waliojitokeza kuomba kusajiliwa katika timu hiyo.

Kibadeni ataanza  rasmi leo na atasaini mkataba kesho ikumbukwe kibadeni alikuwa akiifundisha Kagera Sugar ambapo katika msimu uliomalizika wa ligi kuu vodacom tanzania bara ameiwezesha Kagera Sugar kushika nafasi ya nne ikiwa na jumla ya point 43.

aidha ikumbukwe kibadeni amechuwa nafasi ya mfaransa patric liewig alitupiwa virago clubuni hapo baada ya kuyashindwa maisha ya msimbazi.

hivyo kwa sasa simba itakuwa chini ya kocha mkuu king kabadeni mputa akisaidiwa na jamhuri kihwelu julio pamoja na suleimani abdallah matola.

WASIFU WA KING KIBADEN
1949- Oktoba 11; Alizaliwa Mbagala Kiburugwa Dar es Salaam.
1959- Alitungwa jina Kibadeni na watoto wenzake kutokana kucheza soka ya nguvu akiwa mdogo na mfupi, ambalo limefunika jina lake halisi la Abdallah Athumani Seif. Mwenyewe anasema Kibadeni maana yake ni kitu cha baadaye. Kwamba kila siku alikuwa akionekana bado kwa umri na umbo wakati anaweza soka.
1969- Februari 2; Alijiunga na Simba SC ikiitwa Sunderland akitokea Kahe Republic ya Mtaa wa Kongo na Mchikichi, Kariakoo.
1974- Alifunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Hearts Of Oak ya Ghana nchini Ghana katika Robo Fainali ya Kwanza ya Klabu Bingwa Afrika.
1974- Aliiongoza Simba kuwa klabu ya kwanza na pekee Tanzania kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika hadi sasa.
1975- Aliiongoza Simba kuwa klabu ya kwanza kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Dar es Salaam.
1977- Alifunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Yanga SC.
1993- Aliiwezesha Simba SC kufika Fainali ya Kombe la CAF akiwa Kocha, rekodi ambayo haijavunjwa hadi leo ikiwa ni miaka 20 baadaye
1978-Aling’atuka Simba SC na kwenda kuwa kocha mchezaji Majimaji ya Songea.
2011- Alikwenda Hijja.